Kimara inaharibu taswira ya jiji la Dar, serikali haioni hii aibu?

Kwani Rostam anasemaje?
 
Nenda kawajengee
 
Siyo kimara pekee
Hiyo barabara kutoka ubungo hadi.mwanza ni vibanda vya hovyo tu njiani. Bila kusahau airport Nyerere road mhii
 
Siyo kimara pekee
Hiyo barabara kutoka ubungo hadi.mwanza ni vibanda vya hovyo tu njiani. Bila kusahau airport Nyerere road mhii
Kwa kifupi mleta mada ameionea tu kimara kuifanya ya hovyo wakati hili ni tatizo la kitaifa.

Hii nchi imeoza Kila mahali. Sasa unaona kutoka ubungo,Dar hadi makoroboi Mwanza ni mabanda na slums za kutosha.
 
Ngoja kwanza tumalizane na bwana polepole anatuvuruga sana
 
Sehemu kubwa Dar inatakiwa ivunjwe yote ipangwe upya ukiondoa zile sehemu ambazo baadhi zimepimwa kama Mbweni ,Kibada ,Kinyerezi ,Masaki,mkikocheni ,oyserbay etc
 
Bora hata huko, hivi ukiwauliza wakazi wa Kibaha kwamba Kibaha Mjini ni wapi, wakikuonesha uje nimekaa paleee. Kuna mikoa ukisema unaenda mjini ukifika kweli utasema kweli ni mjini. Utaona mpangilio wa upatikanaji wa huduma mbali mbali, utaona mpangilio wa majengo ya ofisi mabali mbali, utapata restaurant za maana, hoteli, maduka ya vitu mbalibmbali, ofisi za taasisi za serikali. Niiombe sana serikali ipange na kuujenga huu mji uwe wa kuvutia ukiwa bado haujavurugika zaidi. Hili pori la kuanzia hapa Ofisi za Dawasa mpaka Pichabya ndege, linachangia sana kuuharibu huu mji , halafu ni pori lililo barabarani bora Please please.
 
Kwa kifupi mleta mada ameionea tu kimara kunifanya ya hovyo wakati hili ni tatizo la kitaifa.

Hii nchi imeoza Kila mahali. Sasa unaona kutoka ubungo,Dar hadi makoroboi Mwanza ni mabanda na slums za kutosha.
True yaani ukipita kwa mfano moro. Dumila hiyo. Kibaigwa, dom. Singidaa shinyanga.ahaha ha utachoka na mabanda yasiyoeleweka barabarani
 
labda kama kuna namna ya kuwasaidia makazi yao yawe bora.
hembu fikiria mtu aliyejenga kwa taabu na kwa muda mrefu tu,ili apate pa kujisitiri. then aambiwe akarabati kisasa zaidi au ahame jiji, yamkini inakuwa sio poa.

wakishirikishwa kwa ruzuku na elimu watajenga tu. ila ikumbukwa hata huko ughaibuni makazi holela yapo vilevile.
 
Pamoja na uzuri wa baadhi ya maeneo hasa katikati ya mji lakini pia Dar ina maeneo mengi ya hovyo kabisa hasa kama ni mgeni umetoka mkoani basi unajua Dar imejengeka Kila kona kumbe hata maeneo ya hovyo yapo
Tena mengi sana, na ni sababu ya uzembe tu ya mamlaka zetu hawataki kufikiria nje ya box
 
Ni kweli mkuu,nimepataja kimara kwa sababu ndio njia kuu kutoka na kuingia Dar kutokea nchi zote za kusini mwa Afrika na kati pia. Huko kwingine hata manzese panaleta tumaini sababu kwa sasa watu wanapajenga panaanza kuwa na muonekano hata wa shopping centers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…