Kimeumana Bungeni! Spika Ndugai ahoji kama kuna mgao wa umeme nchini

Kimeumana Bungeni! Spika Ndugai ahoji kama kuna mgao wa umeme nchini

Hizi lawama mtazitoa sana lakini kiini cha tatizo ni umeme wa maji. Mfumo wa umeme wa maji unahitaji msururu wa miundombinu kuutoa ulipo Hadi kwenye matumizi.
Je, miundombinu yetu ni ya muda gani na ina hali gani???
Tatizo lingine la pili sambamba na la kwanza ni zile harakati za ghafla za kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kupitia mipango wa REA. Kama plani ilikuwepo ilikuwa ni ya kukurupuka sana kumfurahisha mfalme.
Tatu; kama kuna mgawo wa maji Dar es Salaam kisa ukame kwenye vyanzo unadhani hali itakuwaje tofauti kwenye mabwawa kuzalishia umeme.
Kama unapata umeme hapo ulipo.. Fahamu kuwa TANESCO wamefanya jitihada kubwa sana!

Tunatokaje hapa tulipo: umeme wetu wa maji uongezewe vyanzo mbadala kama gesi na jua (solar), upepo, n.k
Tusipokuwa makini Huko tuendako ipo siku tutakuwa gizani. Na itakuwa balaa!
 
Kwamba scheduled maintanance haikufanyika ila mitambo haikuharibika na ilifanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu😂 ila kwa sasa inafanyiwa maintanance hali ya kuwa haijaharibika?

Hahahah hii awamu hii itakuwa na vioja vya aina yake.

Jamaa anasema kwa sasa mgao upo kwa wingi kwa sababu mitambo mingi ilitembezwa pasipo kufanyiwa scheduled maintenances...walikuwa wanahofu wakizima umeme kwa sababu ya matengenezo basi bwana mkubwa angewala vichwa...
 
TANESCO inapaswa ifumuliwe yote, inaonekana baadhi ya watumishi wa Tanesco wanaihujumu Serikali, hivyo waziri na watendaji wake watupie jicho kila kona ya Tanesco
Huyu jamaa ndo anatoka usingizini anaanza kuhoji madhaifu ya serikali. 2015 - March 2021 alikuwa usingizi wa pono!
 
Makamba anatuletea story...anataka ile stock ya gen sets iishe kwanza? Maana juzi alisema wanafanya matengenezo...mbona kama hayaishi?
Kibaya na maji nayo kama yana mgao...ili yale yanayouza maji yapate wateja?
 
Usidanganye binafsi nilinunua jenereta baada ya hasira ya kukatika kwa umeme hasa muda wa mechi za ligi kuu maana nilkw na kibanda cha kuonesha mpira hyo ilkuwa 2018 kipindi Magu yupo,,nakumbuka wananchi walikata Nguzo baada ya kulalamika umeme kuunguza mota zao kila mara
Ufipa katika ubora wako, chuo kikuu cha kualumu na kutunga uwongo.

Una chuki hadi basi mzee
 
Ufipa katika ubora wako, chuo kikuu cha kualumu na kutunga uwongo.

Una chuki hadi basi mzee
Nitunge uwongo ili iweje,,,tatizo nchi imewashinda mmebaki awamu moja kuichafua awamu nyingine ili kuwazuga wanyonge kama mlivyowabatiza maana hawana uwezo wa kuwadhibiti nyie mapaka shume
 
TANESCO inapaswa ifumuliwe yote, inaonekana baadhi ya watumishi wa Tanesco wanaihujumu Serikali, hivyo waziri na watendaji wake watupie jicho kila kona ya Tanesco
Siyo TANESCO ifumiliwe bali CCM itoke kabisa,, nyani ni walewale tu na wanazidi kukua kwa kasi watamaliza shamba tusipo wawahi!!!
 
Siyo TANESCO ifumiliwe bali CCM itoke kabisa,, nyani ni walewale tu na wanazidi kukua kwa kasi watamaliza shamba tusipo wawahi!!!
Tarehe 28/10/2020 kabla haijapigwa hata kura moja, tayari CCM Wana wabunge KARIBIA 80 wa kupita bila kupingwa! Kwenye vyama vingi unapitaje bila kupingwa? Hii yote sanduku lao la kura wanategemea TISS na Polisi na Wakurugenzi, hali hii kisiasa ni ya hovyo kabisa, imetuzalishia bunge lisilo na maana yoyote sawa na kikao tu Cha kahawa mtaani.
 
