Kilwa: Kutoka mji bora hadi magofu yasiyo na faida

Kilwa: Kutoka mji bora hadi magofu yasiyo na faida

Joined
Dec 31, 2022
Posts
44
Reaction score
44
Habari zenu wanaJF, natumai hamjambo na kila mtu yupo zake vema katika kupambania kombe.

Leo kama mada inavyosema nilitaka nipate zaidi ya nikijuacho ikiwezekana nifute nilichonacho au niongezee kwacho kuhusiana na ni nini kiliufanya mji wa Kilwa kutoka katika Heshima yake na kurudi katika Dharau yake na kutokutamanika haswaa.

Historia inaonyesha wazi ukifika Kilwa kisiwani ukaangalia masalia ya Mijengo iliyokuwepo zama zile, utakubariana na 𝙄𝙗𝙣 𝘽𝙖𝙩𝙪𝙩𝙖 kuwa Kilwa lilikuwa Jiji.

Kuna Muda waislaamu wa Afrika walipaita Kilwa 𝗠𝗔𝗞𝗞𝗔 𝗬𝗔 𝗔𝗙𝗥𝗜𝗞𝗔 kutokana na Wingi na ukubwa wa Misikiti iliyokuwa imejengwa ikajengeka ndani ya Kilwa Kisiwani, ambayo mpaka leo inastaajabisha Foundation yake.

Hapo alipofika Ibn Batuta akasema, "𝐖𝐚𝐥𝐥𝐚𝐡𝐢 (𝐧𝐚𝐚𝐩𝐚 𝐬𝐢𝐣𝐚𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐦𝐳𝐮𝐮𝐫𝐢 𝐧𝐚 𝐧𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨𝐮𝐩𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐮𝐳𝐮𝐧𝐠𝐮𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐌𝐣𝐢 𝐡𝐮𝐮 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐥𝐰𝐚.... 𝐊𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐦𝐣𝐢 𝐡𝐮𝐮 𝐮𝐧𝐚 𝐮𝐬𝐭𝐚𝐚𝐫𝐚𝐛𝐮 𝐧𝐚 𝐡𝐞𝐬𝐡𝐢𝐦𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐞 ...."

Hiyo ni miaka ya 1880's leo hii Mimi hapa, wa miaka ya 2000's huwezi kunishawishi kukaa katika Kisiwa kile, si Mimi tu hata Ibn Batuta mwenyewe akifufuka hawezi kupasifia kwa namna hii tena.

Nilijaribu kufuatilia ni nini kilikuwa mpaka pakarudi chini kabisaa? Sikyona Labda kuna vita iliyotokea watu wakaukimbia mji wake, sikuona ugonjwa ulotokea, sikuona siasa chafu za maudhi kama za leo labda zikawakera wananchi wakauhama, badala yake, naliona 𝙐𝙙𝙞𝙣𝙞 𝙬𝙖 𝙫𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙯𝙞 walokuwepo zama zile, ubaguzi wa Uafrika na Uarabu (𝘼𝙛𝙧𝙖𝙗𝙞𝙖). Hivi ndivyo vinatajwa kwa wingi kiwa viliurudisha na kuuvurugavuruga mji huu ili miji mingine iweze kuanzishwa na kukua, miji gani? Miji waloitaka wao, miji waloipenda wao.

Kabla sijakubariana na wanahistoria hawa, ikabidi nitafute ni nini ushahidi wa hayo, nikajikuta nakutana na kauli ya "𝑺𝒊 𝒕𝒖 𝒌𝑲𝒊𝒍𝒘𝒂 𝒊𝒍𝒊𝒚𝒐𝒅𝒉𝒐𝒐𝒇𝒊𝒔𝒉𝒘 𝒊𝒔𝒊𝒆𝒏𝒅𝒆𝒍𝒆𝒆, 𝒍𝒂𝒂 𝒃𝒂𝒍𝒊 𝑴𝒊𝒌𝒐𝒂 𝒚𝒂 𝑲𝒖𝒔𝒊𝒏𝒊 𝒚𝒐𝒕𝒆.... 𝑴𝒇𝒂𝒏𝒐 𝑴𝒕𝒘𝒂𝒓𝒂 𝒊𝒍𝒊𝒕𝒐𝒍𝒆𝒘𝒂 𝑭𝒆𝒅𝒉𝒂 𝒏𝒂 𝒘𝒂𝒂𝒓𝒂𝒃𝒖 𝒑𝒂𝒌𝒂𝒋𝒆𝒏𝒈𝒘𝒆 𝑹𝒆𝒍𝒊 𝒚𝒂 𝒌𝒖𝒕𝒐𝒌𝒂 𝑵𝒂𝒄𝒉𝒊𝒏𝒈𝒘𝒆𝒂 𝒉𝒂𝒅𝒊 𝑩𝒂𝒏𝒅𝒂𝒓𝒊𝒏𝒊 𝒏𝒂 𝒊𝒏𝒈𝒆𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒊 𝑹𝒆𝒍𝒊 𝒚𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒏𝒛𝒂 𝑬.𝑨, 𝒍𝒂𝒌𝒊𝒏𝒊 𝑹𝒂𝒊𝒔 𝒂𝒍𝒊𝒌𝒂𝒕𝒂𝒂 na 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒅𝒂 𝒌𝒖𝒋𝒆𝒏𝒈𝒂 𝑯𝒐𝒔𝒑𝒊𝒕𝒂𝒍𝒊 𝒚𝒂 𝑩𝒖𝒈𝒂𝒏𝒅𝒐 𝑴𝒘𝒂𝒏𝒛𝒂, 𝒉𝒊𝒊 𝒏𝒅𝒊𝒚𝒐 𝒉𝒊𝒔𝒕𝒐𝒓𝒊𝒂 𝒎𝒔𝒊𝒚𝒐𝒘𝒆𝒛𝒂 𝒌𝒖𝒋𝒍𝒊𝒋𝒖𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂𝒏𝒚𝒊....." Huyu ni Hassan Ilunga Kapungu.

Wanahistoria ni wengi na ushahidi wao ni mwingi juu ya haya, Nilipata kusikiliza hata 𝙏𝙝𝙚 𝙨𝙩𝙤𝙧𝙮 𝙗𝙤𝙤𝙠 ya WCB ya Jamaal Mustafa (Profesa) iliyookuwa ikizungumza kuhusu Kilwa amabyo hii haikutaja 𝙣𝙞 𝙣𝙞𝙣𝙞 𝙠𝙞𝙡𝙞𝙪𝙛𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙢𝙟𝙞 𝙝𝙪𝙪 𝙪𝙖𝙣𝙜𝙪𝙠𝙚? Bali iliishia tu kutaja Utukufu waHistoria yake na Utukufu wa Wakazi wake wa Zama zile.

Hapa nataka kujua 𝙉𝙞 𝙣𝙞𝙣𝙞 𝙪𝙣𝙖𝙠𝙞𝙟𝙪𝙖 𝙠𝙪𝙝𝙪𝙨𝙪 𝙢𝙟𝙞 𝙝𝙪𝙪 𝙬𝙖 𝙆𝙞𝙡𝙬𝙖? 𝙉𝙞 𝙠𝙬𝙚𝙡𝙞 𝙪𝙣𝙖𝙖𝙢𝙞𝙣𝙞 𝙪𝙡𝙞𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙈𝙩𝙖𝙠𝙖𝙩𝙞𝙛𝙪 𝙫𝙞𝙡𝙚 𝙪𝙩𝙖𝙟𝙬𝙖𝙫𝙮𝙤? Kama ndiyo, 𝙉𝙞 𝙠𝙞𝙥𝙞 𝙠𝙞𝙡𝙞𝙪𝙖𝙣𝙜𝙪𝙨𝙝𝙖?

𝙱𝚊𝚍𝚎𝚎'𝚞𝚣𝚊𝚊𝚖𝚊𝚗
p1080591-900x675.jpg
 
Habari zenu wanaJF, natumahi hamjambo na kila mtu yupo zake vema katika kupambania kombe.

Leo kama mada inavyosema nilitaka nipate zaidi ya nikijuacho ikiwezekana nifute nilichonacho au niongezee kwacho kuhusiana na ni nini kiliufanya mji wa Kilwa kutoka katika Heshima yake na kurudi katika Dharau yake na kutokutamanika haswaa...

Ila wa vaakobasi ni washenzi sana acha kupotosha kuhusu suala la reli ya nachingwea to mikindani mtwara ilijengwa na mwingereza kwa lengo la kusafirisha karanga kutoka nachingwea kufikia bandari ya mikindani ili zizafiriswe kwenda ulaya kwaajili ya kusindika mafuta ya kupikia.

Reli ilingolewa na watu wa kusini wenyewe baada ya uhuru

Acha upotoshaji
 
Ila wa vaakobasi ni washenzi sana acha kupotosha kuhusu suala la reli ya nachingwea to mikindani mtwara ilijengwa na mwingereza kwa lengo la kusafirisha karanga kutoka nachingwea kufikia bandari ya mikindani ili zizafiriswe kwenda ulaya kwaajili ya kusindika mafuta ya kupikia...
Hapo upotoshaji ni upi, 𝙍𝙚𝙡𝙞 𝙞𝙡𝙞𝙗𝙤𝙢𝙤𝙡𝙚𝙬𝙖 𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙬𝙖𝙠𝙪𝙨𝙞𝙣𝙞 𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚𝙬𝙚, mbona kauli hii ni dhaifu sana, unataka useme Watu wa kusini ni wajinga wa kuchukia maendeleo kiasi hicho?

Je! Kama kweli usemayo, Serikali ilichukua hatua gani kwa watu hao? Au ilifurahi pia??

Nijibu wala usitangulize matusi vaa hekima
 
Mradi wa kilimo cha karanga ulikufa baada ya Tanganyika kupata uhuru reli ikabaki kuota vichaka wahuni wakaanza kubeba mataruma ndio ngoma ikaishia hapo.
 
Mradi wa kilimo cha karanga ulikufa baada ya Tanganyika kupata uhuru reli ikabaki kuota vichaka wahuni wakaanza kubeba mataruma ndio ngoma ikaishia hapo
Safi sana Ndugu, kama kuna Point naipata hapa. Ila nmeongea na mzee mmoja nisingependa kumtaja jina, ila ni mkazi na mzawa wa Mtwara, Masasi Jida Tandale, yeye anasema:

"𝙉𝙞 𝙠𝙬𝙚𝙡𝙞 𝙧𝙚𝙡𝙞 𝙞𝙡𝙞𝙗𝙤𝙢𝙤𝙡𝙚𝙬𝙖, 𝙡𝙖𝙠𝙞𝙣𝙞 𝙢𝙗𝙤𝙢𝙤𝙖𝙟𝙞 𝙝𝙖𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙢𝙬𝙖𝙣𝙖𝙣𝙘𝙝𝙞 𝙮𝙚𝙮𝙤𝙩𝙚, 𝙗𝙖𝙡𝙞 𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙣𝙘𝙝𝙞 𝙮𝙖𝙤 𝙬𝙖𝙡𝙞𝙗𝙤𝙢𝙤𝙖, 𝙗𝙖𝙖𝙙𝙖 𝙮𝙖 𝙢𝙧𝙖𝙙𝙞 𝙬𝙖 𝙠𝙖𝙧𝙖𝙣𝙜𝙖 𝙬𝙖 𝙣𝙖𝙘𝙝𝙞𝙣𝙜𝙬𝙚𝙖 𝙠𝙪𝙝𝙖𝙧𝙞𝙗𝙞𝙠𝙖.

𝙈𝙧𝙖𝙙𝙞 𝙪𝙡𝙞𝙝𝙖𝙧𝙞𝙗𝙞𝙠𝙖 𝙠𝙬𝙖𝙨𝙖𝙗𝙖𝙗𝙪 𝙢𝙖𝙨𝙝𝙖𝙢𝙗𝙖 𝙮𝙖𝙡𝙞𝙟𝙖𝙖 𝙥𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙬𝙚𝙣𝙜𝙞 𝙨𝙖𝙣𝙖, 𝙣𝙖 𝙠𝙖𝙗𝙡𝙖 𝙮𝙖 𝙝𝙖𝙥𝙤 𝙢𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪𝙗𝙖𝙡𝙞𝙥𝙖𝙣𝙙𝙞𝙠𝙞𝙯𝙖𝙫𝙖𝙞𝙣𝙖 𝙣𝙮𝙞𝙣𝙜𝙞𝙗𝙯𝙖 𝙣𝙮𝙤𝙠𝙖 𝙬𝙖𝙡𝙖𝙤 𝙥𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙞𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙯𝙪𝙞𝙖 𝙪𝙝𝙖𝙧𝙞𝙗𝙞𝙛𝙪 𝙝𝙪𝙤, 𝙣𝙙𝙞𝙮𝙤 𝙢𝙖𝙖𝙣𝙖 𝙢𝙥𝙖𝙠𝙖 𝙡𝙚𝙤 𝙉𝙖𝙘𝙝𝙞𝙣𝙜𝙬𝙚𝙖 𝙠𝙪𝙣𝙖 𝙖𝙞𝙣𝙖 𝙣𝙮𝙞𝙣𝙜𝙞𝙗𝙨𝙖𝙣𝙖 𝙯𝙖 𝙣𝙮𝙤𝙠𝙖.

𝙈𝙧𝙖𝙙𝙞 𝙪𝙡𝙞𝙥𝙤𝙛𝙚𝙡𝙞, 𝙝𝙖𝙪𝙠𝙪𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙯𝙬𝙖 𝙞𝙟𝙖𝙥𝙤𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙆𝙖𝙧𝙖𝙣𝙜𝙖 𝙯𝙞𝙡𝙞𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙗𝙖𝙙𝙤 𝙯𝙞𝙣𝙖𝙬𝙚𝙠𝙖 𝙨𝙖𝙣𝙖 𝙗𝙬𝙖𝙣𝙖 𝙬𝙚𝙬𝙚! 𝙄𝙡𝙖 𝙣𝙙𝙤 𝙝𝙞𝙫𝙮𝙤 𝙨𝙚𝙧𝙞𝙠𝙖𝙡𝙞 𝙬𝙖𝙡𝙞𝙮𝙖𝙛𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙠𝙖𝙢𝙗𝙞 𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙟𝙚𝙨𝙝𝙞, 𝙣𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙖𝙟𝙞𝙡𝙞 𝙮𝙖 𝙈𝙞𝙡𝙡𝙞𝙩𝙖𝙧𝙮 𝘾𝙤𝙫𝙚𝙧, 𝙠𝙖𝙢𝙖 𝙞𝙡𝙞𝙫𝙮𝙤, 𝙬𝙖𝙠𝙖𝙗𝙤𝙢𝙤𝙖 𝙧𝙚𝙡𝙞 𝙞𝙡𝙞 𝙥𝙖𝙨𝙞𝙩𝙚𝙢𝙗𝙚𝙡𝙚𝙬𝙬 𝙨𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙬𝙖𝙣𝙞 𝙞𝙡𝙞𝙛𝙖𝙣𝙮𝙬𝙖 𝙢𝙞𝙠𝙤𝙖𝙗𝙮𝙖 𝙠𝙪𝙨𝙞𝙣𝙞 𝙣𝙞 𝙢𝙞𝙠𝙤𝙖𝙗𝙮𝙖 𝙑𝙞𝙩𝙖, 𝙠𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙞𝙠𝙤 𝙢𝙞𝙥𝙖𝙠𝙖𝙣𝙞"

Hapa nikaelewa kidogo, kama usemavyo, Reli ilibomolewa, ila mpaka sa hizi mkanganyiko ni Nani aliyebomoa? Kwanini wananchi wasishughulikiwe? Au kwanini serikali wabomoe na kuharibu miundo mbinu kwakisingizio cha makambi ya vita na hadi leo hakuna vita yeyote iliwahi kutokakea maeneo hayo? Walikuwa wanazungumza vita ipi?

Na tusisahau mada:
𝙉𝙞 𝙠𝙞𝙥𝙞 𝙠𝙞𝙡𝙞𝙘𝙝𝙤𝙪𝙖𝙣𝙜𝙪𝙨𝙝𝙖𝙗𝙈𝙟𝙞𝙗𝙬𝙖 𝙆𝙞𝙡𝙬𝙖!!?
 
Habari zenu wanaJF, natumahi hamjambo na kila mtu yupo zake vema katika kupambania kombe.

Leo kama mada inavyosema nilitaka nipate zaidi ya nikijuacho ikiwezekana nifute nilichonacho au niongezee kwacho kuhusiana na ni nini kiliufanya mji wa Kilwa kutoka katika Heshima yake na kurudi katika Dharau yake na kutokutamanika haswaa...

Nitajie mkoa mmoja tu uliokaliwa na waarabu ulioendelea! Hakuna!

Waarabu sijui walikua wanalaana gani kila walipokua wanaweka kituo cha makazi yao wakiondoka ndiyo bas!

Anzia bagamoyo kilwa kondoa na sehem nyingine zilizojaa uarabu hamna kitu!
 
Tatizo walikuwa na ushirikina mwingi Sana .......yaani WACHAWI BALAAA
 
Safi sana Ndugu, kama kuna Point naipata hapa. Ila nmeongea na mzee mmoja nisingependa kumtaja jina, ila ni mkazi na mzawa wa Mtwara, Masasi Jida Tandale, yeye anasema...
Mimi mwenyewe ni mzaliwa wa Masasi na nimekulia pale wakati wa makuzi yangu nilipata kusikia kwamba ile reli iling'olewa na serikali ya mwl J.k Nyerere kwa sababu wanazojua wenyewe ila wananchi wanadai ni kutotaka tu mikoa ya kusini isiendelee yani ni kama chuki flani kana kwamba mikoa ya kusini sio ya Tanzania ila ni ya Msumbiji

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Nitajie mkoa mmoja tu uliokaliwa na waarabu ulioendelea! Hakuna!
Waarabu sijui walikua wanalaana gani kila walipokua wanaweka kituo cha makazi yao wakiondoka ndiyo bas!

