Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Wasomi wengi hawawezi kujiingiza kwenye kilimo. Kwanza ndio wanaongoza kwa kuogopa risk lakini pili wanataka white color jobs, tatu wanataka kutumikia elimu yao kama ilivyowaelekeza (kuajiriwa tuu) na nne wanataka assurance zaidi kwamba hata kama usipoenda kazini aidha kwa kuumwa au tatizo jingine unalipwa. Tuwaache asiyoenda shule waendelee na watuajiri.
 
Ashakum si matusi,
Lakini unapoamua kuwatukana watu waziwazi.........unatupa wasiwasi........
Ekari 2 za mahindi mauzo yawe Mil.3 ???
Hebu tujuze kwenye Ekari 2 ulipata magunia mangapi?
.....
Halafu shamba ulisafisha kwa bei gani?
Kulima ni sh'ngapi?
palizi?
Dawa?
gharama za kuvuna?
Kupukuchua?
Gharama za usafiri kwenda shamba? (angalau kwa uchache gharama hizi hazikwepeki).Mbolea?? mfuko ulinunuaje? USD/Tsh.?
 
Mada inatoa ushaur kwa mwanafunz akimaliza chuo anaweza kujiajir kwenye kilimo.
Atajiajiri vip bila kuwa na initial capital?

Usikurupuke kama ulisoma rudi kafunue upya daftar zako na pitia sehemu ambayo mwalimu wako aliweka alama ya vema kama hakuna
Unaweza kwenda qt.

Kama ulisoma mambo ya kicheketile tuuu hapo sawa maana unajifunza na kuamin kwenye maneno ya watu wakale na sio hali ya sasa
Nenda kwa balozi wako atakupa elimu ju uwezaji na biashara
Kila kilimo sio lazima ukakope, hivi kijana aliyemaliza chuo kikuu atashindwa kupata laki 5 akaanzisha kilimo, mimi nakumbuka kipindi nipo chuo nilikuwa natunza pesa kila boom nimemaliza nina zaidi ya milioni moja.
 
Nimesoma Kilimo na kitu kimojawapo nilichofundishwa ni kuwa kilimo kina risks nyingi sana kuliko biashara nyingine zote. Ndio maana hata benki ziko reluctant sana kukopesha wakulima. Sema tu ikitokea usikumbane dhahama utaona ni biashara nzuri sana.

Mfano mvua inaweza kugoma kunyesha, unaweza kuibuka ugonjwa au wadudu wa zao ulilolima au kukatokea price fluctuation kubwa sana ya mazao, hivyo ukauza kwa hasara. Kwa hivyo si sahihi kabisa kusema eti ina faida asilimia 100.
 
Umeelezea zaidi mshahara wa watu kuliko mchanganuo wa project zako...garama za kukodi shamba, kulima mara ya kwanza, gharama za mbegu na aina ya mbegu, garama za upandaji, garama za palizi ya kwanza may be na ya pili, gharama za kuhudumia wadudu kama zilikuwepo, gharama za uvunaji, gharama za kupiga mahindi, udadi ya gunia ulizopata kwa ekari moja! Bei uliouzia na mwezi uliouza,....wakulima ndio tunaongea hivi.
 
Ashakum si matusi,
Lakini unapoamua kuwatukana watu waziwazi.........unatupa wasiwasi........
Ekari 2 za mahindi mauzo yawe Mil.3 ???
Hebu tujuze kwenye Ekari 2 ulipata magunia mangapi?
.....
Halafu shamba ulisafisha kwa bei gani?
Kulima ni sh'ngapi?
palizi?
Dawa?
gharama za kuvuna?
Kupukuchua?
Gharama za usafiri kwenda shamba? (angalau kwa uchache gharama hizi hazikwepeki).Mbolea?? mfuko ulinunuaje? USD/Tsh.?
Kila ekari mbili nimepata gunia 37, nikauza gunia 35×@90,000/=.
Gharama za kulima
Mbolea mifuko 2 @61,000/=
Mahindi kg 20=100000/=
Palizi =140000 ya kwanza na pili
Kupukuchua gunia moja ni shilingi 1500×37=52500
Gharama ya kupanda nilitumia 20000 na nguvu kazi ya nyumbani.
 
Mkuu bado sikuelewi kuna gharama za kulima,ulitumia trekta? au ng'ombe au mikono?
Na hiyo mbolea ni ya kupandia au ya kukuzia?
Pia kuna gharama za kuvuna na pia nauli au usafiri wa kwenda shamba,toka umeanza kulima mpaka kuvuna.
Achilia mbali gharama ndogo ndogo kama vile magunia au viloba.
USIFANYE MCHEZO
WEWE SI MKULIMA.nenda yanapolimwa mahindi uone.
gunia 37 kwa ekari....???? labda uwe umelima ndani ya green house.
 
