Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Umeongelea point ya msingi sana ndugu,,, mi hua najiuliza sikupata bahat ya kusoma na nipate boom,,lakin nilijichanganya kwa msingi wa [coloe=red] 8000[/color] na nikafanikiwa kila kitu,,mpak sasa naweza ajiri zaid ya watu 40 na zaid unashindwaje unaepata mkopo ambao unaweza kuutumia ukafanikiwa kabla hata hujamaliza chuo???
 
iko siku utakuja hapahapa kutuambia hakuna biashara mbaya kama ya kilimo note me kila jambo na wakati wake kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia
Kama unajua kila jambo lina wakati wake wa kulia na kucheka hata ilo unaloona wewe ni zuri litakuwa na muda wa kucheka na kulia.Sasa inakuaje useme kilimo biashara hakifai wakati unajua kila jambo lina muda wa kulia na kucheka kama hilo unaloona wewe ni bora nalo lina muda wa kulia na kucheka.

Acha kukatisha watu tamaa,kilimo kinalipa kuliko chochote.
 
Rudi tena darasani,una mawazo ya zamani sana.Kilimo cha kisasa hakiendeshwi kihivyo.
 
Usijekulia hapa msimu ujao. Ndio maana nchi nyingine zine taratibu za compensate wakulima pale natural disaster inavyo hit.
 
Kweli jembe halimtupi mkulima kama tu utakuwa serious na kilimo, mbegu bora n.k
Hapa nina bustani yangu home ina mchicha, sukuma wiki, kitunguu, maboga, matembele, nyanya chungu, bamia, mahindi...Nina mwezi sasa safari za sokoni zimepungua labda nifate nyama na samaki. Sina stress ya mboga hata kama sina hela...
soon napanda viazi, na wateja wa mboga wameshaanza kupiga hodi. Mdogo mdogo tu nitafika. Miaka mitatu baadae nitakuwa mkulima mkubwa tu...i believe!
 
Eka mbili kwakweli sio rahisi kuzalisha M3, Labda kama mavuno yake yamegongana na msimu wa njaa kali katika eneo lake au labda kama ameongeza thamani.
 
Sidhani
Nimekulia kwenye familia za kulima mboga mboga ila mpaka leo tuko masikini
 

Na kuunga mkono.
 
Si kila mtu anaweza kufanya kilimo akafanikiwa, unatoa ushauri kwa sababu wenda una utaalamu na uzoefu wa hiyo shughuli sio kila mtu atamudu kilimo kama mbadala wa ajira kama unavyofikiria, umetoa mchanganuo mzuri ila ni vizuri ukaleta na changamoto zake ili kuepusha watu kuingia katika hicho kilimo wakiwa uninformed au misinformed, kuliko kufikiri kuwa aliyesoma IR alime aliesoma PR alime, aliyesoma HR alime, tuwe makini kidogo
 

Mkuu naomba namba yako PM. Nahitaji mbegu ya viazi mviringo hata ikibidi na mashamba ya kukodi kuanzia heka kumi na kuendelea
 

Wapi huko ulilimia? Gharama zinaonekana nafuu
 
Acha umama wewe. Huyu amefanya na akapata matunda haongelei theory kujifanya wachambuz ndo kunatuponza kama taifa. Shwaini

Furaha ya mjinga ni kutoa matusi nakujipongeza ujinga wake unaotokana iman zakusadikika na sio kujifunza.
Kilimo ni sayansi na sio mazoea, nenda kasome upya sehemu ambazo mwalim wako akiweka alama ya vema na kama hakuna kafundishwe tena. Elimu haina mwisho
 
Jamani ki ukweli kilimo kinalipa.

Cha msingi unatakiwa kujua ulime nini na wakati gani

Kuna rafiki yangu amelima vitunguu amevuna heka moja kapata gunia 113 na ameuzia shambani kwa 90,000

113 X 90,000 = 10,170,000

Gharama alizotumia ni kama 3M

Amenipa machungu sana kiasi kwamba nimeamua kuacha kazi ili ni base kwenywe kilimo ili nikabikiane na changamoto ambazo nakutana nazo kwenye kilimo
 
Yaani watu wanapotishana kwenye mitandao humu,toa mchanganuo ulilima wapi,kilimo cha kutegemea mvua au kumwagilia,ulipata jumla ya gunia au tani ngapi na uliuza kwa bei gani??,mimi pia ni mkulima wa mahindi nzuri tu ila kwa hekali 2 ukapata mil3 ,mmmhhhh?!???
 

Inawezekana kabisa.

Kwa makadirio ya chini tuseme alivuna gunia 30.
Gunia la mahindi kwa sasa ni 100,000 x 30 = 3M

Kitu kingine mtoa uzi amesema yuko Tarime; Tarime mahindi wanauzia [emoji1139]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…