Kilimo kinahitaji uwekezeji mkubwa ili uone faida

Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Kwanini chainsaw hairuhusiwi Tanzania mkuu? Maana madukani zipo na zinauzwa kihalali kabisa.
 
Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Acha kupotosha. Mi namiliki chainsaw Husqavarna 272 made in Brazil na zinauzwa maduka mengi tu pale mnara wa saa Dar es salaam au samora avenue. Na mafundi wanaziwasha mchana kweupe kuzitengeneza tena wanatengenezea nje kabisa.

Hata hapa mjini Dsm tumeenda kukata miti ya minazi na kucharanga mbao jirani kabisa na kituo cha polisi Sitakishari ina maana polisi walisikia inaanguruma na sio siku moja kama masaa 6 kwa siku.

Kama huna uhakika na kitu kaa kimya bro. Usilte story za vijiweni.
Mi mkulima nina shamba eka lina miti kibao. Unadhani unasafishaje ile miti yote mikubwa. Kile ni kitendea kazi.

Ni sawa kusema tusitumia ng'ombe wanaumia au tunawatesa tutumie jembe tu la mkono nikifananisha.

Usidhani serikali haina macho au imejaa wajinga.

Kuna taratibu za kutumia chainsaw

Usiseme Tanzania. Sema huko kwenu.
 
Nazungumzia reality.
Karibu asilimia 90 au zaidi ya watanzania wana angalau ndugu anayeishi kwa kutegemea peasantry. Wazazi wangu pia wamesomeshwa na kukuzwa na kilimo hicho kidogo.
Ila hali yao kimaisha ilikuwa ya tabu sana na ni hali ambayo siyo lengo la mwanadamu kuishi hasa wakati huu. Kwa hiyo kuendelea na kilimo kidogo hakutainua hali ya maisha ya mtanzania au binadamu kwa ujumla.
Kilimo inatakiwa kiwe kikubwa na kiwe industrialized ili wananchi waweze kunfaika either directly au indirectly. Otherwise wewe utakuwa unapiga hatua mbili mbele na mbili nyuma at the same time.
Hayo mambo ya ubinafsi wangu sijui nini, sidhani kama nina muda au haja ya kujadili.

Kuhusu serikali kutengeneza mazingira, hizo ni ndoto za alinacha ambazo zimepandikizwa vichwani mwenu. Haitatokea serikali itakayokutengenezea mazingira bila wewe kutengeneza mazingira ya serikali kukutengenezea mazingira.

Labda serikali za Ulaya na America ziwatengenezee mazingira, na watakuomba usiwafokee tafadhali.
 
Mimi ni mkulima wa miti ya mbao. Nakueleza kitu cha uhakika. Kama unapinga muulize Afisa misitu ili upate ukweli. Aidha uliza watu wa kutoka Moshi wakueleze kuwa mlio tu wa chain saw ni hatari mpaka watu wanawashia ndani ya ndoo.
 
Sijui umemwandikia nani huu uzi . Kama ulivyosema kilimo ni gharama. Mtu anayeweza kulima heka 20 ni tajiri. masikini halimi ekari 20
Nilijaribu keka 9 nilijuta, za mpunga
nikaambulia kiduchu
 
#39 SIO JIBU

Nivyema ukakubali ulitekosea/kurupuka.

Statement 'Chainsaw haziruhusiwi Tz' na kile unachokiandika hakina uhusiano hata kidogo.

Unasema hairuhusiwi then unaleta habari uwe na vibari blaablaa hii ndio maana ya kutokuruhusiw.

Unajua ni maana ya 'kitu kutoruhusiwa nchini'

We are matured enough bro.
 
Mimi ni mkulima wa miti ya mbao. Nakueleza kitu cha uhakika. Kama unapinga muulize Afisa misitu ili upate ukweli. Aidha uliza watu wa kutoka Moshi wakueleze kuwa mlio tu wa chain saw ni hatari mpaka watu wanawashia ndani ya ndoo.
Uzi unahusu kukata mbao, it seems unatumia nguvu kuhamisha mada just kulisha hoja zako dhaifu.
 
Acha kuleta story zako za kuambiwa hizo...
Kwani kazi ya chainsaw ni kuchana mbao tu!?
Ukienda moja kwa moja kwenye hoja ya mtoa uzi, alimaanisha kwa ajili ya kusafisha shamba. Sio mbao kama unavyowaza wewe.
Alafu nikupe elimu kidogo kwa faida yako, chainsaw zinahitaji kibali kwa baadhi tu ya maeneo nchini. Nenda Songea, Iringa, Njombe, Lindi, nk. Hakuna hizo issue za kibali.
Pia, kitu kinachohitaji uwe na kibali kukimiliki, haimaanishi serikali hairuhusu kumiliki.
 
Mimi ni mkulima wa miti ya mbao. Nakueleza kitu cha uhakika. Kama unapinga muulize Afisa misitu ili upate ukweli. Aidha uliza watu wa kutoka Moshi wakueleze kuwa mlio tu wa chain saw ni hatari mpaka watu wanawashia ndani ya ndoo.
Usiseme Tanzania ndugu Afisa misitu hata huku wapo mbona unakuwa mtu wa ajabu kwani kuna serikali ngapi. Mi nalima kisarawe. Tuambie wewe uko wapi kwenye sheria za ajabu.

Serikali inaruhusu hata bunduki raia kumiliki itakuwa chainsaw.

Hata kijijini ninakolima kuna kamati ya ulinzi na kamati ya misitu. Na kuna maeneo unalipa ushuru serikali ya vijiji na unaonyeshwa eneo unalipia unavuna miti na risiti ya serikali unapewa.

Hata pale njombe raia wana mashamba ya miti ikiisha iva wanatumia chainsaw kuvuna.

Unazungumza vitu vya ajabu sana ndugu yangu. Sio kweli jielimishe.

Kuna mikoa hizo mashine zimebanwa lakini sio kote.

Kama zimepigwa marufuku unadhani wale wenye maduka wamgezining'iniza nje namna ile kama midoli.

Wewe unaleta porojo za vijiweni hapa halafu kwenye mada kama hii unapotosha jamii.
 
Mi nishawah kufanya kilimo aiseee pesa ilinitoka kinyama , uzuri nilipoivisha nikauz nikapata pesa nyingi Kwa mkupuo nikakimbia kabisa Pori Ila nitarudi tena ...!! Kilimo bila pesa ni ngumu kuchomoka
 
Mi nishawah kufanya kilimo aiseee pesa ilinitoka kinyama , uzuri nilipoivisha nikauz nikapata pesa nyingi Kwa mkupuo nikakimbia kabisa Pori Ila nitarudi tena ...!! Kilimo bila pesa ni ngumu kuchomoka
Ha ha ulilima nini bro Slowly mi bado nimekomaa
 
Mkiwa nje mnaota ndoto za mchana kwa kutheorize fanya utafiti kwanza kabla ya kuandika. Kwa taarifa yako chainsaw hairuhusiwi hapa Tanzania
Kumbe siku hizi kumiliki chainsaw ni kama kumiliki silaha ya moto bila kibali!!!!? Kweli maendelea acha tuyaone kwa wenzetu.
 
Tufikirie jinsi ya kutatua hili. Manaweza kucha ga pesa watu watano katika Wilaya moja mkanunua trekta na kila mtu akalitumia kwa wiki moja msimo wa kilimo.
Trekta si kama mil 30 kwa watu watano watachanga kila mtu 6m,😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…