Kina Mangi njooni tubadilishane uzoefu. Tushirikiane.

Hilo la Imani na mambo ya kishirikina litakuangusha usipokuwa makini. Nasema hivi kwa sababu kwenye biashara HAKUNA ushirikina. Huduma yako nzuri kwa wateja ndiyo ushirikina. Kwa uchunguzi wangu ni kuwa maduka mengi Bongo customer care zao ni majanga. Hili la ubovu wa customer care ni jambo common kiasi cha ku weza kuliandikia kitabu kikubwa kama biblia. Baadhi ya tabia mambo mabovu:
1. Dukani kwa nje kukaa watu (hasa vijana) wasio na kazi na kuangalia/kusikiliza kwa udadisi kila anayekuja dukani
2. Wenye maduka kuhudumia wateja huku wanafanya shughuli nyingine kama kuzungumza na simu etc
3. Kauli chafu za wauzaji
4. Kutokuandaa chenji za kutosha hivyo kulazimika kurudisha baadhi ya wateja au kuwachelesha.
5. Kuhudumia kwa dharau wateja wanaonunua mali za bei ndogo
6. Kuuza vitu vyenye hitilafu kwa ujanja ujanja au kurudisha chenji za noti mbovu bila kujali kuwa mteja asiporidhika leo kesho harudi tena
7. Wenye duka wanaume kutongoza wasichana wanaokwenda dukani eg ma-house girls
8. Kutoa majibu ya mkato na kukasirika wanapokutana na mteja msumbufu
9.
10.
11. Kuna mengi sana unatakiwa uzingatia.
Aisee umegusa penyewe, kwenye biashara yoyote ile ni kinachowaangusha watu ni detail ndogo ndogo sana ambazo wanazipuuza, Wahindi na Waarabu wamefanikiwa sana sababu ya attention to details, discipline
Waafrika wote tungeukuwa makini hivi tungekua mbali sana
 
Biashara yako ukichomoa laki 1 ikayumba ujue haijakomaa hiyo, bado inahitaji kulelewa.
 
Hilo la Imani na mambo ya kishirikina litakuangusha usipokuwa makini. Nasema hivi kwa sababu kwenye biashara HAKUNA ushirikina. Huduma yako nzuri kwa wateja ndiyo ushirikina. Kwa uchunguzi wangu ni kuwa maduka mengi Bongo customer care zao ni majanga. Hili la ubovu wa customer care ni jambo common kiasi cha ku weza kuliandikia kitabu kikubwa kama biblia. Baadhi ya tabia mambo mabovu:
1. Dukani kwa nje kukaa watu (hasa vijana) wasio na kazi na kuangalia/kusikiliza kwa udadisi kila anayekuja dukani
2. Wenye maduka kuhudumia wateja huku wanafanya shughuli nyingine kama kuzungumza na simu etc
3. Kauli chafu za wauzaji
4. Kutokuandaa chenji za kutosha hivyo kulazimika kurudisha baadhi ya wateja au kuwachelesha.
5. Kuhudumia kwa dharau wateja wanaonunua mali za bei ndogo
6. Kuuza vitu vyenye hitilafu kwa ujanja ujanja au kurudisha chenji za noti mbovu bila kujali kuwa mteja asiporidhika leo kesho harudi tena
7. Wenye duka wanaume kutongoza wasichana wanaokwenda dukani eg ma-house girls
8. Kutoa majibu ya mkato na kukasirika wanapokutana na mteja msumbufu
9.
10.
11. Kuna mengi sana unatakiwa uzingatia.
Hiyo ya kwanza inakwaza sana. unakuta umefata kitu cha aibu kununua kama kondomu au pedi hlf mijamaa imejazana hapo shop inapiga stori na muuza. nageuza zangu tu chap nasepa.
 
Habari wadau,
Wale wenye maduka ya bidhaa za rejareja (mangi) tukutane hapa tubadilishane mawazo kidogo, tujadili ili kila mmoja aiweke biashara yake kwenyw kipimo kwa kulinganisha na wengine ili tuweze kuboresha zaidi.