You are very bright. Alipewa kishkaji kazi na jk kwa mgongo wa baba yake na kina lowasa enzi zile. Sasa anajiona ni presidential material kuliko hata VP wala PM.
Mtu kapata kazi bila hata kufanyiwa usaili. Kazi unaunganishiwa na baba yako kiushikaji. Ati leo ndo mnasema awe Rais. Ila watanzania! Si heri hata mpeni Lissu kuliko huyu ndugu ambae anakashfa ya wizi wa mitihani. Hajawahi kulijibia hili.
Kapewa wizara hakuna anachofanya wala mikakati yoyote yeye kukimbilia uarabuni. Baadae kuweka vikao na wa Norway ati wanamsifia anaakili sana alisoma marekani yaani ujinga ukisoma ktk mtandao.
 
Hana weledi na uzoefu. Kwa kupendelewa kaanzia kazi ikulu baada ya chuo. Alipewa kishikaji kazi enzi za jk. Tangu hapo anajiona presidential material na huku uwezo hana.
Presidential Material ya konyo hata amiini yani, ngoja wajichanganye waje ndo wataelewa . 😂
😂
 
Mtu kapata kazi bila hata kufanyiwa usaili. Kazi unaunganishiwa na baba yako kiushikaji. Ati leo ndo mnasema awe Rais. Ila watanzania! Si heri hata mpeni Lissu kuliko huyu ndugu ambae anakashfa ya wizi wa mitihani. Hajawahi kulijibia hili.
Kapewa wizara hakuna anachofanya wala mikakati yoyote yeye kukimbilia uarabuni. Baadae kuweka vikao na wa Norway ati wanamsifia anaakili sana alisoma marekani yaani ujinga ukisoma ktk mtandao.
Taifa bado lina ujinga mwingi. Anatakiwa kiongozi dikteta alikwamue.
 
Mjomba alipokuwa akisema anatetea wnyonge nilipinga na kuona mjomba anatuona wadhaifu..
Sasa akili ndio inafunguka neno wanyonge mjomba alimaanisha WAJINGA ila alificha hilo.yaani hii nchi ni hata mchunga ngombe anaweza kuiongoza na akachekewa tuuu
 
Nakuunga mkono, huyu waziri anavisingizio vingini visivyo na mantiki yoyote.

Suala ni kwamba mtoto wa 'elites' hakosei, kapelekwa pale kwa mbereko za baba yake ili kufanikisha biashara zao.

Eti anahujumiwa, wakati anaingia na mbwembwe za kufukuza aliowakuta kwa kuwatweza alifikiri ana akili sana na kwamba hakujua kwamba tangu 2016-Machi 2021 umeme haukuwahi kukaktika kijinga bila taarifa zozote?

Hakuna anayehujumu chochote isipokuwa jwamewekwa pale wasio na weledi wa kazi zaidi ya kuchimbua ni kwanini waliokuwepo walikuwa wanafanikiwa wameshindwa kupata jibu.

Huyo waziri aondoke kama hataki kjiuzulu basi asubiri kulengeshwa kwenye kashfa ambayo atajuta ni kwanini alikubali kupokea jukumu asiloliweza. Ukiingiza siasa kwenye kazi huwezi kufanikiwa kamwe
Mambo mengine magumu sana.Nilipanda aisi au kibasi cha kwenda ngara.Walikuwa wakilalamika wazee wawili, kama mabishano vile kuhusu umeme unavyosumbua sasa hivi.SWali wanalouliza, ni hili hili linaloulizwa humu mtandaoni.Tangu Mach 2016~ Mach 2021 haukuwahi umeme kukatika hadi vijijini.Leo imekuwaje,

Lakini mwisho kabisa mmoja akasema, kwani wewe hukumbuki yale makontena ya majenereta aliyoyazuia jiwe? Sasa wamegundua kuwa yaliingizwa nchini kihalali na wenyewe wamekabidhiwa majenereta yao ndiyo sasa wanajaribu kuyauza kwa kasi ili kila Mtanzania anayeishi mjini ajipatie jenereta lake kazi iendelee..Watu wote kwenye kibasi tukacheka.
 
Kwani amewahi kuongoza wizara ngapi?
  • Sayansi na teknolojia alikuwa naibu waziri (hakuwa na mamlaka ya uamuzi)
  • mazingira alikuwa waziri katika ofisi ya makamu wa rais (hakuwa na mamlaka kamili ya uamuzi)
..... nyingine?
I think hapa Nishati ndio true test tumjue yeye ni nani
Akifaulu uRais anao
Akifeli amekwisha

Mungu amtangulie..
 
Zito anawapenda sana Kikwete na Makamba.

Yuko tayari kutetea kila aina ya ujinga na kujitoa fahamu..

Kwa nini wasikubali tu kwamba wameshindwa kuvaa viatu vya Magufuli?
Mbona Samia amekubali hadharani na hamna aliyemshangaa
 
Back
Top Bottom