Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Hawa jamaa wanafanana na story moja ambayo mtu mmoja aliweka tangazo kwenye TV iliyokuwa inaangaliwa na watu wengi, tangazo hilo lilieleza kuwa ukiweka dollar moja kwenye account yake na ukaweka na email yako atakuelezea siri ya utajiri. Kwa sababu watu waliona dollar moja ni ndogo waliweka wengi Sana baada ya muda mfupi watu zaidi ya million 50 waliweka ambayo sawa na dollar million 50. Watu walipomubana aseme siri ya utajiri aliwaambia nitaingaza kwenye TV siku ilipofika akatangaza kuwa siri ya utajiri ni kutumia akili yako kupata utajiri si nguvu, maana Mimi nimetumia akili nimekuwa millionaire kwa kuchagiwa dollar moja moja. Sawa na hawa jamaa zetu wa vanilla
 
Kwahio wananunua ?
Basi kama kweli wananunua kwa bei husika huu mjadala nadhani hauna maana (The Proof is in the Pudding) Ila kama wanakataa kununua mzigo uliopo hapa naweka Question Marks Sita na Exlamation Marks Saba
 
Umesahau kitu kimoja,, katika kila uwekezaji kuna risk zake hivo hamna sehem ambayo utawekeza usipate challenge
 
Wewe ni mgeni labda vanilla inalipa Ina pesa ndefu hata kabla ya ujio wa hamasa hii.
Uliza kagera.
Madagascar mashamba ya vanilla yanalindwa na bunduki ndo ujue pesa ipo.
Ilikuwa ni jukumu la serikali kuwaunganisha wakulima na masoko.

Kagera walinzi wanaogopa hio kazi maana wezi wanawaua sana ili waibe vanilla..
Kuna professor mmoja kafunga mataa kila kona na cctv camera za kutosha.. usiku kama mchana
 
Kinadharia YES ingawa siyo rahisi kama unavyo iweka kwa mabenki kutoa pesa namna hiyo! Hakuna taasisi zisizo taka risks kama banks, ndiyo maana Serikali yetu "ikajiripua" kwa kuanzisha TADB ili ichukue at least some risks kwenye kilimo ingawa nao hajiripui kihivyo au hovyo hovyo. Hebu tafuta uzi wa Viking wa 02/08/2020 wenye kusomeka "Profesa Kabudi Nenda Madagascar Ukatuletee Miche ya Vanill". Naamini utapata kitu humo.
 
Kwahio wananunua ?
Basi kama kweli wananunua kwa bei husika huu mjadala nadhani hauna maana (The Proof is in the Pudding) Ila kama wanakataa kununua mzigo uliopo hapa naweka Question Marks Sita na Exlamation Marks Saba
Hawanunui kwa watu baki mkuu , wenyewe wanalima ya kwao kwa viwango wanavyotaka wenyewe ..maana mfano walisema mbolea wanayotumia wenyewe huagiza kutoka BARCELONA nchini Hispania hivo unaweza kuona jinsi wanavyohangaika ku maintain standard ya kimataifa ,...pia sio VANILLA TU, WANAJISHUGULISHA NA ULIMAJI PIA WA VITUNGUU NA PARACHICHI ,. Vivyohivyo ukija na VITUNGUU vyako hawanunui
 
Hii kitu ikiruhusiwa na ukawekwa mfumo rahisi wa kuipeleka kwenye masoko ya nje Ulaya na Marekani naacha kila nachofanya naingia kwenye hiki kilimo !
Cannabis vipi!? Unataka ruhusa kutoka kwa nani, mbona hujaomba ruhusa kulima mahindi au kahawa!? Wewe lima, tafuta soko na peleka! Kama huna ujuzi wa kupeleka nje mazao, nenda kwenye taasisi husika za kiserikali wakuelekeze. Wenzako wanalima huko Kagera na kupeleka nje!
 
Hii kweli ni Story.... (Fiction Lakini)
 
Huyo KeyserSoze nilisha mueleza hayo yote, asante kwa kuliweka KIURAHISI labda ataelewa! Wao wana oda maalum kwa viwango maalum na kwa packing maalum na kwa masharti maalum kama yalivyo yale ya AGOA! Kwani ni kwa nini watu wameshindwa kupenyeza kwenye soko la AGOA!? Ni hayo masharti tu.
 
