Common Folk
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 909
- 4,050
Ikiwa nisipotumia VPN, digital address yangu inakuwa uchi uchi TCRA wananiona eneo niliko na nafanya nini mtandaoni, then TCRA hao hao wakanilazimisha nitumie VPN ili kuzifikia baadhi ya huduma mtandaoni walizozifungia, utaniambiaje tena nijisajili kutumia VPN ili unione nafanya nini mtandaoni? Hiyo scenario ni tunasema "Balanced Equation". Yaani, hakuna tofauti ya kutotumia VPN na kutumia VPN iliyosajiliwa.
Kwa upande wangu naona TCRA ni kama wanajitekenya wao, kisha wanataka wacheke wao.
Lengo la VPN ni mtumiaji kuficha "Digital Identity" yake. Na kwa hapa Tanzania mambo ya VPN yalikuja baada ya mamlaka kuanza kuweka restrictions kwenye contents kadha wa kadha za mitandaoni. Walianza na sites za ngono, kisha mwisho wa siku wamehamia kwenye social networks kama Clubhouse, Twitter na sasa wameifikia Jamiiforums.
Hiyo imewalazimu watumiaji wengi wa huduma hizo kutumia VPN ili "Digital Address" zao zisomeke nchi zingine ambako hizo huduma hazijazuiwa. Ikiwa wewe mamlaka umefungia huduma kwa kuiita ni illegal, utaniambiaje nijisajili kwa details zangu? Hapo ni sawa sawa na kuniambia nijipeleke machinjioni mwenyewe nikaelekezwe kibla.