Mimi ni mwana CCM
wa tangu enzi za TANU.Chama chetu kilianza vizuri sana wakati wa Mwalimu,lakini baada ya Azimio la Zanzibar,Chama kiligeuzwa kuwa pango la wanyanganyi na wengi wetu tulikarahishwa sana na tabia hizi,na kwa vile tulikosa msaada tulikaa pembeni na kua waangaliaji.Sio siri kwamba tabia za rushwa bado zipo ndani ya chama chetu.
Ni ukweli mchungu kwamba Mwenyekiti wa chama,TAKUKURU na wana-CCM bado tuna kazi ngumu mbele yetu ya kumaliza tatizo hili.
Nimefurahi kuona kwamba bado wapo wanachama wanaochukia rushwa kwa dhati kabisa ndani ya chama.Ningeomba basi wanachama kama hawa watiwe moyo kwa wahusika wote kushirikiana kutatua tatizo hili mapema iwezekanavyo.Najua JF wapo wawakilishi wa Mwenyekiti wa Chama,TAKUKURU na hata TISS.
Basi wote tushirikiane na tuhakikishe kwamba tatizo hili limepatiwa ufumbuzi mapema ili kutia moyo wanachama wa aina hii.Yeyote aliyeshiriki katika upuuzi huu ashuhulikiwe kulingana na sheria za Chama na nchi kwa haraka.
Katika matukio kama haya ndipo tunapoweza kuonyesha wananchi kwamba kweli Chama chetu kinachukia rushwa,kwa hiyo naomba Elibariki Kingu atolewe kafara iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ovu kama yeye ndani ya Chama.
Ni kweli kabisa kwamba kiongozi aliyepatikana kwa rushwa hawezi kuwahudumia wananchi na hii haiwezi kuvumiliwa,hasa wakati huu wa uongozi wa awamu ya tano.