Kilo moja ya nyama kuuzwa 13,000 ni laana au ni nini?

Kilo moja ya nyama kuuzwa 13,000 ni laana au ni nini?

nyama hailimwi ndugu..

watanzania wengi mnakula misuli sio nyama wacha niwaibie utalamu kidogo ndugu zangu
 
Kitimoto ni 10-12 elfu kutegemea eneo ulipo kwa mjini.
Kule kwetu kilo ya nyama tamu kuliko zote duniani (kitimoto) ni 7000 hadi 5000 kutegemeana na kijiji ulipo.

Hamieni huku kwenye Noah aisee hizo bei zitawaua
 
Kwasasa upatikanaji wa mifugo ni mgumu na wakipatikana bei ni kubwa sana... Hii imesababishwa na gharama kuwa kuwa kubwa kuwahudumia hao mifugo. Chakula bei juu na madawa pia
 
Kwa takwimu za kimataifa, katika bara la Africa, Tanzania ni nchi ya pili kwa wingi wa Ng'ombe (bila kujumuisha kondoo, mbuzi, na kuku) ikitanguliwa na Ethiopia. Sasa cha kujiuliza, kitu gani kinapelekea kupanda kwa bei ya nyama mpaka kilo 13,000?.

Hivi mnajua maana ya 13,000? Kwa familia ya kawaida mboga ya siku moja kilo moja haitoshi angalau kilo mbili kwa 26,000/=. Hii ni aibu kama taifa. Kwa upande wa pili, hivi hawa vijana waliomaliza shule na vyuo wanaolialia hakuna ajira na kushinda mitaani wanazurula na bahasha wakiomba kazi hawaoni hii fursa?

Wanashindwa nini kutafuta mapori na kupewa kibali na serikali za vijiji na kununua ndama na kuzikatia majani na kuzichotea maji na kuzinenepesha ndani ya mwaka zikazaliana ndani ya miaka mitatu wakaanza kuvuna? Yangu ndo haya napita!🚶🏻‍♀️🚶🏻🏃🏻‍♀️🏃🏻
Ulianza vizuri ila hapo mwisho umeonyesha hasira na vijana wanaomaliza chuo kwa shida zako.

Kama unaona kuna fursa changamkia then uje kuajiri hao vijana kukata majani.
 
Kitimoto ni 10-12 elfu kutegemea eneo ulipo kwa mjini.
Kule kwetu kilo ya nyama tamu kuliko zote duniani (kitimoto) ni 7000 hadi 5000 kutegemeana na kijiji ulipo.

Hamieni huku kwenye Noah aisee hizo bei zitawaua
Kitimoto haiwezi kuwa mbadala wa nyama ya ng'ombe! Sijawahi ona sherehe za heshima zikiandaliwa na nyama ya nguruwe
 
Back
Top Bottom