Kimetulamba kwenye written interview

Aha kwahiyo mizigo mizito wapewe walimu duh nchi ngumu hii
 
Mzee hiyo kawaida lazima ukutane na kitu kizito akili ikukae sawa, then urudi ukajipange upya kwa ajili ya mashambulizi mapya wakati ujao



Mi nilipigwa na kitu kizito nusu kudata tena bora weye hapo DUCE wengine ilitukuta Dodoma na hapo ushatumia nauli na gesti, dah njia nzima akili imevurugika ukicheki kwenye mfumo tayari ushaambiwa not selected na wenzako wametoboa basi roho inaauuuma

Ila Mungu si athumani siku hao PSRS walijichanganya wakaingia kwenye mfumo, aisee nilifumua fumua viswali vyao vyote na chenchi juu matokeo yanatoka nimekuwa kinara

Kwa jinsi walivyochoma nauli zangu nenda rudi kama zote wakafanya Dodoma pawe kama nyumbani

mbwa wale Oral sikufanya ajizi nilibamiza maswali yao yote, si unajua tena wakati wa Mungu ndio wakati sahihi? Baada ya kutoka nilimshukuru Mungu nikarudisha fuvu kitaani, the rest is history

To cut the long story short; buyu la asali limenikuta bado kuna mikeka mitatu nasikilizia shortlist na wengine wameniita siku naenda kufata barua

Wangechelewa kutoa mkeka tu hata hiyo ningelipua tu, maana kanuni ni haijaisha mpaka iiishe


All the best kwako kwenye vipengele vinavyofuatia
 
Hongera sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…