Uchaguzi 2020 Kimbunga cha Lissu chaingia Muheza Tanga

Uchaguzi 2020 Kimbunga cha Lissu chaingia Muheza Tanga

Uzuri bunge siku hizi limekuwa la uwazi kweli pamoja na makelele ya watu wanaojiita wanaharakati.

Kila swali na mchango wa mmbunge wananchi wanaona. Mfano maswali ya kihehere mmoja kutoka CDM, John Mnyika yanapatikana hapa👇

Bunge Polis

Asilimia kubwa ya maswali ya Mnyika ni barabara, maji, elimu, ardhi na afya; yanachukua kama 95% ya maswali yote aliyouliza mwaka huu yanayohusiana na Kibamba.
.................................................................................

Huyo Lissu aje alete michango ya mmbunge wowote wa CDM tu ambayo kwa ujumuisho wake aifiki 80% kuhusiana na maswala ya afya, elimu, umeme na miundombinu mengine). Akumbuke tu michango ya kila mtu ipo on record.

Hayo anayobeza ndio mambo watanzania wanataka kwa sasa. Tatizo sijui kama bunge wana statistics za majumuisho ni wapi kuna changiwa zaidi ili aonyeshewe upuuzi anao ongea.

Huyu mtu ni mwanaharakati tu hajui shida halisi za watanzania or what it takes to propel an economy yeye ni kuropoka tu hivi kabisa kuna watu wanadhani anafaa kwa nafasi ya uraisi.
 
Katika miaka yoooote
Huyu jamaa kila neno analoongea linatafakarisha na ni chakula cha ubongo!

Yaani Lissu sasa anawazindua watanzania kutoka katika usingizi mzito wa propaganda za Magufuli na chama chake!
Katika miaka yoooote,safari hii wapinzani wamepata mgombe sahihi kabisa,Huyu Nguli wa sheria anafundisha,anaelimisha na anatumia ujuzi wake wa sheria historia kuweka mambo sawa na kupangua hoja na mbinu haramu za CCM.
Amepangua mbinu za kutaka kumuengua kwa kuitangazia hadhira na Dunia kuwa kumuengua kisheria haiwezekani hiyo Ni pre emptive strike,au Ni technique ya kuvuruga mashambulizi.
Jamaa Ana akili za Karne ijayo.
 
Bado munaamini kwenye siasa za mafuriko? Muulizeni Slaa na Lowassa. Ccm itashinda asubuhi tu.
Tunaamini Mkuu,wacha tufurahie miaka mitano tumekua tukisikia maneno ya upande mmoja,wacha tufaidi na maneno ya upande wa pili.Fundi karudi.
Hatukupata nafasi ya sisi malofa kujumuika kwa miaka mitano wacha tujifariji na Lisu Ghost wetu.Marehemu wetu anayeishi.
Hi ndio faraja yetu mtu aliyeshinda mauti.
 
Hadi sasa Lissu amepata wadhamini wangapi?
Kama wameshafika namshauri asevu nguvu kwa ajili ya kampeni.
 
Hii ni laana. Jitu linakula mahari ya mama yake aliye kitandani amepooza halafu bila aibu linatangaza hadharani. Busara za wapi hizi? Tulikosea Sana miaka 5 iliyopita. Miaka 5 ijayo haturudii kosa. URAIS bila hekima Ni dhihaka.
Mkuu share ,hili ni kweli? Mtu amekula mahari ya mamake!!? Huyo mtu ni mzima kichwani kweli!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Mgombea uraisi wa CHADEMA, Tundu Lissu baada ya kufanikiwa kupata zaidi ya wadhamini 6000 huko Same, Leo alipita Muheza mkoani Tanga.

Kama kawaida akaendelea kugawa dozi ya elimu ya mambo ya uraia kwa wananchi wa Tanga.

Huku wakimsikiliza kwa makini, na kwa kuyatafakari maneno yake, Mheshimiwa Lissu ameelezea uhusiano wake na mkoa wa Tanga ambapo anasema ndiko alipopatia elimu yake ya kidato cha tano na sita mwaka 1987 hadi 1989 katika shule ya sekondari ya Galanos.

Unaweza kumsikiliza hapa akiwaeleza wananchi juu ya magumu ambayo nchi hii imepitia chini ya utawala uliofeli kila idara wa CCM

Ameanza kampeni mapema sana, lakini Rais ni Jpm.
 
