Wanabodi (kwa sauti ya Paskali Mayalla a.k.a Njaa), kati ya vitu vilivyobaki vinachafua taswira nzuri ya jiji la Dar basi ni kimara. Yaani pembezoni mwa barabara hapaeleweki ni ma vibanda tu na vinyumba vyenye mabati yenye kutu hadi unajiuliza hivi shida ni nini? Mbona hata manzese siku hizi panapenndeza?
Mbona bagamoyo road yote inapendeza? Yaani kuanzia kimara mwisho hadi ubungo interchange hakuna kitu cha maana cha kuleta taswira ya kuvutia kwamba sasa upo Dar, na mbaya zaidi hii ndio njia kuu ya wageni wote wanaotokea nchi za kusini mwa Africa na kati.
Inamaana serikali haijaliona hili na hawaoni aibu pia? Pale ubungo interchange karibu na kituo cha daladala cha 'maji' zilipo ofisi za zamani za DAWASA yamejaa mabanda na vijumba vikuukuu visivyo na mbele wala nyuma, hivi serikali mmeshindwa hata kuwahamisha mkafanya kitu cha maana? Tuondoleeni hii aibu bana mbona mnakua kama hamtembeagi kwenye miji ya nchi nyingine hata za jirani tu.