Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Puma yetu

Senior Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
111
Reaction score
125
Wasalaam viongozi wangu taifa!


Kwanza kabisa ninaomba kuwasilisha vilio vingi kwa niaba ya wanachama wa CCM jimbo la Singida magharibi kupitia jukwaa hili.

Ninamfahamu kabisa viongozi wangu mwenyekiti na katibu wa chama changu taifa uadilifu wenu hauna mashaka na hauwezi kutiliwa shaka ya aina yeyote kabisa na walio ndani na nje ya CCM.

Kwa masikitiko makubwa kabisa sitokaa niamini macho yangu kua rushwa sasa inaweza kutupatia viongozi watakaowakilisha chama chetu kutupatia mbunge.

Imefika mahali viongozi wa chama chetu kugawana pesa nyingi wazi wazi ilimradi mgombea flani apite? Hili hapana na wanasingida Magharibi hasa wanaccm hatupo tayari kumpokea kiongozi wa aina hii.

Viongozi wangu, naomba kusema wazi kabisa kwa yakini ya moyo wangu kwamba ndugu Elibariki Kingu aliyekua mbunge wa jimbo la jimbo letu ameshinda kura za maoni kwa kutoa rushwa ya wazi wazi kabisa.

Kitendo hiki kimefanyika viongozi wote wa chama Wilaya akiwemo Mwenyezi ndugu Pius Sankha na mwenyekiti wa chama wilaya ndugu Mika Likapakapa wanajua kabisa na walitumikia kiasi flani kusimamia haya, Makatibu wote wote wa kata zote 15 wanalifahamu hili, wenzetu na wenyeviti wote kata wanayajua haya.

Kama kweli chama changu kinataka kushuhudia kuadhibiwa na wananchi katika uchaguzi ujao wa Oktoba basi huyu ndugu Elibariki Kingu arudi.

Huyu ndugu hatakiwi kabisa na wananchi kutokana tabia zake za uongo,ahadi zisizotekelezeka na kushindwa kabisa kuwahudumia wananchi wa jimbo zima.

Kwa kutambua kua hatopitishwa na hatochaguliwa tena,aliamua kutumia rushwa kurubuni wajumbe zaidi ya 300 ili waweze kumchagua.

Mheshimiwa huyu siku ya kuamkia uchaguzi wa kura za maoni jimbo la Singida Magharibi aligawa pesa usiku 70,000 kwa kila kiongozi wa kata na 50,000 kwa kila kiongozi wa tawi.

Mkitaka kupata ushahidi wa hili pitieni kwa wanachama wa CCM wa kawaida na siyo viongozi ambao hawawezi kusema kweli kwa sababu nao walitafuna pesa zake.

Elibariki Kingu pia liwalipia wapiga kura usafiri wa kutoka maeneo walipo hadi maeneo ya kupigia kura.Hii sio rushwa ni nini?

Viongozi wangu, Sambamba na hilo huyu ndugu Elibariki Kingu siku chache zilizopita aliitwa na TAKUKURU kuhojiwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya pesa za mfuko wa jimbo.

Tunawaomba sana viongozi wetu mlifanyie kazi hili jambo maana wananchi pamoja na wanaccm wanachama wa kawaida wamesikitishwa sana na vitendo hivyo na kwa minong'ono yao wanasema wanaweza kumwadhibu ndugu huyu nje ya CCM ikiwa kweli atapitishwa.


Ninawatakia majukumu mema viongozi wangu.Ni imani yangu kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Singida Magharibi hili jambo litafanyiwa kazi.
 
Singida cha mtoto.

Same MAGHARIBI Mathayo David ameganya kufuru kwa kununua kura moja kwa laki moja na kisha yamini kwa kunuwia kwamba wajumbe wampe kura.

Wananchi wanasikitishwa na CCM kuachia watoa rushwa uwanja watambe licha ya maelekezo ya chama kukemea rushwa.

Kiufupi wananchi na wana CCM tunasubiri kuona kama CCM kweli inaichukia Rushwa.
 
Amechaguliwa? Kwa kura halali? Za wajumbe halali? Kama ujaridhika ujue mfumo wa Chama ndo Mbaya!
 
Sishangai hao watu kutoa rushwa maana hawawezi kujiajiri wamezoea kuajiliwa na wananchi siku zote na kula keki ya nchi.

Ila wakiwa bungeni wanatoa maneno ya kashifa sana kuwa watoto wa wapiga kura wajiajiri, wapuuzi sana baadhi yao

Dawa la hao ni kutowapa kura ili watoe vizuri rushwa, unachukua rushwa harafu unamnyima kura tuone kama hajajinyonga
 
Hafai kabisa Kingu anatuchafulia Chama chetu.Huu ujinga chama chetu hakiwezi kuuvumilia
 
Sisi tumejionea kwa macho Wajumbe wakipigwa 70000 mpaka 100000 live. TAKUKURU Singida wanasubiri mpaka waambiwe wapo maofisini tu
 
Bila kutoa ahadi za uongo wananchi hawawezi kukuelewa. Vumilia tu miaka mitano sio dili
 
Huu!! Huyu Kingu amejawa na u.tap.eli na Usanii mwingi. Ninyi watu wa Singida Magharibi wajinga sana, Mtimueni huyo msanii aondoke.Yawezekana ana watu Wake TAKUKURU sio bure
 
Sishangai hao watu kutoa rushwa maana hawawezi kujiajiri wamezoea kuajiliwa na wananchi siku zote na kula keki ya nchi.

Ila wakiwa bungeni wanatoa maneno ya kashifa sana kuwa watoto wa wapiga kura wajiajiri, wapuuzi sana baadhi yao

Dawa la hao ni kutowapa kura ili watoe vizuri rushwa, unachukua rushwa harafu unamnyima kura tuone kama hajajinyonga
Right kabisa mkuu
 
Chama hakifanyii kazi maoni ya kwenye mitandao, wasilisha malalamiko yako sehemu husika na uwe na ushahudi usio na shaka
 
Back
Top Bottom