Kina dada wa JF tumechoka malalamiko yenu, tunaomba ufafanuzi wa hii hoja

Kina dada wa JF tumechoka malalamiko yenu, tunaomba ufafanuzi wa hii hoja

🤣🤣🤣 Daby

Unanitamanisha nijaribu hayo ya kufaidi maisha ya kutongozwa na videti tena.

Kwa jinsi nilivyokua na kujua kusaka pesa yangu.. eeeh

Ningefungua uwanja wa kufatiliwa na kutoa nafasi

Mimi kwanza ningependa mwanaume aje na story za current news na za teknolojia miaka hii ya kijiditali.. hapo anakuwa anajua list ya top 5 or 10 ya bidhaaa fulani fulani.. mimi nachagua tu kama tatu tuuu KUANZIA..

Na mimi nimwambie hiki na kile.. halafu akiweka interest kuuliza nataka zawadi gani

Eeeeeeh..
Hahahahaaa. shikamoo Coco. Nimechukua ujuzi
 
Yiiiih. Story yangu jamani. MTU kaniambia karibu lunch nikamwambia asante. Muda huo huo akatuma na message naomba Namba ya Wakala nikutumie kidogo ya lunch. Wanaume kawa Hawa waishi milele JF
Yaani wabarikiwe mno, mno.
Na wanaume hawa huwa wapo kimya muda wote.
Akina pangu pakavu tia mchuzi sasa....fujo kila majukwaa.
Khaaa!!!!
 
Kwahiyo wanaoweka maneno matamu katika post zao na mbwembwe nyingi ndio hawana mvuto and vicevesa is true?

Kwahiyo ili umjue mtu ni mrembo inabid asiweke maneno matamu kwenye post zake.

Acha uzushi jamaa humu hakuna anayemjua mwenzie kama hamjawah kukutana. Unaweza ona kama mwanamke anapost maneno ya kimcharuko kumbe ni dume mwenzio.

Hata wanaume pia mpo nyuma ya keyboard na wapo wanaojisifu kwa kila hali na wao unawazungumziaje? Usipende kujudge tabia ya mtu usiyemjua kwa maandishi utakuja kutongoza na kuhonga wanaume mwenzio.
Na ndio maana hawataki kukutana nao sababu utaendaje kukutana na dume mwenzio hali anajua wewe ni ke tena mrembo
 
Lalamiko la wadada lina mantiki kubwa na ni vyema wanaume mkalifanyia kazi. Daby huwezi kumfuata mdada PM from no where eti kwa kuvutiwa tu na avatar au umesikia watu wakidanganyana kuwa yuko hivi na vile.

Kabla ya kumfuata PM msome ili ujue interest zake, then unapomfuata PM anza kuchomekea maneno yanayolandana na interest zake. Hii ni kwasababu binadamu tunatofautiana. Lakini sasa ikiwa utakuwa unagawa tu dozi ya salamu kutwa mbili mara tatu kama panadol inabore!
Tawileee
 
Watu mna maneno ,eti ukifika kwa mfano kwenye pm ya mzigua90 moja kwa moja uanze kumwaga factors for soil formation[emoji1]
Hahahahahaaa. Eeeh. mimi napenda kujifunza ukinikumbusha hayo mavitu nitakua interested kuwasiliana na wewe. Lakini mambo asubuhi mpaka asubuhi hapana. Sema wanaume wajanja wanajua Ndo maana wanajibiwa mpaka Mwisho wa maongezi
 
Mie kuna mwanaume mmoja alinitumia picha Pm.
Mpaka nikahisi ni mbilikimo wa Congo.
Afu jukwaani anavyoponda wanawake sasa...chefuuuuu!!!

Namtazama tu.
Kutwa anajishaua shaua kama nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa.
Ila ni mbovu wa sura mpaka umbo.
Yaani nahisi anaishi huko Tandale/Manzese ndani ndani ila akiwa jukwaani, anaishi Masaki.

Namsubiria siku aingie cha kike
Hahahahahaaa. Yani unanichekeshaa
 
Back
Top Bottom