Anzia bagamoyo kilwa kondoa na sehem nyingine zilizojaa uarabu hamna kitu!
Sio kweli chief ikumbukwe panapoitwa Dar es salaam enzi hizo Mzizima pameishi Waarabu Tanga, Mombasa na Unguja ni sehemu ambazo wameishi pia sijajua umetumia minzani ipi mkuu.
 
Kuna sehemu nilisoma ikaonyesha Mtwara ndio kulijengwa reli ya kwanza na waingereza ila nchi ilipochukua uhuru na reli ikang'olewa hadi Leo sidhani km Mtwara kuna reli na sidhani km kuna reli itajengwa kuelekea Mtwara, kosa sio la Kilwa
 
Mimi mwenyewe ni mzaliwa wa Masasi na nimekulia pale wakati wa makuzi yangu nilipata kusikia kwamba ile reli iling'olewa na serikali ya mwl J.k Nyerere kwa sababu wanazojua wenyewe ila wananchi wanadai ni kutotaka tu mikoa ya kusini isiendelee yani ni kama chuki flani kana kwamba mikoa ya kusini sio ya Tanzania ila ni ya Msumbiji

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
Ukweli ni huo chief iling'olewa na mamlaka ya nyakati sole na sio Reli tu iko mitambo kibao ilitolewa enzi za sokoine
 
Nitajie mkoa mmoja tu uliokaliwa na waarabu ulioendelea! Hakuna!
Waarabu sijui walikua wanalaana gani kila walipokua wanaweka kituo cha makazi yao wakiondoka ndiyo bas!

Anzia bagamoyo kilwa kondoa na sehem nyingine zilizojaa uarabu hamna kitu!
Dubai, Qatar, Sharjah, Zanzibar City sio Zanzibar Country

Tembelea hapo
 
Habari zenu wanaJF, natumahi hamjambo na kila mtu yupo zake vema katika kupambania kombe.

Leo kama mada inavyosema nilitaka nipate zaidi ya nikijuacho ikiwezekana nifute nilichonacho au niongezee kwacho kuhusiana na ni nini kiliufanya mji wa Kilwa kutoka katika Heshima yake na kurudi katika Dharau yake na kutokutamanika haswaa...
Acha uongo miaka ya 1880 kilwa ilikuwa ishakufa na ibn batuta alifika kilwa mwaka 1332
 
Nitajie mkoa mmoja tu uliokaliwa na waarabu ulioendelea! Hakuna!
Waarabu sijui walikua wanalaana gani kila walipokua wanaweka kituo cha makazi yao wakiondoka ndiyo bas!

Anzia bagamoyo kilwa kondoa na sehem nyingine zilizojaa uarabu hamna kitu!
Hebu we nawe acha kuongea kwa msisimko, Hawakuwa na laana yoyote, ukweli unabakia kuwa, nyumba na majengo huchakaa na kuanguka kama mji haukaliwi tena

Miji ya waarabu ipo ambayo ipo hadi leo, mfano Dar es salaam ni mji wa waarabu na upo hadi leo

Ila kuna miji zama zake ni za zamani mno na miji ilikufa toka muda kama hiyo kilwa ama bagamoyo. Kama miji hiyo ingeendelea kuwa na watu ingekuwa miji mikubwa hadi leo
 
Nitajie mkoa mmoja tu uliokaliwa na waarabu ulioendelea! Hakuna!
Waarabu sijui walikua wanalaana gani kila walipokua wanaweka kituo cha makazi yao wakiondoka ndiyo bas!

Anzia bagamoyo kilwa kondoa na sehem nyingine zilizojaa uarabu hamna kitu!
Halafu zikija takwimu za mikoa maskini mikoa ya huko huko bara ambayo mnaona halikuwa na waarabu ndio inaongoza kwa umaskini
 
Sio kweli chief ikumbukwe panapoitwa Dar es salaam enzi hizo Mzizima pameishi Waarabu Tanga, Mombasa na Unguja ni sehemu ambazo wameishi pia sijajua umetumia minzani ipi mkuu.

Tanga kuna maendeleo gan mji unajifia taratibu ule?
 
Back
Top Bottom