WATANZANIA WANAPENDA SANA MTEREMKO
UKITAKA KULIMA INGIA MWENYEWE SHAMBANI AU MUWEKE MTU UNAYE MJUA AKUSIMAMIE
UKITAKA FUGA KUKU DO THE SAME WAY!
SASA UTAKUTA WATU INAFANYA KAZI MAOFISINI WAO WAKIPELEKWE KWENYE
MAWORKSHOP WAKIWEKEWA MAPROJECTOR
NA WAKIONESHWA MAGRAPH SJUI WATAPIGA MAMILION MANGAPI WANACHANGANYIKIWA
KITU CHOCHOTE LAZIMA UKITOLEE JASHO
LAZIMA UINGIE FIELD

ova
 
Haa Teh
Tena Avacado Wanawadanganya Utamu
Ukilima Hizi Unauza Ulaya Wao Wanawapiga Tu
Kwa kusoma hii post yako na ya Bondpost, naamini sasa kuna uelewa mdogo juu ya kilimo hiki cha vanilla na hicho cha Parachichi au Avocado. Ni ukweli kuwa hayo mazao pia yanalimwa Njombe na ya soko kubwa sana Ulaya, in fact Avocado ya Njombe, karibu yote, inanuliwa na walanguzi kutoka Kenye. Wao wana REPCK na kulabel upya na kusema inatoka Kenya na kuuza kwa bei ya juu sana.

Wakenya wana ready market ambayo mkulima wa Njombe halijui wala hawezi kulitafuta. Ikifika wakati wakiibuka watu kama akina Vanilla International na ku - mobilize watu wawekeze kwenye zao hilo na kuwalipa mahela mazuri zaidi ya Wakenya na kwa utaratibu wao wa sasa, wataibuka wana JF nakupiga kelele UDECI au UTAPELI. Hili linawezekana na ni suala la kukamata fursa ya Economies of Scale kwenye eneo hilo na kusonga mbele.
Haa Teh
Tena Avacado Wanawadanganya Utamu
Ukilima Hizi Unauza Ulaya Wao Wanawapiga Tu
 
Mkuu; Nime-quote kwa waliokuwa wanashabikia huo mradi. Lakini ki-ukweli zao hilo linalimwa Hai na bei yake ni Tshs. 20,000/= kwa kilo. Ipo taarifa hiyo humu jamvini jaribu kuifuatilia - Pole sana kama nimekukwaza bro.
 
Binafsi nilimpigia huyo jamaa wa Vanila international nikamwambia kuwa nina tani moja ya vanila nimpeleekee .

Akanijibu kuwa kwa sasa hashughulikii na ununuzi na hawajaanza kununua ndiyo nikajua kuwa ni matapeli.
Bei ya juu niliyowahi kuisikia miaka ya 2010 ilikuwa sh. 40,000. Ni mkoa wa Kagera, mnunuzi wao mkuu alikuwa Uganda. Sasa wameibuka matapeli hawa, tena wajinga kabisa wanaumiza watu baadaye wavune na kujiondokea.

Matangazo ya aina hii hayana tofauti na DECI iliyoumiza watu. Angalia baada ya kuwaelekeza wa-TZ kwenye korosho; pwani hadi Singida, wengine wakaelekea kwenye palachichi, Haijafika mwisho sasa imekuja vanilla na matangazo ya TV. Bahati mbaya wengi wanaiamini TV na ndo maana hata Tatu mzuka na Biko wanajitangaza utadhani ni watu wa maana. Wananchi wanaumizwa serikali iko kimyaaa! Mkuu wa mkoa wa Njombe anastahili sifa kwa kuliona hili.
 
Vanilla ni SAwa na opium ya mexico inalindwa na bunduki.
Nilipanga kulima vanilla hata kabla ya promotion.Ila shughuli yake sio rahisi heka 1 moja tu we umasikini kwaheri ila shughuli pevu.
Mziki wake upo kwenye kuchavusha "pollination" acha kabisa hili zao!
 
Kwenye TV huwa ni picha zile zile mwaka umekatika shida ni kamera au nini? Swali la pili hizo green house ambazo mche wa vanilla unatambalia kwenye ka-ubao kembambaa ni demo au really? Maswali mengine yanakuja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…