Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Mwanafunzi wa chuo anaweza kujipanga mwenyewe kabisa, ila ubaya ni kwamba watu wengi hatuna kitu kinacho itwa "saving culture" tunategemea mwisho wa siku tutapewa au tutaomba kila kitu.

Tuchukulie mfano wa kijana aliyejitambua na mwenye malengo thabiti kabisa. Anapo anza mwaka wa kwanza akaweza kuhifadhi 50,000 kwenye pesa yake ya kujikimu kila mwezi ndani ya miezi minne kijana huyo atakuwa na 200,000 na akiendelea kufanya hivyo kwa miaka mitatu atakuwa na 600,000 kama pesa hii itakuwa alikuwa akiiweka fixed account kwa bank kama Azania wana account unayo weza kuongeza pesa kila mwezi ila ina act kama fixed account.

Pesa hii baada ya miaka mitatu itakuwa mtaji wa kutosha kabisa kwa kijana kuanza maisha na sio lazima kijana huyo aweke 50,000 ila anaweza weka kiwango chochote anacho ona hakita haribu matumizi yake ya kila siku.

Ila kwasababu hatuna desturi ya kuthamini vidogo tulivyo navyo inatusumbua sana baadae tunaanza kulalamika ajira hakuna, mitaji hakuna, serikali hithamini vijana.

Cha msingi hapa ni vijana tuelewe kwamba kabla ya kunyoosha vidole kwa watu wengine na kusema hatujasaidiwa, sisi tumechukua hatua gani ya kujisaidia.??
Umeongelea point ya msingi sana ndugu,,, mi hua najiuliza sikupata bahat ya kusoma na nipate boom,,lakin nilijichanganya kwa msingi wa [coloe=red] 8000[/color] na nikafanikiwa kila kitu,,mpak sasa naweza ajiri zaid ya watu 40 na zaid unashindwaje unaepata mkopo ambao unaweza kuutumia ukafanikiwa kabla hata hujamaliza chuo???
 
iko siku utakuja hapahapa kutuambia hakuna biashara mbaya kama ya kilimo note me kila jambo na wakati wake kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia
Kama unajua kila jambo lina wakati wake wa kulia na kucheka hata ilo unaloona wewe ni zuri litakuwa na muda wa kucheka na kulia.Sasa inakuaje useme kilimo biashara hakifai wakati unajua kila jambo lina muda wa kulia na kucheka kama hilo unaloona wewe ni bora nalo lina muda wa kulia na kucheka.

Acha kukatisha watu tamaa,kilimo kinalipa kuliko chochote.
 
Nimesoma Kilimo na kitu kimojawapo nilichofundishwa ni kuwa kilimo kina risks nyingi sana kuliko biashara nyingine zote. Ndio maana hata benki ziko reluctant sana kukopesha wakulima. Sema tu ikitokea usikumbane dhahama utaona ni biashara nzuri sana. Mfano mvua inaweza kugoma kunyesha, unaweza kuibuka ugonjwa au wadudu wa zao ulilolima au kukatokea price fluctuation kubwa sana ya mazao, hivyo ukauza kwa hasara. Kwa hivyo si sahihi kabisa kusema eti ina faida asilimia 100.
Rudi tena darasani,una mawazo ya zamani sana.Kilimo cha kisasa hakiendeshwi kihivyo.
 
Kuna watu wapo busy kuhangaika kutafuta ajira serikalini na mashirika binafsi, wengi hufikiri kuwa wanaweza kutoka kwa kuajiriwa, vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo aidha wanafikiri kuwa kilimo hakilipi na wajanja waliopo huko hawawambii wenzao kuwa kilimo kinalipa.

Nitoe ushuhuda kidogo mwezi wa 9 mwaka jana nimelima ekari mbili gharama haikuzidi laki 5 lakini nimeuza mahindi hayo zaidi ya milioni 3. Na bado mengine nikaacha kwa ajili ya chakula, hebu fikiria sasa ni biashara gani ya laki tano ambayo unaweza ifanya kwa mtaji wa laki tano ukapata mil 3 kwa muda wa miezi 4 kwa kifupi haipo.

