Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Uchaguzi 2020 Kilio hiki kikufikie Dkt. Bashiru na Rais Magufuli. Rushwa yatoa mgombea Singida Magharibi

Hao unaosema walichukua rushwa na kumpitisha ni miongoni mwa wananchi sasa watashindwaje kumpitisha kwenye kura za uchaguzi wa wabunge. Kama kawanunua chamani basi atawanunua na hao wengine.

Ila naona kama unatapatapa; mara useme viongozi wamekula rushwa mara wapiga kura wamekula rushwa: kwani huko kwenu hakuna PCCB? Naona kama vile jamaa kakupiga sasa kama kawaida unaanza majungu.
 
Singida cha mtoto.
Same MAGHARIBI Mathayo David ameganya kufuru kwa kununua kura moja kwa laki moja na kisha yamini kwa kunuwia kwamba wajumbe wampe kura.
Wananchi wanasikitishwa na CCM kuachia watoa rushwa uwanja watambe licha ya maelekezo ya chama kukemea rushwa.
Kiufupi wananchi na wana CCM tunasubiri kuona kama CCM kweli inaichukia Rushwa.

Acha uongo, sema wa pili ndio amefanya hayo.
 
Utaratibu wa kutoa rushwa ndani ya CCM ni wakawaida sana, umekuwepo miaka mingi, na haitatokea uishe leo ama kesho. Ni utamaduni usio rasmi wa CCM. Ukiwa ndani ya CCM unapaswa ulitambue hilo.
 
Kama Kuna mgombea ambae hajafanya hivi katika waliokua wabunge Basi hawafiki 01%
 
Before to compete, try to know rules of the game firstly.
Chaguzi zenye kuihusisha CCM ni vigumu zikafanyika bila rushwa.
 
Ukiona mtia nia ndani ya CCM hatoi rushwa basi ujue hana pesa za kutoa au ameingia kusindikiza wengine.
 
Tulia dawa iingie, rushwa ni moja ya mbinu ya kufanikisha jambo rushwa mbaya ni za kudhulumu wanyonge tuu..
 
Uyo jamaa kazoea sana kula na kutoa rushwa toka enzi za JMK. JMK na upole wake alimtumbua alivokua mkuu wa wilaya igunga
 
Kwa udadisi wangu mpana katika kura za maoni ndani ya CCM, rushwa hutolewa na wagombea wengi. Mshindi na walioshindwa wote hutoaga rushwa, tena unaweza kukuta, aliyeshindwa katoa rushwa kubwa zaidi kuliko hata mshindi.
 
Kuna clip nmeiona inamuonesha jamaa anawapa Wajumbe Hela, anawambia..... Ngojeni niwape Hela mkanywe maji au soda [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mshana Jr

Ova
 
Umeshindwa unasingizia rushwa. Ni jukumu la wapiga kura kukataa rushwa. Unaweza pewa rushwa na usimpigie aliyekupa, ndio maana wengi wazito wamegaragazwa. Na kama alitoa rushwa ungemripoti TAKUKURU.
 
Umeshindwa unasingizia rushwa. Ni jukumu la wapiga kura kukataa rushwa. Unaweza pewa rushwa na usimpigie aliyekupa, ndio maana wengi wazito wamegaragazwa. Na kama alitoa rushwa ungemripoti TAKUKURU.
Tunasema tunachokijua ndugu yangu wewe endelea kuongea tu muda ni mwalimu mzuri
 
Tunasikia hata jimbo la kilombero kulikuwa na fujo za aina hiyo hiyo. Mkutano ulianza kwa kuchelewa sana saa 12 jioni. Poleni sana. Bila shaka viongozi wetu wa chama wamesikia na hatua kuchukuliwa.
 
Mimi ni mwana CCM
wa tangu enzi za TANU.Chama chetu kilianza vizuri sana wakati wa Mwalimu,lakini baada ya Azimio la Zanzibar,Chama kiligeuzwa kuwa pango la wanyanganyi na wengi wetu tulikarahishwa sana na tabia hizi,na kwa vile tulikosa msaada tulikaa pembeni na kua waangaliaji.Sio siri kwamba tabia za rushwa bado zipo ndani ya chama chetu.

Ni ukweli mchungu kwamba Mwenyekiti wa chama,TAKUKURU na wana-CCM bado tuna kazi ngumu mbele yetu ya kumaliza tatizo hili.

Nimefurahi kuona kwamba bado wapo wanachama wanaochukia rushwa kwa dhati kabisa ndani ya chama.Ningeomba basi wanachama kama hawa watiwe moyo kwa wahusika wote kushirikiana kutatua tatizo hili mapema iwezekanavyo.Najua JF wapo wawakilishi wa Mwenyekiti wa Chama,TAKUKURU na hata TISS.

Basi wote tushirikiane na tuhakikishe kwamba tatizo hili limepatiwa ufumbuzi mapema ili kutia moyo wanachama wa aina hii.Yeyote aliyeshiriki katika upuuzi huu ashuhulikiwe kulingana na sheria za Chama na nchi kwa haraka.

Katika matukio kama haya ndipo tunapoweza kuonyesha wananchi kwamba kweli Chama chetu kinachukia rushwa,kwa hiyo naomba Elibariki Kingu atolewe kafara iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ovu kama yeye ndani ya Chama.

Ni kweli kabisa kwamba kiongozi aliyepatikana kwa rushwa hawezi kuwahudumia wananchi na hii haiwezi kuvumiliwa,hasa wakati huu wa uongozi wa awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom