Kina dada jifunzeni hapa, usimdharau mwanaume asiye na kitu huwezi jua kesho yake

Kina dada jifunzeni hapa, usimdharau mwanaume asiye na kitu huwezi jua kesho yake

Nini maana ya ndoa au ni nini sababu za watu kufunga ndoa?

Sina hakika kama lengo la ndoa ni kupata "utajiri". Mtu anayeingia kwenye ndoa kwa lengo la kuwa tajiri, awe mwanamke au mwanaume, mtu huyo atakuwa ameingia kwenye ndoa kwa sababu zisizo sahihi.

Mtu huyo atakuwa at the wrong place, at the wrong time and for the wrong reasons! Ndoa hiyo haitadumu.

Ndoa ina maana kubwa sana. Moja ya sababu za kufunga ndoa ni kuendeleza uzao duniani huku kila mmoja akimtimizia mwenzake "mahitaji ya kimwili" ambayo hayaepukiki kirahisi. Kila jinsia inahitaji mwenza kwa ajili ya kutimiza hitaji hili muhimu la "kimwili".

Uwe tajiri au uwe maskini, hitaji la kimwili lipo pale pale.

Kutajirika mkiwa ndani ya ndoa hiyo ni bonus tu katika maisha. Siyo wote wanaotajirika wanaishi maisha ya raha ndani ya ndoa zao. Na pia, siyo wote walio maskini wanaishi maisha ya huzuni ndani ya ndoa zao.

Tukielewa maana halisi ya ndoa ni nini, pesa ni matokeo tu, zikiwepo au zisipokuwepo siyo kigezo cha sisi kuwa na furaha au kukosa furaha na wenza wetu.
 
Back
Top Bottom