Mishahara mingi ya waajiriwa wenye shahada ni 450,000/=(kwa wale wenye mikopo) na 560,000/= kama huna mkopo, sasa tufanye hesabu fupi tuchukulie uhalisia kwamba vijana wengi wamesoma kwa mkopo, 450,000 ukilipia nyumba, umeme, maji na matumizi mengineyo unajikuta haifiki tarehe kumi tano unaanza kukopa tena, lakini ukichukua 450,000×12 =5,400,000/= kwa mwaka mzima, hii pesa kwa mkulima ni msimu mmoja tena huyo ni mkulima mdogo kabisa na kwa mwaka kuna misimu miwili.

Ushauri wangu kwa vijana tujaribu kuwekeza kwenye faida yake ni kubwa lakini pia kilimo ni mradi endelevu, idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo mahitaji ya chakula ni mengi kuliko idadi ya watu.
Usijekulia hapa msimu ujao. Ndio maana nchi nyingine zine taratibu za compensate wakulima pale natural disaster inavyo hit.
 
Kweli jembe halimtupi mkulima kama tu utakuwa serious na kilimo, mbegu bora n.k
Hapa nina bustani yangu home ina mchicha, sukuma wiki, kitunguu, maboga, matembele, nyanya chungu, bamia, mahindi...Nina mwezi sasa safari za sokoni zimepungua labda nifate nyama na samaki. Sina stress ya mboga hata kama sina hela...
soon napanda viazi, na wateja wa mboga wameshaanza kupiga hodi. Mdogo mdogo tu nitafika. Miaka mitatu baadae nitakuwa mkulima mkubwa tu...i believe!
 
Ashakum si matusi,
Lakini unapoamua kuwatukana watu waziwazi.........unatupa wasiwasi........
Ekari 2 za mahindi mauzo yawe Mil.3 ???
Hebu tujuze kwenye Ekari 2 ulipata magunia mangapi?
.....
Halafu shamba ulisafisha kwa bei gani?
Kulima ni sh'ngapi?
palizi?
Dawa?
gharama za kuvuna?
Kupukuchua?
Gharama za usafiri kwenda shamba? (angalau kwa uchache gharama hizi hazikwepeki).Mbolea?? mfuko ulinunuaje? USD/Tsh.?
Eka mbili kwakweli sio rahisi kuzalisha M3, Labda kama mavuno yake yamegongana na msimu wa njaa kali katika eneo lake au labda kama ameongeza thamani.
 
Sidhani
Nimekulia kwenye familia za kulima mboga mboga ila mpaka leo tuko masikini
 
Kujifanya mnajua research sana ndo kunawafanya muwe maskini. Watu wanaongelea ushuhuda bado unataka afanye research tena theoretically??? Ili approve nini wakati tayari ameshafaya pratically??

Tatizo letu vijana tunakuwa sio risk takers! Na lazima tujue the mkre risk you take the more reward you are likely to get!

Sasa mkikutana na waoga kama jawa wanaoogopa kuthubutu na mkawasikiliza mtajikuta mnazeeka maskini na sio katika kulima tu, katika kila biashara watu wa namna hii wapo. Mtu anakwambia mimi nina boda boda yangu na napiga hela kiasi flan kwa mwezi, badalaya kumuuliza unafanye upate hela kama hiyo unaanza kumwambia pikipiki nikinunua itapata ajali! Hawa watu wa type hii ni wa kupuuzwa kabisa!

Mimi nawahakikishia hela ipo kwenye kilimo na ni uhakika sana. Ukichemka msimu wa kwanza msimu ujao unatusua. Cha msingi ni kuwauliza wanaofanikiwa wanapitia njia zipi na sio kuwaambia ukilima mazao yatakauka mvuahaitanyesha.

Achamaneno andaa shamba alafu uvune tuone yakikosa soko sasa!

Na kuunga mkono.
 