Huyu Lissu kaja kuwazindua watanzania na propaganda za jiwe

Ndio maana hanazuia vyama vya upinzani zisifanye siasa
 
Lisu fundi,karudi kufundisha,mtaalamu wa sheria na maneno,Jamaa anajua kueleza Jambo,anajua historia,anajua kushawishi,anajua kujenga hoja.
Safari hi dunia inaenda kushuhudia maajabu.
Jiwe tupa kule.
Kinachotia huruma kwa ccm kabla ya Lisu walishajiakikishia ushindi kabla ya hata kupigwa kwa kura lakn baada ya kuwasili lisu naona wote wamepoteana, na ndio maana kinana aliwaambia wanaccm kuwa msibweteke hakuna ushindi rahisi hiyo msg ilinifikirisha mara 2.
 
Ukuona lile nyomi la jana.
Kuna nyomi Sasa? Na Ile ya lowasa ilikuwa nini,halafu ikawaje nasema nyie Ni vyura tu mnapiga kelele mtoni tembo atakunywa zake maji taratiibu Cha Domo Ni losers [emoji23][emoji1787]
 
Kuna nyomi Sasa? Na Ile ya lowasa ilikuwa nini,halafu ikawaje nasema nyie Ni vyura tu mnapiga kelele mtoni tembo atakunywa zake maji taratiibu Cha Domo Ni losers [emoji23][emoji1787]
Wewe kima acha kudandia treni kwa mbele, mimi naongelea nyomi ya Ccm uwanja wa uhuru, wewe kima sijui unaongelea nyomi lipi
 
Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji, Chadema na Lissu Ni kelele za chura tu
Jiwe akisoma hii atakuwa anakutukana... maana ingekuwa nikweli ulichoandika asingekuwa anatumia bunduki kuwazuia
 
Katika miaka yoooote
Katika miaka yoooote,safari hii wapinzani wamepata mgombe sahihi kabisa,Huyu Nguli wa sheria anafundisha,anaelimisha na anatumia ujuzi wake wa sheria historia kuweka mambo sawa na kupangua hoja na mbinu haramu za CCM.
Amepangua mbinu za kutaka kumuengua kwa kuitangazia hadhira na Dunia kuwa kumuengua kisheria haiwezekani hiyo Ni pre emptive strike,au Ni technique ya kuvuruga mashambulizi.
Jamaa Ana akili za Karne ijayo.
Unajua hauwezi kwenda mahakamani na ushahidi wa kubabaisha utayumba tuu, ndio maana kila anayechomoza anateleza Angalia Siro akifikiwa na hoja ya Lissu anaangalia chini
 
Jiwe akisoma hii atakuwa anakutukana... maana ingekuwa nikweli ulichoandika asingekuwa anatumia bunduki kuwazuia
Hivi vimaneno vyenu vya mipasho Bora mngeanzisha Cha Domo taarabu maana yamechuja Sasa tafuteni mengine magufuli Ni tembo lisu na Wana Sacco's wa chadema Ni vyura mnapiga vikelele havina madhara yeyote,ushindi kwa jembe magufuli Ni wakishindo
 
Huyu jamaa kila neno analoongea linatafakarisha na ni chakula cha ubongo!

Yaani Lissu sasa anawazindua watanzania kutoka katika usingizi mzito wa propaganda za Magufuli na chama chake!
Ukimsikiliza TL kwa utulivu, unaongeza wasiwasi wa iwapo wataruhusu agombee urais huyu mtu! Mwaka huu tunaweza kushuhudia kampeni ambazo hazijawahi kuonekana kutokea upande wa upinzani!
 
Hivi vimaneno vyenu vya mipasho Bora mngeanzisha Cha Domo taarabu maana yamechuja Sasa tafuteni mengine magufuli Ni tembo lisu na Wana Sacco's wa chadema Ni vyura mnapiga vikelele havina madhara yeyote,ushindi kwa jembe magufuli Ni wakishindo
Inawezeka ikawa mipasho yenye ukweli ndani yake maana ukiona my anachukia just kuna ukweli japo no kidogo
 
Nashkuru kwa link. Kwa kweli Lissu ndiye atayetufaa. Twendeni na genius Lissu. Kwanza akiongea vitu vyote vinatema bila shida, bila kukosea kosea. Hata kuturepresent kama nchi mtu unakuwa proud.
 
Back
Top Bottom