Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Keshapita muungeni mkono inaelekea wote wasiomtaka ndio wanalalamika sasa mnamtaka nani na Kura tayari?

Hamieni Vyama vingine km CCM imejaa rushwa Kura bila rushwa CCM hutoboi
 
Panga la kuzuia rushwa lazima liwapitie...CCM hii ni adilifu
 
Hao unaosema walichukua rushwa na kumpitisha ni miongoni mwa wananchi sasa watashindwaje kumpitisha kwenye kura za uchaguzi wa wabunge. Kama kawanunua chamani basi atawanunua na hao wengine.
Ila naona kama unatapatapa; mara useme viongozi wamekula rushwa mara wapiga kura wamekula rushwa: kwani huko kwenu hakuna PCCB? Naona kama vile jamaa kakupiga sasa kama kawaida unaanza majungu
Rushwa ilitamalaki, Ila hapa walizidiana tu viwango
 
Kwani hao akina bashiru ni wasafi? Unafikiri Ununuzi wa wabunge na madiwani wa upinzani kwa fedha nyingi za walipa kodi unafanywa bila idhini yao??!

Rushwa ndani ya ccm ni halali na ipo kisheria, wao wanaita TAKRIMA.

Ccm na Rushwa ni kama mwili na damu.. kimoja kikiondoka kingine kinakufa hapo hapo!
 
Pasipokuwa na mpokea rushwa huyo mtoa rushwa atampa nani hiyo rushwa yake, tafakari. Tatizo kura zinauzwa mtu asiyetoa basi imekula kwake hapati kura hata moja.
 
Elibariki Kingu aliyekua mbunge wa jimbo la jimbo letu ameshinda kura za maoni kwa kutoa rushwa ya wazi wazi kabisa.
Mkuu katika enzi hii ya teknolojia, ulishindwa kabisa kuvaa miwani janja au saa janja au hata kutumia simu janja yako kumrekodi ili upeleke takukuru kama ushahidi?
 
Siyo Singida tu,hata Shinyanga na Kishapu. Rushwa haiwezi kuisha.
Vyama vya upinzani vingekuwa hai,shinyanga mjini na Kishapu CCM isingeshinda
 
Mkuu katika enzi hii ya teknolojia, ulishindwa kabisa kuvaa miwani janja au saa janja au hata kutumia simu janja yako kumrekodi ili upeleke takukuru kama ushahidi?
atawezaje kurekodi wakati yeye ndio mpokeaji? yaani ajifunge kitanzi??
 
Unapoikubali rushwa kwa kuwa inakunufaisha (kwa jina lolote lile) uendelee kuikubali hata pale itakapokuumiza!
Kumbuka kuna nyakati watu waliruhusiwa kutoa takrima, na ikahalalishwa kabisa yaani kuwapa wajumbe chakula, kinywaji nk ikawa ni halali kwa kuwa unawakirimu! Tukawa na wabunge ndani ya bunge walioingia kwa kutoa takrima. Mahakama iliposema takrima ni rushwa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waliojinufaisha na hiyo takrima.
Kama nimepata nafasi kwa kutoa takrima si ni lazima nitafute namna ya kurudisha hizo gharama? Hapo ndipo sheria na mikataba mibovu iliposhika kasi.
Rushwa imekuwa kama kansa sasa, na dawa ya kansa ni kukata sehemu iliyougua au kuichoma sehemu iliyougua, Nani afanye hivyo? Labda JPM anaweza kuthubutu, lakini yanayoendelea sioni kama yanampa nguvu hiyo. Ukisoma thread hii hapa Uchaguzi 2020 - Membe au Lissu msisahau kuusema uozo wa "undugunaization", tribalism na nepotism wakati wa Kampeni utaona ni kwa nini naona ugumu Angalia maoni ya wachangiaji, wengi wanakiri kuwa hayo yapo ila ni kutesa kwa zamu na kwamba yapo kila mahali na katika vyama vyote. Hakika hii ni kansa.
 
Mkuu katika enzi hii ya teknolojia, ulishindwa kabisa kuvaa miwani janja au saa janja au hata kutumia simu janja yako kumrekodi ili upeleke takukuru kama ushahidi?
Rushwa inagawiwa kijana sana, pesa zinatumwa kupitia MAWAKALA wa mitandao ya simu itakamata nani? Utamrekodi nani? Hawa makatibu ndio wanatumika sana
 
Unapoikubali rushwa kwa kuwa inakunufaisha (kwa jina lolote lile) uendelee kuikubali hata pale itakapokuumiza!
Kumbuka kuna nyakati watu waliruhusiwa kutoa takrima, na ikahalalishwa kabisa yaani kuwapa wajumbe chakula, kinywaji nk ikawa ni halali kwa kuwa unawakirimu! Tukawa na wabunge ndani ya bunge walioingia kwa kutoa takrima. Mahakama iliposema takrima ni rushwa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waliojinufaisha na hiyo takrima.
Kama nimepata nafasi kwa kutoa takrima si ni lazima nitafute namna ya kurudisha hizo gharama? Hapo ndipo sheria na mikataba mibovu iliposhika kasi.
Rushwa imekuwa kama kansa sasa, na dawa ya kansa ni kukata sehemu iliyougua au kuichoma sehemu iliyougua, Nani afanye hivyo? Labda JPM anaweza kuthubutu, lakini yanayoendelea sioni kama yanampa nguvu hiyo. Ukisoma thread hii hapa Uchaguzi 2020 - Membe au Lissu msisahau kuusema uozo wa "undugunaization", tribalism na nepotism wakati wa Kampeni utaona ni kwa nini naona ugumu Angalia maoni ya wachangiaji, wengi wanakiri kuwa hayo yapo ila ni kutesa kwa zamu na kwamba yapo kila mahali na katika vyama vyote. Hakika hii ni kansa.
Hii sio sawa
 
CCM kama chama tuna shida kubwa sana kuiondoa rushwa.Sijui ni lini tutapata wagombea imara wasiotokana na rushwa,sijui ni lini tutaenzi kwa vitendo matendo ya Rais wetu?
 
Tukio linakua planned kwa dakika 3, Wajumbe wanapangwa wanaelekezwa sehemu ya kusubiria pesa, walishakaa tayari wanampigia simu mwenye pesa, yaani anapita kama mwewe dakika 3 smeshawagawia na kuondoka. Sasa mpaka PCCB wafike eneo la tukio saa ngapi ndugu yangu?
 
Geita kwa Mkuu ndo kunanuka harufu yamizoga ya kila aina ya Rushwa..... Ni matapishi kwa CCM mwaka huu itoshe kusema wagombea nafasi 1-3 ni wachafu tena wachafu sanaaa kwa rushwa....

INATISHA HUKO CHATO NDO HATA SISEMI .....
 
Mtoa post kubali matokeo, wewe mbona na wewe ulikuwa unatoa pesa? Lizika nahiyo nafasi ya tano uliyopata. Wewe so ulikimbia chadema Kimia Kimia. Au unafikili hatujui?
 
Kama huna ushahidi nadhani ungekaa kimya mkuu! Hapo mlitakiwa kuchukua picha au sauti ya watoa rushwa na wapokea Rushwa na kupeleka TAKUKURU.
Vile vile fahamu kuwa TAKUKURU haina meno ya kung´ata wanachama wa CCM wenye hela.
Fahamu kuwa bila CCM na Rushwa haviachani,ni kama Chapati na Kikaaongo.
Poleni sana na huyo ndiye mbunge mtarajiwa!
 
Back
Top Bottom