Kimeumana: Mo ameanza kudai Hadi pesa zilizonunua mchicha, ndala na boxer za wachezaji

Kimeumana: Mo ameanza kudai Hadi pesa zilizonunua mchicha, ndala na boxer za wachezaji

Yote kwa yote huyo CPA Issa Masoud mjumbe wa Bodi alikuwa wapi miaka yote mitatu wakati Simba inaharibikiwa mdogo mdogo mpaka mwaka huu imeingia ICU? Huyo na wajumbe wenzake wote wa bodi ni wa kufukuza kwani wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa wakati. Walipaswa kurekebisha mambo mapema sio sasa hivi wanakuja hadharani kulalamika kama watu wa kawaida wakati wao walikuwa kwenye chombo cha maamuzi. Ni unafiki wa hali ya juu na kutafuta tu huruma kwa umma baada ya kuona mambo yanaenda kuwaharibikia na wao.
Ndo hivyo Kila mtu hataki kuonekana mkorofi
 
Huu utapeli ndio alikuwa anaufanya Manji Yanga, kila siku utasikia yeye ndio anaidai timu.

Fukuza Wahindi wote weka Waarabu hawanaga longolongo kwenye maswala ya pesa.
Kwa MANJI sio kweli
Namna klab ilivyokuw anaiendesha MANJI huwezi fananisha na MO aliyokuwa anaiendesha SIMBA hoiya kisasa baada kutangaza kuinunua

MANJI hakuwahi kuinunua YANGA ama kutaka kuinunua na FEDHA alizokuwa anatoa alikuwa anatoa kwa MAPENZI yake pale TIMU inapokwama

Timu zamani zilikuwa zinaendeshea kwa. UFADHILI sio UDHAMINI
Mdhamini wa kwanza wa YANGA ni QUALITY GROUP lakini nae alikuwa MDHANINI lakini kwa namna Nyingine MFADHILI kwa maana katika huo UDHAMINI hakukuwa na faida yoyote isipokuwa walitaka tu kuiendesha TIMU kisasa

MANJI hakuwa na ujanjaujanja FEDHA za ufadhili alizokuwa anatoa zilionekana na watu tuliona namna gani anafanya UFADHILI
lakini jambo kubwa alikuwa anaelewana vizuri na viongozi wa klabu na wazee wa klab ingawa walikuwa wanamchimba wazeee lakini akitoa FEDHA wananyamaza na kwamwe hakuisakama KLABU kisa anatoa pesa

Manji ndo MFADHILI pekee alikuwa anatoa pesa yake kumnunua mchezaji anayemtaka na wala asilalamike timu ikifanya vibaya au kulialia kuwa anapata hasara na kuanza kupiga hesabu ya oesa alizotoa
Yanga ikifanya vizuri alikuwepo kwa moto uleule
Yanga ikifanya vibaya alikuwepo kwa moto uleule
Na hata kuondoka kwake YANGA wote tuliona 7bu ya misukosuko yake na SERIKALI
Na ndo mana mpk kesho MANJI yupo kwenye mioyo ya WANAYANGA

Hayo machache ila kuna mengi zaidi na zaidi

Hvyo kumfananisha na MO mfanyabiashara ama kwa kumuita tapeli MANJI basi wewe utakuwa hauifahamu YANGA vizuri na si mfuatiliaji wa SOKA la TANZANIA
 
Ivi timu Ina miaka zaidi ya 80 inashindwq kujiendesha mpaka itegemee MTU mmoja

Imeshindwa kuwa na vitega uchumi vyake mpaka Leo

Mo Kama ana hela si angeanzisha timu yake angalau tuwe timu zenye ushindani kuliko ujanja ujanja anaufanya hapo

Wabongo nini ni tunaweza Sasa

Mashabiki na matangazo tu yangewekewa utaratibu mzuri timu ingeingiza mapato ya kutosha

Hizi akili zetu zikoje ,
Taasisi Ina miaka 80 inategemea MTU mmoja ambaye ana umri mdogo kuliko hata taasisi
Naona ni upuuzi kabisa
Wanachama wa Simba hawana maamuzi yoyote ndani timu

au nao ndo hawachangii hata Kadi wanasubiri Mo awalipie !! kelele tu

Sijui niite ni undondocha au ni nini ???
Alianzisha African Lion [emoji881] ikamshinda muhimdi kanjanja[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom