Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

Hebu tuache dharau za kwa Mh. Rais, kwani hawa waliokamatwa wamekamatwa na Magufuli? Hivyo tuwe na imani kabisa mama atatuvusha salama! Hawa leo watawataja wadau wao wote!
 
Ko Congo pana magari makali ya bei mbaya kumbe mengi ni uwizi toka south
 
kwa asiyefikiri sawasawa anaweza kutoa bonge la LIKE kwenye comment hii. ila kwa tunaofikiri sawasawa kuna uwezekano tukajiuliza/kuwaza yafuatayo kuhusu tukio la kukamatwa hayo madawa na comment hii ya huyu mdau aliyeitoa;

1. je, haiwezekani kwamba hiyo ilikuwa kawaida yao kwa muda mrefu tu (pengine way back 2015 huko) na ndo maana wakawa na confidence ya kusafirisha mzigo mkubwa hivyo? kwa biashara ya kujaribu tu, tena ya hatari kama hiyo, KAMWE hakuna taahira wa kujaribu kwa kiwango hicho ghafla bin vuuu tu.

2. je, haiwezekani kuwa mtoa comment huyu ndiyo wale 'wapigania legacy' wa mheshimiwa aliyetangulia na hapa amekimbilia haraka ili kuja kufifisha hongera yoyote ambayo pengine ingetolewa kwa wanausalama hawa waliofanikisha jambo hili walio chini ya mama yetu Samia? natafakari tu kwa sauti!!!

fact: wazoefu hao, hawakuanza leo wala jana!
 
Hao kipindi cha Magu walikuwa hawakamatwi, mama kaanza kazi kwa kishindo hakuna jiwe litaacha kuguswa
Walikuwa hawakamatwi au walikuwa hawatangazwi😝😝😝!!! Hao walikuwa wanakula shaba wote au wote wanapigwa ndichi kimya kimya shughuli inakuwa imeisha!
 
Hao wameyakanyaga itakua wamekimbia vita hapo fukwe za msumbiji ndio wanakotua huko na unga kupelekwa SA...wahuni wana risk aisee daah
Kwenye trillion 2 we huwezi risk mzee! 1 Billion USD usiichukulie poa
 
Hajaweka source ya habari yake achana nae!
NEWZALERT - ZAIDI YA TANI MOJA YA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN YAKAMATWA MKOANI LINDI.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya @dceatanzania kwa kushirikiana na kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekamata zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya heroin.

Dawa hizo zimekamatwa eneo la Kilwa Masoko katika Bahari ya Hindi zikisafirishwa kwa kutumia jahazi la Al Arbo.

Katika tukio hilo, watu saba wamekamatwa ambao ni
1. Jan Mohammad Miranira (Nahodha ).
2.Amir Hussein.
3. Yusiph bin Hamad.
4 Salim Bin mohammad.
5. Ikbal Pakir mohammad.
6. Jawid Nuhan Nur Mohammad.
7. Mustaphar Nowani Kadirbaksh
 
Biashara hii ni ngumu kuitokomeza.
Ina pesa ya haraka sana hio business sema ndio very risky yani! Kama kubeti ni game yenye odd 100! Ina maana 1% ikitoa umeukata ila kuchana ni 99% sure!
 
Hawa washenzi hawajaogopa hata mwezi mtukufu wao wanapiga dili chafu
 
Kumbe ndio maana kule IG kuna kajamaa kila muda kinampost hundredwatch kumbe anayake anayoyajua yeye.

Hii inchi ngumu sana.
 
Madawa tani 2 na mpunga ambao wangepata ni wa uzito kama huo daah
Jiwe katoka wameamua kucompensate mzigo ambao wangekua wamevusha ndani ya miaka 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…