Fanya utafit kwanza ndipo utoe ushaur, japo ushaur wako ni mzur sana
Lakin tuangalie risk katika kilimo tanzania tena kilimo endelevu.
Ni kweli mazao ya chakula soko lake ni lauwakika sana
Ila swali la kujiuliza shortage ya mahid iliyopo maeneo ya mikoa ya kaskazin wakulima wa kusuni ambao wanasuplus ya mahid wataweza faidika na hali hiyo
Je nyanya za dumila, mkulima anaweza faidika na shortage ya nyanya dar.
Kisha waza mtu alie chukua mkopo bank na anatakiwa kulipa na riba, kwa hali kama hiyo ataweza.
Maana utafit unasaidia kupunguza riski, ila kuingia ktk biashara bila utafik na kuangalia flan alipata nin tena kwa kipind kifup ni hatar sana.
Ni vema kujua taarifa za zao utakalo kulilima kama sehemu ya uwekezaji wako kuanzia mazingira ya uzalishaji (inputs) kama chanzo ya maji yako kwa hali ya sasa, usafirishaji, pembe jeo na mambo mengine.
Naunga mkono wazo lako
Hakuna mafanikio bila risk
 
Hiyo ni sawa na hesabu za

Mhindi 1=500tsh
500tsh*100mahindi=50000ths kwa siku
50000tsh*30days=1500000tsh kwa mwezi,

Kilimo kina ujinga wake ukibahatika shukuru
 
Kila kilimo sio lazima ukakope, hivi kijana aliyemaliza chuo kikuu atashindwa kupata laki 5 akaanzisha kilimo, mimi nakumbuka kipindi nipo chuo nilikuwa natunza pesa kila boom nimemaliza nina zaidi ya milioni moja.

Upo sahah sana
Uliweza kutunza mtaj kwa kusave na ulikuwa na chanzo cha kipato ambacho mkupo wa elimu.
Njia za kifaines mradi wako wowote moja ni kutoka kwenye hakiba yako, pili ni kukopa kutoka vyanzo vya nje.
Kama mradi wako unafaida ukiangalia projected cash flow yako unaweza upata mkopo popote
Na kama unaogapa hilo wewe sio mjasiria mali.
Maana ukikopa na kuwekeza unaweza lipa deni na kukuza biashara yako kama uliweza kutumia muda na akili yako kwa kuangalia kubadilika kwa soko kwa bidhaa yako.
Unapo toa ushaur wa uwekezaji kuanzia level ya familia, kijij, wilaya mkoa hata taifa lazima ueleze njia za kuwezesha mradi wako.
Tafuta wataalam wakueleweshe vema ili utimize lengo lako maana ni lengo zuri sana kwako na watanzania kwa ujumla
Na mafanikia yako yatakuwa ni shule kwa wengine pia
Weng watapenda jifunza kwako uwez waambia mi nilianza tuu had leo najikuta napata faida kubwa itakuwa ujawasaidia.
 
Hakuna mafanikio bila risk

Ndio maana watu hufanya utafiti ili kupunguza risk na sio kukurupuka Sio kila sehemu unaweza jenga hotel kisa jiran kajenga hotel anapata faida. Watafute wachumi wakupe elimu ya uwekezaji na risk management au watu wa insurance na risk management watakusaidia kupunguza risk kama umekuwa mvivu wa kufanya utafiti mdogo wa soko la kitu utakachotaka kufanya.

Kumbuka wavivu na wajinga hupenda ushauri wa wanganga hata kwa kupewa masharti ya mateso na hawataki ushauri wa wataalam na kujiongezea knowledge ya kitu anachokifanya. Nenda SUA utapewa elimu ya kilimo na watu waliofanikiwa na kilimo na nini walikifanya
 
Mkuu bado sikuelewi kuna gharama za kulima,ulitumia trekta? au ng'ombe au mikono?
Na hiyo mbolea ni ya kupandia au ya kukuzia?
Pia kuna gharama za kuvuna na pia nauli au usafiri wa kwenda shamba,toka umeanza kulima mpaka kuvuna.
Achilia mbali gharama ndogo ndogo kama vile magunia au vilob.
USIFANYE MCHEZO
WEWE SI MKULIMA.nenda yanapolimwa mahindi uone
gunia 37 kwa ekari....???? labda uwe umelima ndani ya green house.
Kulima nilitumia ng'ombe zangu, ila kama ningelinunua basi gharama yake isingelizidi 80,000/= mbolea niliweka ya kupandia tu, nililima ekari mbili sio moja.
 
