Kilio Cha tozo za miamala ni ushahidi kuwa wananchi wanakaribia kuzisahau tofauti zao za kisiasa dhidi ya maisha Yao.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wanasiasa someni alama za nyakati, kaeni chonjo saa mbaya. Tozo kubwa kwenye miamala ya simu imekwenda kufuta mstari muhimu sana kwa wanasiasa unaowatenganisha watanzania kwenye itikadi za vyama vyao vya siasa. Hakuna wanaCCM wala wapinzani kwenye tozo za miamala ya simu. Hii sio ishara njema kwa wanasiasa wa makundi (divide and rule).

wanaCCM tumewazoea wakiimba iyenaiyena hata pale nchi Yao inapoporwa na wanasiasa wakati maisha Yao kwenye mahospitali, mashule, masoko, pembejeo, usafirishaji ni magumu sana. Tumeona wakiimba hiyenahiyena hata wakati wa wizi wa Richmond, EPA, Escrow, mashirika ya umma kuuzwa, nyumba za serikali kugawanwa na wanasiasa, mikataba mibovu ya madini, nk. Lakini Sasa wanakaribia kusema HAPANA kama watanzania bila kujali vyama vya siasa.

Sio vizuri wanasiasa wakaishi kwa mazoea (stereotyped) wakidhani CCM ni ileile na wananchi ni walewale jana, Leo na kesho.

Wanakaria kuisogeza kete mbaya waliyoisongeza wenzetu wenye vurugu. Hasa pale unapomsikia kiongozi akisema kama hutaki hamia Burundi.
 
Pro CCM wachache tu wanaojiona ni wafalma, Rais wa Mali huko kakoswakoswa Ibadani kwa kisu....
 
Wanasiasa someni alama za nyakati, kaeni chonjo saa mbaya. Tozo kubwa kwenye miamala ya simu imekwenda kufuta mstari muhimu sana kwa wanasiasa unaowatenganisha watanzania kwenye itikadi za vyama vyao vya siasa. Hakuna wanaCCM wala wapinzani kwenye tozo za miamala ya simu. Hii sio ishara njema kwa wanasiasa wa makundi (divide and rule).

wanaCCM tumewazoea wakiimba iyenaiyena hata pale nchi Yao inapoporwa na wanasiasa wakati maisha Yao kwenye mahospitali, mashule, masoko, pembejeo, usafirishaji ni magumu sana. Tumeona wakiimba hiyenahiyena hata wakati wa wizi wa Richmond, EPA, Escrow, mashirika ya umma kuuzwa, nyumba za serikali kugawanwa na wanasiasa, mikataba mibovu ya madini, nk. Lakini Sasa wanakaribia kusema HAPANA kama watanzania bila kujali vyama vya siasa.

Sio vizuri wanasiasa wakaishi kwa mazoea (stereotyped) wakidhani CCM ni ileile na wananchi ni walewale jana, Leo na kesho.
Hii dhambi itawatafuna japo wameziba maskio
 
54B7EFD4-54C8-4EFA-B026-6B968E319620.jpeg
84602EEE-351D-48B0-AC20-D992E7C33176.jpeg
 
Back
Top Bottom