Si kila mtu anaweza kufanya kilimo akafanikiwa, unatoa ushauri kwa sababu wenda una utaalamu na uzoefu wa hiyo shughuli sio kila mtu atamudu kilimo kama mbadala wa ajira kama unavyofikiria, umetoa mchanganuo mzuri ila ni vizuri ukaleta na changamoto zake ili kuepusha watu kuingia katika hicho kilimo wakiwa uninformed au misinformed, kuliko kufikiri kuwa aliyesoma IR alime aliesoma PR alime, aliyesoma HR alime, tuwe makini kidogo
 
Ni kweli lakini ujue kwamba watanzania wengi wanafanya kilimo duni, hawalimi kisasa na wengi hulima kwa ajili ya ya chakula cha familia, ukilima kibiashara utafanikiwa na kupata mtaji wa kuanzisha biashara nyingine, lakini ujue kwamba watu wengi hawana elimu ya matumizi sahihi ya pesa, mfano kuna vijana nawajua walilima viazi wakauza pesa nyingi sana lakini sasa hivi hawana hata mia, mkulima anajua baada ya miezi minne atapata tena.

Mkuu naomba namba yako PM. Nahitaji mbegu ya viazi mviringo hata ikibidi na mashamba ya kukodi kuanzia heka kumi na kuendelea
 
Mwaka Jana nimelima heka moja ya vitunguu na jumla gharama nilitumia 1,700,000/= nikafanikiwa kupata gunia 72 ambayo kila gunia niliuza kwa 90,000/= sawa na tsh 6,480,000/= ukitoa gharama zangu unapata baki ya tsh 4,780,000/= Nilipotoa gharama zangu zote nyingine kama usafiri na chakula nilipokuwa shamba nikabakiwa na 4,300,000/= Nilitumia miezi minne mpaka kuvuna na approximation ni kama kila mwez niliingiza 1 million. Ni kiasi kidogo na ni kikubwa pia.
Tujifunze kuwekeza shambani

Wapi huko ulilimia? Gharama zinaonekana nafuu
 
Acha umama wewe. Huyu amefanya na akapata matunda haongelei theory kujifanya wachambuz ndo kunatuponza kama taifa. Shwaini

Furaha ya mjinga ni kutoa matusi nakujipongeza ujinga wake unaotokana iman zakusadikika na sio kujifunza.
Kilimo ni sayansi na sio mazoea, nenda kasome upya sehemu ambazo mwalim wako akiweka alama ya vema na kama hakuna kafundishwe tena. Elimu haina mwisho
 
Jamani ki ukweli kilimo kinalipa.

Cha msingi unatakiwa kujua ulime nini na wakati gani

Kuna rafiki yangu amelima vitunguu amevuna heka moja kapata gunia 113 na ameuzia shambani kwa 90,000

113 X 90,000 = 10,170,000

Gharama alizotumia ni kama 3M

Amenipa machungu sana kiasi kwamba nimeamua kuacha kazi ili ni base kwenywe kilimo ili nikabikiane na changamoto ambazo nakutana nazo kwenye kilimo
 
Yaani watu wanapotishana kwenye mitandao humu,toa mchanganuo ulilima wapi,kilimo cha kutegemea mvua au kumwagilia,ulipata jumla ya gunia au tani ngapi na uliuza kwa bei gani??,mimi pia ni mkulima wa mahindi nzuri tu ila kwa hekali 2 ukapata mil3 ,mmmhhhh?!???
 
Yaani watu wanapotishana kwenye mitandao humu,toa mchanganuo ulilima wapi,kilimo cha kutegemea mvua au kumwagilia,ulipata jumla ya gunia au tani ngapi na uliuza kwa bei gani??,mimi pia ni mkulima wa mahindi nzuri tu ila kwa hekali 2 ukapata mil3 ,mmmhhhh?!???

Inawezekana kabisa.

Kwa makadirio ya chini tuseme alivuna gunia 30.
Gunia la mahindi kwa sasa ni 100,000 x 30 = 3M

Kitu kingine mtoa uzi amesema yuko Tarime; Tarime mahindi wanauzia [emoji1139]
 
Back
Top Bottom