Kilwa Beach Lodge iweke tangazo rasmi kama haitaki waafrika na watanzania

We unaenda sumbuwa watu kuuliza uliza bei ukiambiwa soda elf kumi unaanza kulalamika ukinunua unakaa lisaa watu wakose pa kukaa, ila iko ki eneo kipigwe moto tu ubaguzi hatutaki peiod
 
Ushimen Huwa sijawah soma comment yako kwenye Uzi wowote bila kucheka sijui kichwani mwako Kuna Nini 😃😃😃
Hata waifu hua ananiambia kwamba......
Nanukuu: Sijui hua unawaza nini kwenye kila uzi unapo comment, maana hautumii akili....😜
Then minamjibu tu "sababu sna akili"...🤣
 
Sasa wao wanabagua live bila chenga
Kwa mfano kwa taarifa hii uliyoitoa mtu yeyote atakayeenda maeneo hayo,ataenda kwa jicho la uchunguzi.
Ikitokea akafanyiwa lolote hata kwa bahati mbaya picha atakayoipata ni ile aliyowahi sikia.
Jambo hili ni hatari sana kwenye biashara ya hoteli,
Ndo maana mahotel yanayojitambua,ikitokea waiter akawa na lugha mbaya kwa wageni na akalalamikiwa zaidi ya mara tatu mtu huyo,hupumzishwa kazi.

Wakati mwingine mgeni aliyelalalmikia jambo fulani hupewa hata offer,kama vile free lunch etc
ili kufuta asiondoke na picha mbaya akawaaribia biashara huko aendako.
Ni hayo tuu,huyo muacheni muda utaongea.
 
Sio watanzania, sema Kilwa beach lodge haitaki wamakonde.. huoni kondeboi anavyotuaibisha mitandaoni?
 
Ndugu yangu umeruka steji, ukifika lodge unatakiwa kupokelewa kuanzia unavyoshuka kwenye gari. Rudi ulingoni kaza na endelea kupambana utafikia steji ya kufika hapo kulwa lodge.
 
Wabongo unaweza kuta wanaenda hapo alafu wanaanza tena kulalamikia gharama juu tena unaweza kuta hata wanauliza kuna nini cha gharama hadi kuwa bei hii?

Kumbe huo upekee anaoutengeneza huyo mwenye biashara ndio unaomuingizia hela.

Hicho unachotaka wewe cha kuweka tangazo kina kanuni zake hakipo ila gharama ndio zitakuweka kando.

Madaraja yapo duniani kote hata huko masaki kuna sehemu utakuta white wamejaa ukadhani ni sehemu maalumu ila ukwasi ndio unafanya wengine wakae kando.
 
Nilishawahi kulala hapo.
Kumbe wana mambo ya kise£nge hivyo?
Basi next time nikibahatika tena kulala hapo asubuhi nakata gogo nalifunika na mto afu nalog out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…