Kilombero sugar yapokea kundi la wapandaji mlima kilimanjaro kutoka illovo sugar africa, warejea salama na chapa ya bwana sukari kutoka kileleni

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
132
Reaction score
75
Image.jpg
Mhe. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasiali na Utalii, Nkoba Mabula (kulia) akiongozana pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Ndugu: Ephraim Balozi Mafuru(kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sukari Kilombero Ndugu;-Derick Stanley (katikati) kuwakaribisha Kundi la Wapandaji Mlima Kilimanjaro kutoka Illovo Sugar Africa ambao walipanda mlima kuenzi urithi wa Mandela na kuchangisha fedha kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la hedhi salama kwa watoto wa kike.
View attachment KP_L5413.JPG

Marangu, Kilimanjaro. 22 Julai 2024. Kampuni ya Sukari Kilombero ilipewa
heshima kubwa ya kuikaribisha tena timu ya ‘Illovo Sugar Africa Kilimanjaro
Climber’, baada ya kurejea salama kutoka kwenye kilele cha mlima huku
wakisindikizwa na chapa maarufu ya "Bwana Sukari." Tukio la kuwakaribisha
tena limefanyika katika lango la Marangu na kulakiwa na Naibu Katibu Mkuu
wa Utalii, sambamba na timu ya Bodi ya Utalii Tanzania. Katika hafla hiyo ya
kufurahisha kikundi hicho kilikabidhiwa vyeti vya ushindi wao wa kupanda
Mlima Kilimanjaro na kufikia kilele cha Uhuru katika mwinuko wa mita
5895/19841 kutoka usawa wa bahari. Tukio hili la aina yake linasimama kama
msingi wa Kampeni ya ‘Kilimanjaro Expedition’.
Maazimio ya pamoja ya kuupanda mlima Kilimanjaro yalikuwa kwa ajili ya
kuheshimu urithi usiofutika wa Mandela na kuchangisha fedha na uhamasishaji
katika mapambano dhidi ya hedhi salama, katika kuhakikisha wasichana
20,000 wanasaidiwa kupitia nchi ambazo Illovo Sugar inatoa huduma kwa
kutoa taulo za kike kwa mwaka mzima.
Sherehe ya kuwakaribisha wageni hao ilifana sana na uwepo wa Naibu Katibu
Mkuu wa Utalii Ndugu Nkoba Mabula akishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania
sambamba na mwakilishi kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero ambapo
Kampuni hiyo ya Sukari ni mwenyeji wa wageni hapa nchini.
Katika hafla hii muhimu, Naibu Katibu Mkuu wa Utalii Bw. Nkoba Mabula
aliwapongeza wapanda mlima wote kwa kurejea salama wakiwa na furaha na
mshikamano. Alisisitiza nia thabiti ya Serikali katika kusaidia na kuwezesha
sekta ya utalii, kuhakikisha mazingira yanasaidia shughuli za Utalii. Akiwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo, Bw. Mabula aliwapongeza wapanda mlima huo

kwa kufanya ziara ya kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro, wakitumia jitihada
hizo kukusanya fedha za kukabiliana na hedhi salama kwa watanzania na jamii
nyinginezo ambako Kampuni hizo zinafanya kazi, ikiwa na dira ya ustawi wa
jamii ni kuwa na maendeleo.
Akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wageni hao, Mkurugenzi wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Ndugu: Derick
Stanley, alisisitiza jukumu kubwa la nchi mwenyeji katika kuhakikisha jitihada
za kutangaza kivutio cha mlima Kilimanjaro zinafanikiwa. Alisisitiza umuhimu
wa kuonyesha utofauti na ushirikishwaji kwa ushiriki wa vikundi mbalimbali
vya wapanda mlima, hivyo kudhihirisha fahari ya Tanzania kama nchi mwenyeji
na Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio cha watalii.
Ndugu, Derick aliipongeza zaidi hatua ya chapa ya 'Bwana Sukari,' kufikishwa
katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na wawakilishi wa Tanzania, kuashiria
ubora wa bidhaa hiyo, uwepo wake sokoni, na utofauti katika mlima huo
mkubwa. Kampuni ya Sukari Kilombero inawatakia kheri wapanda mlima wote
amani na furahi wanapoendelea kufurahi vivutio vya nchini Tanzania.
Kwa upande mwingine, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), mshirika mkuu katika
Kampeni hii ya ‘Kilimanjaro Expeditions’, ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu,
Bw. Ephraim Balozi Mafuru imeliona tukio hili kama kichocheo cha kukuza
vivutio vya utalii nchini na imejikita kusaidia mipango ya kuendelezea sekta ya
utalii.
Kama ishara ya kushukuru wakati wa hafla ya kuwakaribisha wageni hao, timu
iliyoongoza wapandaji ikiongozwa na , Dk. Ernest Peresu, ilionyesha shukrani
ya dhati kwa ukarimu wa watanzania na maliasili nyingi za Tanzania, na
kuwahimiza watu duniani kote kuja na kushiriki katika kufurahia vivutio vya
aina yake vinavyopatikana Tanzania.

Kampuni ya Kilombero ambayo ni kampuni tanzu ya ‘Illovo Sugar’, itabaki
imara katika kuhakikisha inakuza ustawi wa jamii kupitia Kampeni mbalimbali
kama vile ‘Kilimanjaro Expeditions’, yenye lengo la kupambana na tatizo la
hedhi salama. Sambamba na ahadi hiyo, kampuni imetoa msaada wa taulo za
kike 2400 kwa Shule ya Sekondari Mieresini iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro.​
 
Attachments

View attachment 3049082

Great story
 
Back
Top Bottom