Uchaguzi 2020 Kimbunga cha Lissu chaingia Muheza Tanga

Uchaguzi 2020 Kimbunga cha Lissu chaingia Muheza Tanga

Tanga, Tanzania

Sheikh Makarama atetea Maendeleo ya Vitu


Sheikh maarufu wa jiji la Tanga atetea sera za mgombea wa CCM Urais Mh. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuegemea na kuleta Maendeleo ya Vitu kama miundo mbinu ya barabara, reli, bandari na kuuliza ni kitu gani kingine wanaTanga kitawafanya wamtupe Mh. Magufuli 2020.

Sheikh Hassan Makarama adai kwa Tanga wameridhika na itakuwa ngumu mtu mwingine jijini Tanga kupata wadhamini wa kumbeba kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Makarama asema wakaazi wa mji wa Tanga hawawezi kukaa mabarabarani kupigwa / kuungua jua na mvua kumsubiri mpinzani wa Mh. John Pombe Joseph Magufuli.

Sheikh Khassan Makarama amesema sasa Tanga shule zimekuwa nyingi kuliko madrasa . Sheikh Makarama ampongeza Augustine Lyatonga Mrema kwa kumpendekeza Magufuli kuwa mgombea wa urais kupitia 'TLP' .

Sheikh Khassan Makarama hata hivyo amehitimisha hotuba yake kwa kumpongeza Tundu Lissu kwa ushupavu wake.
 
kaongea vizuri sana kwa lugha ambayo kila mtu atamuelewa hasa kuhusu ujenzi wa miundombinu na kutoongeza wafanyakazi mishahara pamoja na kunyanyasa na kusimanga watu wa kisingizio cha kujenga miundombinu.
 
Huyu jamaa kila neno analoongea linatafakarisha na ni chakula cha ubongo!

Yaani Lissu sasa anawazindua watanzania kutoka katika usingizi mzito wa propaganda za Jiwe na chama chake!
Fact. Fatilia maneno ya wanaccm ndio utajua jamaa kawakamataje. Yaani wanahangaika[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa kila neno analoongea linatafakarisha na ni chakula cha ubongo!

Yaani Lissu sasa anawazindua watanzania kutoka katika usingizi mzito wa propaganda za Jiwe na chama chake!
Elimu ya kiuraia ya wiki moja kutafuta wadhamini na kuchukua fomu, tayari CCM wanagwaya.

Je siku 60 mfululizo za kampeni CCM Mpya si itazimia!
Huyu jamaa ana kipaji na uwezo mkubwa wa kujieleza, achana na yule mwingine aliyepewa mahari ya jogoo kwa kumuozesha mama yake.
 
Wananchi hao hao kila ukisikiliza bunge na vikao vya madiwani ndio wanawatuma wawakilishi kwenda kuomba barabara, madaraja, umeme, zahanati, shule, maji na miundombinu mengine.

Kama hawana shida navyo kwanini bungeni asilimia kubwa ya maombi kutoka kwa wabunge iwe miundombinu tu; huyo mkoloni na maraisi waliotangulia awakuzimaliza hizo shida kwa zaidi ya 100?

Umati wenyewe naona hizo siku chache za campaign zake (yes it’s a campaign) inaonekana washasikia kila kitu hakuna shamra shamra tena; ata wale wamama wanaopazaga sauti sema baba, kweli tumewachoka, vigelegele na kutia chumvi zingine washaanza kuishiwa nguvu sijawasikia kabisa.

Just a dull political campaign watu wanajipanga akishaanza kuongea unaona hakuna spirit ya ku engage ata kwa makofi. Hana jipya yale yale kupinga tu kazi ya maendeleo.
 
Muda wa kampeni bado, huu sio mkutano ni muda wa kusalimia watu na kutafuta wadhamini , tusubiri baada ya tarehe 26 Agosti 2020 wakati geti litapofunguliwa la kuingia katika mikutano ya kampeni.
 
Leo Mgombea uraisi wa CHADEMA, Tundu Lissu baada ya kufanikiwa kupata zaidi ya wadhamini 6000 huko Same, Leo alipita Muheza mkoani Tanga.

Kama kawaida akaendelea kugawa dozi ya elimu ya mambo ya uraia kwa wananchi wa Tanga.

Huku wakimsikiliza kwa makini, na kwa kuyatafakari maneno yake, Mheshimiwa Lissu ameelezea uhusiano wake na mkoa wa Tanga ambapo anasema ndiko alipopatia elimu yake ya kidato cha tano na sita mwaka 1987 hadi 1989 katika shule ya sekondari ya Galanos.

Unaweza kumsikiliza hapa akiwaeleza wananchi juu ya magumu ambayo nchi hii imepitia chini ya utawala uliofeli kila idara wa CCM


Ukimwangalia LISU kwa macho yako na kisha ukafikilia kile alichofanyiwa (SHAMBULIZI), Hakika lazime useme kuwa MUNGU anafanyakazi kwenye maisha ya watu hapa duniani.
 
Hakuna lolote lilie Lissu kaongea hapo Muheza, zaidi anazidi kupandikiza chuki tu kwa wananchi hapo ili hali nao wanaona kazi inakwenda kwa kasi na ujenzi wa taifa!
Kodi ya mtanzania inatumika vyema tofaut na awamu zotee

Jpm sio Mungu bali makosa ya kibinadamu yapo tu ya kitamushi
Zaidi JPM licha ya mapungufu yake lkn kafanya kazi kubwa mno

Oooh! Kasema watu walikuwa wanalia njaa nikakumbuka namna alivo pigia chapuo kipindi hicho et wananchi wanalia njaa lkn hapakuwepo na yeyote aliyeripotiwa kafa na njaa😂😂😂😂

JPM alikaza kama alivokaza kwa Zito kuishinikiza nchi iingie lockdown kipindi cha Corona😂😂😂😂😂
Jiwe jiwe tu hapangiwi na anasimamia msimamo haswaaa😂😂😂😂
Nadhani Lissu jipange kwa sera zaidi nini nchi au taifa utalifanyia zaidi ya haya ya JPM, jipange haswa,
Usije shangaa JPM ataibuka na ahadi konki zaidi kwa wananchi na ni rahsi kuaminika kwani kaonesha namna alivo mtekelezaji mzuri wa ahadi zake😂😂😂😂

Jipange sana Ndg LIsu😂😂😂

Karibun kwa maoni.
 
Back
Top Bottom