Kilomita za gari na miaka ya kutengenezwa gari..

Kilomita za gari na miaka ya kutengenezwa gari..

lordchimkwese

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2015
Posts
1,914
Reaction score
3,356
Wakuu nimekua nikiona gari zinauzwa mtandaoni mfano gari ya mwaka 1999... Lakini ina kilometa 45000 sasa ninachojiuliza inamana ilitengenezwa 1999 ikawa ina park tu ama wanafanyaje huko kwa wenzetu..
Mana huku ukipaki kigari chako miezi 6 complication kibao
 
Uzi umesuswa Asee. Hata Mimi nilikuwa Nasubiri majibu
 
Mi nadhani gari kama hiyo inakuwa inatumiwa na watu wasio na mizunguko mingi mfano mtu anatoka kwake hadi kazini na kurudi(sio mbali)na week end gari imepark tu

Wajuzi zaidi wataelezea.
 
Inawezekana.

Nimeona harrier ya 1999 imenunuliwa 2012 ikiwa na 30.000Km hadi sasa 2019 ina 50.000Km.

Ingetumiwa na mtu mwingine ingeshafika 150.000Km.
 
Mana ku maintain gari miaka 20 ngoma nzito huku ki IST namba B unakuta kimeoza kabisa ila yanakuja mazuriiii
Inawezekana.

Nimeona harrier ya 1999 imenunuliwa 2012 ikiwa na 30.000Km hadi sasa 2019 ina 50.000Km.

Ingetumiwa na mtu mwingine ingeshafika 150.000Km.
 
Haingii akili gari ya 2004 leo inakilomita 45000...
Wapakiii tu mda wote
Wanachezea hizo meter kuna jamaa yangu kauza spacio yake mwezi wa nne leo ipo yard mpya kabisa na km zimepungua na kubaki 45,000
 
Gari unaweza kuipaki ila ukiwa unaendelea kuifanyia service mara kwa mara hata baada ya miaka 10 itaonekana bado nzuri... mazingira yanachangia kutunza gari...

Kitunze kudumu...

Cc: mahondaw
 
Nilinunua gari ya 2005 Japan ikiwa na 43,000 Km. Japan hawachezei mileage ila usinunue gari used Tanzania ukategemea utapata genuine mileage
Hapa Bongo labda ununue gari kwa mtu unaejuana nae au ubahatishe gari kwa mtu mstaarabu anaejua magari. Nimenunua gari kwa mwana ina 190k+ kms ila very well maintained inaweza kuzipita gari nyingi za >80k kms kwa ubora.
Napeta nayo tu.
 
Yes, ni bora kabisa ununue kwa mtu unaemjua...mie niliuza gari ya mwaka 2000 kwa dalali ikiwa na 190,000 km
Baada ya wiki naiona kwenye mtandao ina 85,000 km.
 
Developed world watu wana magari matatu matatu na zaidi
 
Alphard, Crown nyingi ukiagiza mwenyewe km huwa zinasoma 100000 na zaidi
Ukienda Yard unapigwa kuwa hii imetembea km 45k tu tena wakikuona wa kuja wanakwambia hii ya mwaka 2015
Wanakuonesha na Mkanda kumbe Mkanda wamecherehani Kkoo
 
Nilinunua gari toka Japan 2014 mileage ikionesha imetembea 86,000km. Baada ya documents za gari kutumwa toka Japan, kuna document moja ilionesha idadi ya watu waliowahi kuimiliki hiyo gari na kwa kila mmoja, ilionesha alitembea nayo muda gani.

Wa kwanza alitembea nayo 90,000km, wa pili ambaye ndio mileage yake ilionekana kwenye picha, ilikuwa hiyo 86,000km. Ukijumlisha, utaona ilitembea umbali gani kule. Baada ya kuitumia kama mwaka huku, ikaanza kupoteza kumbukumbu ya mileage, injini ikafail kwenye piston rings, oil ikawa inavuja hadi kwenye combustion chamber. Ilibidi kufanya overhaul.

Bado ninaitumia hadi leo, overhaul ilitatua matatizo mengi, ila ilinipa changamoto kadhaa. Hizo mileage unazoona kwenye picha, huenda zikawa za owner wa pili au hata wa tatu.
 
Wakuu nimekua nikiona gari zinauzwa mtandaoni mfano gari ya mwaka 1999... Lakini ina kilometa 45000 sasa ninachojiuliza inamana ilitengenezwa 1999 ikawa ina park tu ama wanafanyaje huko kwa wenzetu..
Mana huku ukipaki kigari chako miezi 6 complication kibao
Tuende kwenye uhalisia sasa... Hapa tunakuja kwenye hesabu mkuu...

Mwaka 1999 na sasa hivi ni mwaka 2019 so ni miaka 20 hapo au sio?

Kilometers 45,000 / 20 years unapata 2250 kilometers per year... Ambayo ni sawa na kilometers 6.16 per day.

Sasa, fanya huyo owner alikuwa hana gari moja... Let's say alikuwa nayo matatu hivi... Na hayo yote hayaendeshwi kila siku, uwezekano wa kuwa na hizo kilometers 45,000 for over 20 years ni mkubwa tu...

Lakini Ukumbuke pia wenzetu infrastructures zao ni nzuri kushinda za kwetu... Lakini pia wana means of transportation nzuri tu kiasi kwamba hata akiacja gari nyumbani haoni tabu sana mfano presence ya train za umeme.
 
Back
Top Bottom