Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Kwa takwimu za kimataifa, katika bara la Africa, Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa Ng'ombe (bila kujumuisha kondoo, mbuzi, na kuku) ikitanguliwa na Ethiopia. Sasa cha kujiuliza, kitu gani kinapelekea kupanda kwa bei ya nyama mpaka kilo 13,000?.
Hivi mnajua maana ya 13,000? Kwa familia ya kawaida mboga ya siku moja kilo moja haitoshi angalau kilo mbili kwa 26,000/=. Hii ni aibu kama taifa. Kwa upande wa pili, hivi hawa vijana waliomaliza shule na vyuo wanaolialia hakuna ajira na kushinda mitaani wanazurula na bahasha wakiomba kazi hawaoni hii fursa?
Wanashindwa nini kutafuta mapori na kupewa kibali na serikali za vijiji na kununua ndama na kuzikatia majani na kuzichotea maji na kuzinenepesha ndani ya mwaka zikazaliana ndani ya miaka mitatu wakaanza kuvuna? Yangu ndo haya napita!🚶🏻♀️🚶🏻🏃🏻♀️🏃🏻