Binafsi sina duka ila nna kijiduka au kibanda nilichokianza baada ya kupoteza kazi yangu niliyokuwa nayo mwanzo,

Wakuu mi nitagusia mambo yafuatayo;

1. Mauzo.
Hapa tujue mauzo ya kawaida kwa siku.
Mimi binafsi siku hazilingani, siku za j3 na j4 mauzo hushuka sana na kufikia angalau 120K kwa siku. Siku zingine hupanda kidogo mpaka kwenye 170, 150,... Siku za jmos na jpili mauzo hufika laki mbili au zaidi kidogo kwa siku.

2. Ushindani.
Hapa wakuu tushee picha halisi ya mazingira tunayofanyia biashara, na unakabiriana vipi na changamoto ya ushindani.
Binafsi mi nilipo nilikuta maduka mawili, mimi nikawa wa tatu. Mmoja wetu ana duka na genge, hivyo wateja wengi hupenda kwenda pale kwa sababu wanapata huduma zote kwa pamoja. Mi niliona nifanye tofaut, nikamix bidhaa za kawaida na nyingne kama baadhi ya vifaa vya umeme (taa, holder,..) Makufuli, etc.. maana niliona huduma hizi hakuna hapa mtaani, imenisaidia kufanya nizoeleke maana wateja wengine huja kufata vitu hivyo baada ya kuvikosa kwa hawa wenyeji.

3. Imani.
Wengi uhuhusisha hizi biashara na imani za kishirikina, na huenda sana kwa waganga kutafuta kitu kinachoitwa mvuto au king'amuzi.
Binafsi naamini hayo mambo yapo na watu wanachangamsha sana biashara zao kupitia mambo haya. Lakini mimi sijawahi kujihusisha na sina mpango sababu mambo haya huchukua hela nyingi na ukishayaanza ni ngumu kuacha. Vile vile mwisho wake mara nyingi sio mzuri.
Je nyie wadau mnalichukuliaje suala hili? Je wewe huwa unaenda?

4. Faida. Je hii biashara ina faida? Na ni kiasi gani? Unaijuaje au unaiona kwa namna gani hiyo faida?

Binafsi huwa sicomplicate, kila siku nachukua elf 20 naweka akiba. Haijalishi nimeuza kiasi gani.
Chakula cha kupika kinatoka dukani pamoja na mahitaji mengine, (hiyo yote ni faida). Lakini ninatoa kwa umakini sana. Na biashara yangu haijawahi kurudi nyuma, zaidi naongeza bidhaa mpya na kupanua kidogo kidogo.

Nawakaribisha wote wenye biashara ya namna hii tujadili, tubadilishane uzoefu, tufundishane, tufunguane, tunaeza pia kugusia na mengine zaidi kama namna ya kununua bidhaa, sehemu za kununua na mengine mengi.

Karibuni.
Natumaini neno "Mangi" ni wafanya biashara na siyo swala la ukabila?!
Tumeipenda thread yako tatizo ni hilo la "Umangi"...
 
Mkuu hujajibu ni kwa namna gani unapambana na mikopo/wakopaji?
Mkuu mi sikopeshi. Sina maana kuwa sikopeshi kabisa. Nina mama ntilie watatu tu ndo wanachukua vitu asubuhi na mchana then wanalipa jioni. Nina watu kama wanne nawakopesha ila huwa hawalazi hela yangu zaidi ya siku mbili.
Mtu akija kukopa hata kama ni mteja wangu huwa nampa maelezo mazuri ya uongo, ninamwambia nina mzigo wa tajiri na leo anatakiwa kuchukua hela yake lakin bado haijatimia.
Au namwambia biashara nafanya kwa mkopo hivyo narejesha kila sku.
Au namueleza kwa sasa hali ni ngumu sana na nina watu wengi sana naowadai kwahiyo kwa sasa nimesitisha kidogo kukopesha ili nisijekurudi nyuma.

