Kina Mangi njooni tubadilishane uzoefu. Tushirikiane.

Wakati huo huo kuna mtu hiyo elf 70 anaipata kwa mteja mmoja tu. Location muhimu sana
Umeongea point Mimi eneo nilipo hapa mauzo ya juu kabisa kwa siku ni 70 na chini kabisa 30 kwahyo hii biashara inategemeana na location ulipo
 
Hilo la Imani na mambo ya kishirikina litakuangusha usipokuwa makini. Nasema hivi kwa sababu kwenye biashara HAKUNA ushirikina. Huduma yako nzuri kwa wateja ndiyo ushirikina. Kwa uchunguzi wangu ni kuwa maduka mengi Bongo customer care zao ni majanga. Hili la ubovu wa customer care ni jambo common kiasi cha ku weza kuliandikia kitabu kikubwa kama biblia. Baadhi ya tabia mambo mabovu:
1. Dukani kwa nje kukaa watu (hasa vijana) wasio na kazi na kuangalia/kusikiliza kwa udadisi kila anayekuja dukani
2. Wenye maduka kuhudumia wateja huku wanafanya shughuli nyingine kama kuzungumza na simu etc
3. Kauli chafu za wauzaji
4. Kutokuandaa chenji za kutosha hivyo kulazimika kurudisha baadhi ya wateja au kuwachelesha.
5. Kuhudumia kwa dharau wateja wanaonunua mali za bei ndogo
6. Kuuza vitu vyenye hitilafu kwa ujanja ujanja au kurudisha chenji za noti mbovu bila kujali kuwa mteja asiporidhika leo kesho harudi tena
7. Wenye duka wanaume kutongoza wasichana wanaokwenda dukani eg ma-house girls
8. Kutoa majibu ya mkato na kukasirika wanapokutana na mteja msumbufu
9.
10.
11. Kuna mengi sana unatakiwa uzingatia.
 
Tunazidi kupata somo mkuu, natumaini na wengine wataongeza mengine
 
Ni kiduka kidogo. Na sio frem bali kibanda cha chuma. Majirani zangu nafikiri wanalaza zaidi ya 500K kutokana na kuwa na wateja wengi sana sababu wamekaa miaka mingi sana hapa.
Issue ya kuuza high or low inategemea na ile actual population unayoitegemea kwa atleast kila siku pamoja na location
 
Umeongea point Mimi eneo nilipo hapa mauzo ya juu kabisa kwa siku ni 70 na chini kabisa 30 kwahyo hii biashara inategemeana na location ulipo
Hatutofautiani sana mimi frame niliopo zipo tatu ya kwanza duka la dawa ya pili duka la mabitaji ya nyumbani na latatu lakwangu mahitaji ya nyumbani bado eneo hili hili lina frame zakutosha yani mzunguko ni mdogo hapa inahitajika ubunifu wa hali ya juu nategemea kupitia huu uzi kuna vitu na ubunifu naeza pata, aksante.
 
usidanganyike na uwing wa mauzo mkuu..viduka vya mtaani nadra sana mtu kununua sukari 5kgs ..ni nusu na robo..!inahitaji wito sana hii biashara
Duka ukiweka mtaani itachukua miaka mingi sana kuwa na maendeleo au litabaki vilevile miaka yote. Ndo maana ishu ya location ni muhimu, biashara ya namna hii inatakiwa sehemu ambayo iko busy kidogo
 
Duka ukiweka mtaani itachukua miaka mingi sana kuwa na maendeleo au litabaki vilevile miaka yote. Ndo maana ishu ya location ni muhimu, biashara ya namna hii inatakiwa sehemu ambayo iko busy kidogo


Hyo 500k naamini ninsokoni mzee baba sio kitaa..au ni mjini..ila sio maduka ya kina mangi aisee ya mtaani
 
Ila mkuu unatakiwa uwe nadaftari la mauzo ambalo unaregister vitu ulivyonunua idadi, bei ya kununulia na faida atleast siku unaeza kaa ukafanya tathmini,
Kwamfano ulinunua catton ya sabuni faida 15k ukiona catton imeisha kama kuna uadilifu unauza duka peke yako jua kwenye mzunguko pameongezeka 15k likewise kwa bidhaa nyingine, so hii itakusaidia kufanya tathmini ambayo itakuzuia usitumie kuliko una hoingiza
 


hii mm hata bure siirudii..eti uweke kwa sk 20 haipo hyo..jua.utafeli tu kuleta mzigo...yaan ukikaza sana uweke 10 per day..! mie naijua ndan nje..! ht nipewe 10m siifanyi ng'o..jiashue unaumwa uchukue 30 UMEKWISHAA😂😂😂
 
Hyo 500k naamini ninsokoni mzee baba sio kitaa..au ni mjini..ila sio maduka ya kina mangi aisee ya mtaani
Ndo maana kuna sehemu hapo juu nilitaja mfano wa sehemu ambazo zipo vituoni kama Mbezi, Kimara Korogwe, etc.
 
Ni kweli mkuu. Tathimini muhimu sana, nilijaribu kuandika badae nikashindwa.... Uvivu. Ila nitaanza tena.
Nilichofanya niliandika kila nilichokuwa nauza kila siku kwa sku 3 then nikaculculate faida nlopata kwa kila nlichouza, mwisho wa sku nikapata total faida, nikajua faida ya kila sku kwa makadilio. Ndo nikaja na maamuzi ya kuwa nasev hicho kiasi.
 
Hiyo biashara ukiipata unitag
 
Nipe namba yako ya watsap dm nikuoneshe namna ninavyo track mauzo japo biashara yangu ndogo na location haijakaa poa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…