Tanga, Tanzania
Sheikh Makarama atetea Maendeleo ya Vitu
Sheikh maarufu wa jiji la Tanga atetea sera za mgombea wa CCM Urais Mh. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuegemea na kuleta Maendeleo ya Vitu kama miundo mbinu ya barabara, reli, bandari na kuuliza ni kitu gani kingine wanaTanga kitawafanya wamtupe Mh. Magufuli 2020.
Sheikh Hassan Makarama adai kwa Tanga wameridhika na itakuwa ngumu mtu mwingine jijini Tanga kupata wadhamini wa kumbeba kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheikh Makarama asema wakaazi wa mji wa Tanga hawawezi kukaa mabarabarani kupigwa / kuungua jua na mvua kumsubiri mpinzani wa Mh. John Pombe Joseph Magufuli.
Sheikh Khassan Makarama amesema sasa Tanga shule zimekuwa nyingi kuliko madrasa . Sheikh Makarama ampongeza Augustine Lyatonga Mrema kwa kumpendekeza Magufuli kuwa mgombea wa urais kupitia 'TLP' .
Sheikh Khassan Makarama hata hivyo amehitimisha hotuba yake kwa kumpongeza Tundu Lissu kwa ushupavu wake.