Hali ya usafi na mazingira katika eneo la Mathare 4A, jijini Nairobi, imezua hofu miongoni mwa wakazi baada ya maji ya majitaka (sewage) kuvuja na kumwagika moja kwa moja karibu na mlango wa nyumba ya mkazi.
Video inaonesha maji hayo machafu yakibubujika kutoka kwenye mfereji au bomba la majitaka na kusambaa katika eneo la makazi. Maji hayo yanaonekana kuwa na uchafu na kutoa harufu kali, huku baadhi ya nguo zilizofuliwa zikiwa zimetundikwa karibu na eneo lililoathiriwa.
Wakazi tuna hofu kuwa hali hiyo inaweza kuongeza hatari ya magonjwa yanayohusishwa na maji machafu, yakiwemo kipindupindu, homa ya matumbo na magonjwa ya ngozi, hasa kwa watoto wanaoweza kugusana na maji hayo.
Mbali na athari za kiafya, kuvuja kwa majitaka kunaathiri usafi wa mazingira na ubora wa makazi yetu, huku harufu kali ikitulazimu wakazi kuishi katika mazingira yasiyofaa.
Wito kwa Mamlaka
Wakazi tunaiomba Nairobi City Water and Sewerage Company (NCWSC), kwa kushirikiana na Serikali ya Kaunti ya Nairobi, kuchukua hatua za haraka kubaini chanzo cha uvujaji huo, kurekebisha miundombinu ya majitaka na kusafisha eneo lililoathiriwa.Pia, viongozi wa eneo hilo tunawaomba kufuatilia suala hilo na kuhakikisha malalamiko yetu yanafikishwa kwa mamlaka husika na kushughulikiwa kwa wakati.
Wakazi wa Mathare 4A tunasisitiza umuhimu wa kupata mazingira safi na salama na tunaomba hatua zichukuliwe haraka ili kuzuia hali hiyo kuendelea kuhatarisha afya na ustawi wa jamii.