Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Duu huyo kijana umempata wapi, maana mimi nina vijana wawili wangalau wanakula kilo moja ya unga kwa siku.

Nilikuwa na vijana sita, walikuwa wapiga kg 30 kwa wiki. Bahati nzuri nilibakisha chakula msimu uliopita
 
Ni kilimo cha umwagiliaji, dharama inategemeana na zao unalotaka kulima alafu pia inategemeana na shamba linatumia maji ya mifereji au ni la kutumia pump

Kama unalima vitunguu shamba kukodi ni shi ngapi?
Iwe kwa ku pump maji au mfereji.
Na je heka moja vitunguu unapata gunia ngapi?
 
Mkuu ni mazao gani ulilima na ulilimia wapi, mbona gharama za nguvu kazi saidizi ni nafuu?
Mkuu nililima Dodoma na nililima mahindi. Mwaka huu kwa sababu ya njaa nguvu kazi bei imepungua palizi ni elfu nane kwa ekari au elfu mbili kwa robo ekari.
 
Mkuu kwa hapa Dodoma bei ya kulima kwa trekta ndo hiyo , na nilima mahindi,.Kama wewe uamini endelea kufanya theoretical research ,'wakati sisi tunafanya practical research. Ubarikiwe sana.
 
Kwenye suala la trekta 25 elf inawezekana.
Kwenye vibarua, bado ninaweza kumuamini japo kwa shida.
Kwenye mbegu hapo mpaka atuambie kwanza ni zao gani na alilimia wapi?
Mkuu nililima mahindi aina ya Stuka huku Dodoma na hizo zilikuwa gharama za mwaka jana, mwaka huu palizi ni sh elfu nane kwa ekari au elfu mbili kwa robo ekari kwa ajili ya njaa ni kubwa sana huku mwaka huu.
 
Wewe unalimia mdomo.😛
Hulijui shamba.
 
Unasemea yule jamaa aliyelima nyanya pale nje ya sevia??
 
Nataka kulima hekari mbili za vitunguu mwaka huu,,wapi kwenye ardhi nzur washkaji nije niweke kambi hapo???
 
hivi kwanini nyie wakulima huwa mnapoleta mafanikio yenu mnapenda sana kuwataja kwa kebehi vijana wanaotafuta ajira...?

na kwa nini uamini sehemu pekee ya kupata faida ni kilimo pekee, na wala sio shughuli zingine,mfano uchimbaji wa madini, uvuvi, biashara n.k...

kingine jarbu kufikilia kila mwaka kuna waitumu zaidi ya laki moja hao ni graduate, bado kuna vijana wa diploma na form six leaver wale wanaoshindwa kuendelea na masomo, Wote hao waende kwenye kilimo kama unavyoelekeza...!wewe unadhani utapata hyo faida ya m3., au utamuuzia nani??
 
Mtanzania akifanikiwa huwa anakaa kimya ili aendelee kupiga hela mwenyewe na baadaye aonekane wa maana kuliko wengine. Ukimsikia m'bongo analeta ngonjera za hivi ujue anafanya utafiti, nia na madhumuni anataka asikie wengine wanasema nini kuhusu wazo lake.
 
Ni kweli usemayo mkuu, lakini mbona wakulima ndio jamii masikini kabisa humu nchini kama kweli inalipa kihivyo?
kua mkulima na kufanikiwa kupitia kilimo ni vitu viwili tofauti sana na usije kuvichanganya tena kiongozi
 
hahahahaha angalia usije fuga hao samaki nao wakadumaa
 
Wewe unalimia mdomo.😛
Hulijui shamba.
Ha ha haaaaaa, mkuu umenikumbusha jamaa yetu mmoja alikuwa analimia mdomo kwamba mwakani nitalima ekari 5 za mpunga kila ekari nitavuna magunia 30 hivyo nitakuwa na maguni 150 ya mpunga. Hapo nitakuwa nimetoka kimaisha!! mwaka ukafika hata nusu ekari hana msimu wa kilimo ukaisha tusione hata shina moja la mpunga jamaa akabaki anatutishia kutupiga tu kila tukimkumbusha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…