Kimedani: Vijana wasomi badilisheni Mbinu za kivita. Upepo wa mashambulizi umebadilika

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KIMEDANI; VIJANA WASOMI BADILISHENI MBINU ZA KIVITA. UPEPO WA MASHAMBULIZI UMEBADILIKA

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Upo kwenye Vita.
Vita vinahitaji mambo makuu yafuatayo ili ushinde;
1. Nguvu kazi(jeshi)
Jeshi ni wewe Mwenyewe!

2. Elimu, ujuzi, maarifa na mafunzo ya kivita.
Hapa utafundishwa mbinu, mipango, mikakati na mafunzo ya mapigano Mbalimbali uwapo kwenye uwanja wa mapambano, mafunzo ya matumizi ya Silaha.
a) kujua kupanga mipango na mikakati, na utekelezaji wake.
b) kujua kutumia silaha na kutengeneza silaha za kawaida Katika mazingira yoyote yanayokuzunguka uwapo vitani.
c) kunyumbulika Kwa haraka katika mapigano kulingana na mbinu za adui..

3. Kuwa na Ramani ya vita.
Hii ni muhimu Sana.
Huwezi kupigana kwenye vita ukashinda kama hauna ramani ya vita.
a) Elewa mazingira yanayokuzunguka.
b) Elewa watu wanaokuzunguka
c) Elewa sehemu potential na nyeti.
d) Elewa Dira ya eneo husika.

4. Pata taarifa sahihi kadiri iwezekanavyo.
Lazima uhakikishe unavyanzo vya uhakika vya kukupatia taarifa ambazo utazitumia kwenye kupigana na adui zako ushinde.

5. Mbinu Mbadala au Mbinu Kinzani.
Vita haipiganwi na mbinu moja au formula moja.
Hata hivyo unaweza ukawa na mbinu nyingi mbadala lakini kuna mazingira yatakulazimu utumie mbinu Kinzani ili ushinde.

Nitakupa Mfano,

Imezoeleka na kuwa sehemu ya maisha kuwa mapambano ya maisha yanahitaji uwe na umakini, utumie akili na ufanye kwa kujielewa.

Lakini kuna mazingira ya mapambano ya maisha haihitajiki akili Sana wala ujielewe Sana.
Kuna wakati unaweza kutumia Ujinga kama mbinu kinzani ya kutumia akili kushinda vita yako kirahisi.

Vijana lazima muwe Flexible, Mnyumbulike. Mbinu nyingi kama hazizai matunda basi tumia mbinu kinzani.

Jioni njema!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Uzi uko vema sana, anayeukashifu achunguzwe huenda ana ugonjwa wa wivu wa kinyegere.
 
Namba 3 nimeelewa sana.
Namba 5 pamoja na mfano wake nimeelewa zaidi.,kumbe Kuna muda inatakiwa ujizime data ili uweze kushinda baadhi ya mapambano
 
S
Sisi tuna amani ndoto ya vita ya nini?
Amani inayo letwa na watekaji na wapotezaji watu kelelele zikizidi unatupwa ambapo watakutambua kirahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…