Vipi zile story za "jogoo oyee!" au "jee nyinyi mnataka kupanuliwa?" Watanzania bado wanahamu ya kuzisikia?Huyu jamaa kila neno analoongea linatafakarisha na ni chakula cha ubongo!
Yaani Lissu sasa anawazindua watanzania kutoka katika usingizi mzito wa propaganda za Magufuli na chama chake!
Tafuta malimau umeze ili uweze kupumua, usiyempenda kajaaa....Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji, Chadema na Lissu Ni kelele za chura tu
Jipe matumaini maana Tsunami ikija utatafuta njia zote usizione...Bado munaamini kwenye siasa za mafuriko? Muulizeni Slaa na Lowassa. Ccm itashinda asubuhi tu.
Yawezekana wewe miaka 5 hii ilikuwa ya kheri kwako basi mpigie aliye nuru kwako.Ngoja tuone mkuu. Wote tuwe wapole kwenye kisanduku cha kupigia kura. Mutampigia kura mgombea wenu, na sisi wananchi tutampigia kura rais wetu. Nasisitiza kwenye matokeo tuwe wapole.
Tanga ni kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa sana lakini kama Kawaida imekosa Maendeleo tangu Mkoloni alipoondoka. Hakuna miundo Mbinu bora japo kuna Ardhi nzuri yenye Rutuba iliyoporwa na na Mabeberu na kupandwa mkonge. Tupo bilionea namba moja Mo aliyewekeza kwenye mkonge kwa malaki ya hekari lakini hakuna miundombinu hata madaraja ni hafifu .Leo Mgombea uraisi wa CHADEMA, Tundu Lissu baada ya kufanikiwa kupata zaidi ya wadhamini 6000 huko Same, Leo alipita Muheza mkoani Tanga.
Kama kawaida akaendelea kugawa dozi ya elimu ya mambo ya uraia kwa wananchi wa Tanga.
Huku wakimsikiliza kwa makini, na kwa kuyatafakari maneno yake, Mheshimiwa Lissu ameelezea uhusiano wake na mkoa wa Tanga ambapo anasema ndiko alipopatia elimu yake ya kidato cha tano na sita mwaka 1987 hadi 1989 katika shule ya sekondari ya Galanos.
Unaweza kumsikiliza hapa akiwaeleza wananchi juu ya magumu ambayo nchi hii imepitia chini ya utawala uliofeli kila idara wa CCM