Kilo ya dagaa yaipiku ya nyama kwa sasa bongo

Kilo ya dagaa yaipiku ya nyama kwa sasa bongo

Ni kweli nimetoka sokoni.
Hata mie nimeshangaa.
Maana najua ni 7,000 ila nimeuziwa 11,000 nikalalama mpaka 10,000.
Anyway watatusogeza mwezi mzima.
 
Ni kweli nimetoka sokoni.
Hata mie nimeshangaa.
Maana najua ni 7,000 ila nimeuziwa 11,000 nikalalama mpaka 10,000.
Anyway watatusogeza mwezi mzima.
Ilaa nyama kilo mojaa ni siku mojaa[emoji1787][emoji1787]
 
Laki na kumi kwa kilo ya kauzu NEVER! this is strong tea.
 
Kweli hii vita hatari sana Jana nimeenda kununua dagaa bukoba kilo moja ni Tsh 110000 na nikaenda buchani kununua nyama ni 8000 nikastajaabu jinsi dagaa zilivyokuwa ni chakula cha mtu wa chini kwa kipato now azishikiki yaaani sasa nyama ni chakula cha mtu wa chini dagaa matawi ya juu mambo yanaenda yakibadilika hatari sana
Mama anaupiga mwingi [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ilaa nyama kilo mojaa ni siku mojaa[emoji1787][emoji1787]
Yes
Kwanza nikaanza kulalamika nilihisi sababu nimebadili soko eti soko hilo linauza vitu bei juu mwee.
 
Mimi nilienda sokoni ndani ya wiki 1 dagaa nilikuwa nanunua 600 ni elfu 1 halafu wa elfu moja ni elfu moja mia nane nikamwambia mzee muuzaji mama anaupiga mwingi nikampa elfu 2 kurudisha mia 2 nikaondoka
 
Kweli hii vita hatari sana Jana nimeenda kununua dagaa bukoba kilo moja ni Tsh 110000 na nikaenda buchani kununua nyama ni 8000 nikastajaabu jinsi dagaa zilivyokuwa ni chakula cha mtu wa chini kwa kipato now azishikiki yaaani sasa nyama ni chakula cha mtu wa chini dagaa matawi ya juu mambo yanaenda yakibadilika hatari sana
Ulimaanisha 11'000/=?
Hata hivyo kilo 1 ya dagaa ikipikwa kama kitoweo inaliwa na watu 30 kwa kushiba, wakati kiloc1 ya nyama ikipikwa kama kitoweo inaliwa na watu4 au 5 tu.
 
Hao dagaa wanatoka wapi hadi bei iwe hiyo.au wanawapiga kwakisingizio cha vita ya ukrain na bei a mafuta.Nimeuliza bei ya debe maeneo ya Kasenda mganza wanasema debe ni elfu 30.
 
Acha uongo wewe fungu la dagaa kipindi hicho lilikuwa 300 mpk 500 inakuwaje dagaa wafike 15k.
Unajidhalilisha mzee kama kitu hujui hebu nyamaza.. Kaulizie bei ya dagaa wa kigoma rightnow halafu tuletee majibu sasa hivi..
 
Usisahau kwenye nyama unauziwa na mifupa.

Kuna siku nilishangaa jamaa wakati anapima, alipoona kipimo hakijafika akaongeza na mfupa. Kumuuliza akanijibu na wao wakiwa wanapimiwa ng’ombe na wauzaji huwa anakuwa na mifupa yake, ikabidi niondoke kimya kimya.

NB: Pamoja na uwezekano wa dagaa kuliwa wiki nzima, bado kilo moja ya nyama hiyo hiyo ikiwa ni steki bila ya mifupa, inaweza kuwa na gharama zaidi ya Tzs 11,000/= ya dagaa.
 
Dagaa wameadimika hata kwenye mialo ,kama unabisha nenda lake Tanganyika au njoo Mwanza na Bunda au kama Una ndugu yako muulizie jinsi mialo ya dagaa na samaki ilivyodorora sasa hivi , dagaa hamna kabisa na sijui tatizo ni nini Maana kuna ndugu yangu anamiiliki boti za uvuvi na amekuwa akilalamika Kwa miezi kadhaa sasa kwamba biashara sio nzuri kabisa mzigo kwenye maziwa hasa dagaa haupatikani wavivu wamekuwa wanarudi mikono mitupu na saa nyingine mzigo kidogo sana
 
Sijasema laki ni elfu kumi namoja wakuu
 
Dah Hao dagaa ni wale wa kuchinjwa labda kilo laki na 10 loh
 
Back
Top Bottom