Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Hakika kila mgombea wa nafasi ya ubunge karibu Inchi nzima ametoa rushwa wakati wa kutangaza nia, kabla ya kutangaza nia na wakati wa kugombea.
Ndiyo maana hata wale walioshinda wanaugulia baada ya kutumia pesa nyingi katika mchakato huu.
Kuna gharama gani za kutumia hadi milioni hamsini lakini bado kwenye kura za maoni kura hazikutosha.
Kila mtu katoa rushwa kwa namna moja au ingine. Wengine baada ya kutoa rushwa, ametoa ahadi kwa wapiga kura kuwa akishinda ni lazima arudishe shukurani. Kwa hiyo baada ya watu kuchaguliwa kuwa wabunge rushwa itaendelea ila itaitwa ni misaada.
Rushwa inapotolewa ni jambo la siri kubwa kati anayetoa na anayepokea.
Wote wawili, aliyetoa na aliyepokea ni wahalifu.
Ikitokea mpokea rushwa hajalalamika na hakuna mtu wa watu aliyewakamata wakati wanapeana rushwa, kisiasa tutamwita mlalamikaji anafanya majungu na anamchafua mtoa rushwa. Kisheria tunasema hakuna kesi ya kujibu kwa sababu hakuna ushahidi.
Wanyaturu ni watu waliostarabika, wasio na ukabila wala udini.
Kingu ni Mnyiramba lakini waliomchagua katika kura za maoni wengi ni Wanyaturu.
Huko Ilongero , lililokuwa jimbo la Mh. Nyalandu, wao wamempitisha Mhindi ( nawapa hongera , maendeleo hayana ukabila). Katika jimbo la Singida mjini awamu za nyuma , Mh . Mohamed Dewji (MO), mhindi)alipewa Ubunge kwa kura nyingi
Kijana Kingu, ukilinganisha na wabunge wengi wa jimbo hili waliopita hakuna mbuge anayemfikia kwa kuwa na ukaribu na watu (social interaction) katika maswala ya maendeleo, misiba na kadhalika.
Tukisema Kingu ni mtoa rushwa na hiyo rushwa imepokelewa tunawadhalilisha zaidi wapiga kura kuliko Kingu MWENYEWE.
Kingu bado atabaki ni bora kuliko wabunge wote waliowahi kushinda jimbo la Singida vijijini au Singida Magharibi kwa sasa.
Kinachoendelea kumgharimu Kingu ni Historia, bila hivyo angekuwa amepewa Uwaziri siku nyingi.
Katika kipindi cha nyuma alikuwa ni mfuasi wa Lowasa kabla Lowasa hajahamia CHADEMA. Watu wa kundi hili wameendelea kusota.
 
Back
Top Bottom