Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
Kwa maelezo yako hapa sijaona huo utapeli, acha wivu wacha jamaa apige hela kwa akili zake.Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe
šSerikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.
Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.
šKazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.
Kama vipi na wewe kaanzishe kwenye zao la Magimbi.