Pre GE2025 Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara

Pre GE2025 Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kushukuru ni kuomba tena , hongera bwana Mbunge Kwa uungwana .

My Take
Mama amewafuta machozi

=====

Screenshot_20240804_160959_Chrome.jpg

Mbunge wa Kilombero Abubakari Asenga, amepiga magoti kumshukuru Rasi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha jambo kubwa la barabara ya lami ya Kidatu hadi Ifakara.

Kama unakumbuka mwaka 2022 Mbunge huyo alipiga magoti katika barabara hiyo hiyo ikiwa ya matope na kumwomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumsaidia kupata barabara ili wananchi wake waweze kuepukana na hadha waliyokuwa wakiipata wakati wa kipindi cha masika.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Utumwa hauwezi kuondoka Africa, Unampigiaje goti mtu ambaye hatoi hata mia, Kwanza hajawahi kulipa kodi hata mara moja, Poor Tanzania!
Serikali yake imetoa,ingeweza kuzipeleka Kyela mnakosombwa na Mafuriko Kila msimu.
 
Na sio Maboss wake yeye na huyo anayemshukuru (wananchi) waliomchagua na kulipa kodi zinazowapa mahitaji yao ?!!

Hivi hapo nani amshukuru nani ? (Hakuna sababu ya kuwashukuru hawa watumishi bali kuna kila sababu ya kuwalaumu kila mara wanapofanya chini ya kiwango) which is always by the way
 
Wangeweza kulipa na Serikali ikapeleka kwingine.

Mfano wewe umchague Mwabukusi harafu Jimboni kwako Kuna Changamoto ya Daraja utaambiwa Serikali inaendelea kutafuta hela,Je utafanyaje?
 
Back
Top Bottom