Kimenuka: Mchezaji Geremi Njitap ataka kumtaliki mkewe baada ya kubaini watoto mapacha aliowakuza kwa miaka 16 sio wake'

Ignorance a Bliss....; Sasa hapo baada ya yote mwenye faida ni nani ? Binafsi ni true believer kwa anayetunza ndio baba wa kweli kuliko Sperm Donor yoyote.... (That's just my Perception)...; Jiulize hapo watoto wana Kosa gani Mama yao maybe (Lakini kututangazi Jamii their Dirty Laundry is not Kosher...)
 
Safi sana
 
Ndiyo maana mimi nilipima DNA watoto wangu wote kabla ya kumjengea nyumba mke wangu kwao. Nakataa kabisa kuwa siwezi na sitaki kulea mtoto wa mwanamme mwenzangu na siku nikigundua mke wangu anachapwa na mtu mwingine ndiyo mwisho wa ndoa yetu.
Swala la kuchwapwa usiwe na wasiwasi hakuna ndoa ya Miaka kumi ambayo hawajakuotea
 
M
MAandiko katika bibilia yanasema hivi

" “Ilikwisha semwa pia: ‘Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka’. Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.'

Mathayo 5:31-32


Sababu ya takala kwa mujibu wa YESU ni UZINZI.Yesu anafundiaha kuwa ukigundua / kuwa na ushahidi juu ya uzinzi wa mkeo basi MPE TALAKA fastaa.
 
Mathayo

5.31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;

5.32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Bro check vizuri biblia yako " isipokua kwa habari ya uasherati" biblia haisemi "isipokua kwa Habari ya uzinzi"

Kuna tofauti kubwa kati ya uzinzi na uasherati Mkuu

Uzinzi > ni kitendo cha wanandoa kufanya tendo la NDOA na mtu ambaye si mme au mke wake( i.e kufanya tendo la NDOA na mtu ambae si mke au mume halali)

Uasherati> ni kitendo cha watu ambao Bado hawajafunga NDOA takatifu ya AGANO kufanya Tendo la NDOA

Sasa hapa YESU alisema isipokuwa kwa sababu ya uasherati ina maana isipokua kwa watu ambao Bado hawajafunga NDOA

Mfano

Watu ambao wapo katika uchumba Bado hawajafunga NDOA mmoja wapo akifanya Tendo la NDOA na akabainika haya mahusiano ndio YESU aliyapa uhalali wa kuvunyika lakini sio mahusiano ya NDOA

Angesema isipokua kwa habari ya uzinzi hapo ingekua halali mwanandoa kuvunja NDOA pindi anapomkuta mwenzake amefanya ngono nje ya NDOA

Undugu wa mke na mume wale waliounganishwa na MUNGU haufuiiiiiii Mkuu
 
Wanawake wengi hawajui Kwamba baba mzazi ndie anae bariki

kumpa watoto baba ambaye si wao ni kuwatengenezea mazingira magumu Sana katika MAISHA yao
 
Hiyo yangu ni biblia habari njema (BHN). Nenda kafungue kamusi ya Tuki uangalie maana ya neno Uzinzi na uasherati. Inawezekana una uelewa mdogo juu ya lugha ya kiswahili.
 
Dah unapindisha sana maana ya maandiko aisee hebu rudi ukae chini usome vizuri maandiko.

Wewe unadhani kuwa wayahudi kipindi cha yesu walikuwa wakiishi kwa mahusiano ya boyfriend na girlfriend kama ilivyo sasa?

JITATHMINI sana na acha kupotosha maandiko ili kufaidisha matamanio ya nafsi yako.
 
Wanawake wengi hawajui Kwamba baba mzazi ndie anae bariki

kumpa watoto baba ambaye si wao ni kuwatengenezea mazingira magumu Sana katika MAISHA yao
What if huyo Baba ni Mme wa Mtu na kufanya unachofanya ni kuvunja familia mbili ?; What if Baba Mzazi hawataki hao watoto ? Narudia tena Mlezi anastahili pongezi za kufa mtu (na Sins of the Parents zisi-determine future ya watoto) Kwahio huyo mama kama angekuwa na Busara angeweza kukubali hata monetary-wise asipate kitu na Mwanaume sababu ushawalea kama wako / ukidhani wako..., DNA isibadilishe mapenzi yako kwao; Kosa alifanya mama yao na sio wao
 
Watoto walizaliwa miaka minne kabla ya ndoa lakini.
 
Kwa alizungumzia talaka kwa mtu ambaye hamjaoana?
 
Watoto walizaliwa miaka minne kabla ya ndoa lakini.
Kwa hiyo ndio kigezo cha kuwakubali au ulitaka wazaliwe ndani ya ndoa?

Definition ya ndoa kiserikali ukikaa na mwanamke kwa miezi sita ,tayari ushaoa.
 
Kwa hiyo ndio kigezo cha kuwakubali au ulitaka wazaliwe ndani ya ndoa?

Definition ya ndoa kiserikali ukikaa na mwanamke kwa miezi sita ,tayari ushaoa.
Unamlaumu vipi mwanamke kwa watoto aliozaa kabla hujamuoa. Mwanamke kabla hajaolewa anakuwaga na alternative
 
ndo maana hatupimi hata ngoma bora maisha yaendelee,japo vipimo vya DNA tanzania kwa mtanznia havijawahi mkataa mtoto siyo wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…