Nilinunua gari toka Japan 2014 mileage ikionesha imetembea 86,000km. Baada ya documents za gari kutumwa toka Japan, kuna document moja ilionesha idadi ya watu waliowahi kuimiliki hiyo gari na kwa kila mmoja, ilionesha alitembea nayo muda gani.
Wa kwanza alitembea nayo 90,000km, wa pili ambaye ndio mileage yake ilionekana kwenye picha, ilikuwa hiyo 86,000km. Ukijumlisha, utaona ilitembea umbali gani kule. Baada ya kuitumia kama mwaka huku, ikaanza kupoteza kumbukumbu ya mileage, injini ikafail kwenye piston rings, oil ikawa inavuja hadi kwenye combustion chamber. Ilibidi kufanya overhaul.
Bado ninaitumia hadi leo, overhaul ilitatua matatizo mengi, ila ilinipa changamoto kadhaa. Hizo mileage unazoona kwenye picha, huenda zikawa za owner wa pili au hata wa tatu.