Debby the FEMINIST
Member
- May 4, 2020
- 32
- 37
Mahakama ya Wilaya ya Kilwa masoko mkoani Lindi imemuhukumu Muharami Ngayoma maarufu Kibwege (30) kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu watu kumwingilia kinyume na maumbile.
Hukumu hiyo ya kesi namba 27 ya mwaka 2023 imetolewa Aprili 17,2023 na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Carolini Mtui ikiwa ni baada ya kumkuta na hatia juu ya kosa hilo ambalo lipo kinyume na kifungu namba 154 kifungu kidogo cha kwanza, sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16.
Mshitakiwa amekiri kosa hilo hivyo amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa lengo la kuifanya jamii kuachana na vitendo ambavyo vinakinzana na sheria za nchi.