  • Thanks
Reactions: B40
Watanzania wengi wanaishi vijijini na shughuli yao kubwa ya kiuchumi ni kilimo, karibu theluthi moja ya watanzania ni masikini na sehemu kubwa ya theluthi hii wanaishi vijijini ambako shughuli kubwa ya uchumi ni kilimo.
 
Fanya utafit kwanza ndipo utoe ushaur, japo ushaur wako ni mzur sana
Lakin tuangalie risk katika kilimo tanzania tena kilimo endelevu.
Ni kweli mazao ya chakula soko lake ni lauwakika sana
Ila swali la kujiuliza shortage ya mahid iliyopo maeneo ya mikoa ya kaskazin wakulima wa kusuni ambao wanasuplus ya mahid wataweza faidika na hali hiyo
Je nyanya za dumila, mkulima anaweza faidika na shortage ya nyanya dar.
Kisha waza mtu alie chukua mkopo bank na anatakiwa kulipa na riba, kwa hali kama hiyo ataweza.
Maana utafit unasaidia kupunguza riski, ila kuingia ktk biashara bila utafik na kuangalia flan alipata nin tena kwa kipind kifup ni hatar sana.
Ni vema kujua taarifa za zao utakalo kulilima kama sehemu ya uwekezaji wako kuanzia mazingira ya uzalishaji (inputs) kama chanzo ya maji yako kwa hali ya sasa, usafirishaji, pembe jeo na mambo mengine.
Naunga mkono wazo lako
90% ya miradi hushindwa kabla haijaanza kutekelezwa
 
Mkuu kilimo nachoongelea hapa sio cha kwenda kuchukua mkopo benki, hoja yangu unawagusa zaidi vijana wahitimu wanaosubiri ajira ambao watafanya kilimo cha kawaida.
Sio rahisi kueleweka, wenzio wanawazia kilimo cha kwenye internet. Wanatazama mashamba makubwa ya wazungu, halafu wanataka nao waanze hivyo, wakati hata mahindi yenyewe wanayaona tu kwa wachomaji mjini!! Ukiwaambia ekari moja wataanza ooh, research, mara ukame, mara masoko sijapata n.k. Wanashindwa kabla hawajaanza
 
Watanzania wengi wanaishi vijijini na shughuli yao kubwa ya kiuchumi ni kilimo, karibu theluthi moja ya watanzania ni masikini na sehemu kubwa ya theluthi hii wanaishi vijijini ambako shughuli kubwa ya uchumi ni kilimo.
Ni kweli lakini ujue kwamba watanzania wengi wanafanya kilimo duni, hawalimi kisasa na wengi hulima kwa ajili ya ya chakula cha familia, ukilima kibiashara utafanikiwa na kupata mtaji wa kuanzisha biashara nyingine, lakini ujue kwamba watu wengi hawana elimu ya matumizi sahihi ya pesa, mfano kuna vijana nawajua walilima viazi wakauza pesa nyingi sana lakini sasa hivi hawana hata mia, mkulima anajua baada ya miezi minne atapata tena.
 
Kweli unachokisema. Ila zipo changamoto kubwa na nyingi kwa vijana.

Siyo kwamba hatutaki kilimo laa!
Hali ya hewa ni nzr kwa baadhi ya mikoa tu. Mf Mbeya, Iringa na Bk.

Mikoa iliyo baki ni kiangazi.
Mm ombi langu kwa serikali ni kujenga mifumo ya umwagiliaji nchi nzima.

Tusitegemee mvua ya God. Tutalima mara 2 au 3 kwa mwaka.

Lakini wao kipaumbele ni viwanda vya mbolea na madawa (madili yao) sijui nani kawambia ardhi zetu hazina rutuba?
Samadi imejaa kila mahala.

Kilimo cha sasa kinahitaji kiwe cha kisasa na Large scale kulisha nchi nzima. Coz vijana wote wako town wanaokota makopo na kuuza mifuko ya 100. Hovyo mtaji wa Trekta ni mhimu sn. Mikopo Benki hailipiki. Riba 19% to 24% utafungwa buree.

Serikali ikiweka mazingira vzr na miundombinu rafiki hata mm nategemea kuwa mkulima.
 
Back
Top Bottom