Kilo 1.2 ya heroin yawafikisha mahakamani

Kilo 1.2 ya heroin yawafikisha mahakamani

View attachment 1850630

Watu watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mkoani Dar es salaam, wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kilo 1 na gramu 200.

Washtakiwa hao ni Andrew Paul, Said Mugoha na Geroge Mwang’ata wote wakazi wa Temeke mkoani Dar es salaam.

Akiwasomea washtakiwa hao shtaka lao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Ritha Tarimo, Wakili wa Serikali Yusuf Aboud amedai washtakiwa hao wametenda kosa hilo Juni 21 mwaka huu maeneo ya Mivinjeni katika manispaa ya wilaya ya Temeke.

Mara baada ya washtakiwa hao kusomewa shtaka lao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Aidha wakili Aboud amedai upepelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo kuomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 27 mwezi huu kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

TBC Taifa
Japo wanahatarisha maisha ya watu kwa kuwapiga dozi za madawa, wao wanajilinda COVID-19 kwa kuvaa barakoa. Ubinafsi huu
 
Dah! Ila mjini watu wanatafuta hela kibabe!! Full kuendesha magari makali, kuishi kwenye mahekalu! Full kumiliki pisi kali!!

Ila siku ukiotewa, ndiyo basi tena!
Na hata pisi kali zote zinakukimbia, neno baby linakuwakama msamiati, hutalisikia tena huku ukiendelea kunyaea debe.
 
Hao wanakuwa ni wafanyabiashara Tena?

Wafanyabishara watatu wa jijini Dar es Salaa wakiwa chini ya jeshi la Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wafanyabishara watatu wa jijini Dar es Salaa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 1.02.

Wakili wa serikali , Yusuph Aboud akisoma hati ya mashtaka amesema washtakiwa hao kuwa ni Andrew Paul (34) Mkazi wa Kurasini, Said Mugoha (45) Mkazi wa Mtoni Kijichi Temeke na George Mwakang’ata (38) Mkazi wa Mbagala Kuu.

Washtakiwa hao wamesomewa Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo ambapo imedaiwa Juni 21,2021 huko Mivinjeni ndani ya Wilaya ya Temeke Dar es Salaam, walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 1.2 huku wakijua ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 27 mwaka huu.
 
Sichangii mpaka nithibitishe toka kwa chanzo kingine.
TBC siiamini.
Kama Kuna anayejua kuondoa TBC kwenye King'amuzi Cha DStv anifahamishe, hata hela nitampa.
 
Back
Top Bottom