Yaani mtu unampa maneno ambayo yatamuonesha hujamnyima. Ajue ulikuwa na nia ya kumpa lakini bahat mbaya mambo yako sio mazuri. Ili aendelee kununua kwako.

Kuna mtu mwingine anakuwa sio mteja wako kabisa, ila akitaka kukopa ndo anakuja kwako, huyo unamchana live kuwa huwa sikopeshi.

Na kwakweli hapa nilipo sijafikisha hata miaka miwili, hivyo watu wengi hawajanizoea kivile kiasi cha kunikopa hovyo hovyo.

Ukishaona madhara ya mikopo huwezi kuiendekeza. Maana tabia ya wengi ni kuwa mtu akishakukopa hata kama ni 1000 anahama duka, humuoni tena hata njia anabadilisha.

Kama upo kwenye location nzuri ukaepuka mikopo, matumizi mabaya ya pesa, na kuzingatia manunuzi yaani kununua bidhaa zako penye unafuu mbona biashara inalipa. Mfanyabiashara hupaswi kukalili duka moja la kununulia bidhaa, utashangaa unauziwa mafuta elf 52 kumbe yalishafika 49. Unatakiwa kuwa mtafiti wa bei. Nenda Manzese, nenda K. Koo nenda River side, nenda Kimara, nenda Tandale.

Mi mzee wangu ana maduka mawili ya reja reja, hana kazi nyingine lakini kanunua assets za kutosha kupitia biashara, ana maviwanja, majumba, magari. Katusomesha pia. Na mifano ya watu wa namna hiyo wapo wengi tu.
Na mimi najiona huko miaka ijayo Mungu akipenda.

Wanaoponda biashara hii jua waliifanya kwa kujaribu tu hawakuwa serious au ni watu wenye tamaa ya mafanikio ya haraka. Jamani hii biashara usifanye ukajua utafanikiwa ndani ya mwaka mmoja.
Mimi hapa nilipo nimefungua mara ya tatu. Nilifungua sehemu ya kwanza mauzo yakawa chini nikashindwa kulipa kodi nikafunga, nikaenda sehemu nyingine zikatokea changamoto kubwa sana nikafunga, nikaenda sehemu nyingine hapa nilipo kwakweli Alhamdulillah. Kama umeamua kufanya usifel mara moja ukaacha, jaribu jaribu jaribu na tena.

Pia kumbuka biashara nzuri ni ile unayoianza na mtaji kiduchu ukaikuza taratibu. Biashara ya kuanza na mtaji mkubwa au biashara ya kufunguliwa na mtu ni mara chache sana hudumu.
Wewe binafsi epuka kufanya biashara yako kwa mikopo. Tumia hela yako \ mtaji wako binafsi hata kama ni mdogo.

Angalizo; Ukimuajiri mtu dukani usitarajie maendeleo.
 
Natumaini neno "Mangi" ni wafanya biashara na siyo swala la ukabila?!
Tumeipenda thread yako tatizo ni hilo la "Umangi"...
Mkuu hili umekuja na jipya ambalo halikuwa kichwani kwangu. Au una lengo la kubadili mwelekeo wa thred
 
Hapo kwenye imani umeongea ukweli, mtaani kuna jamaa mmoja alianza biashara taratibu sana kwa mtaji mdogo baadae akapanuka kidogo.... Baadae biashara iliinuka ghafla mpaka duka likawa dogo ikashindikana kuhudumia wateja mwenyewe

Wakawa watatu tena hapo ni baada ya kumuhamisha jirani yake na kuunganisha zikawa frem mbili.... Biashara iliendelea kuumuka mpaka akaifikia frem ya 3 na yenyewe akamuamisha mtu

Biashara ilichanganyia mpaka gari la TBL likiwa likija linamalizia mzigo hapo.... Gari ya sigara ilikua inakuja na security na bunduki... Hawa Coca-Cola na Pepsi walikuwa wanamgombania..

Alikua anavamiwa mpaka na majambazi wenye bastola wanaiba pesa kwenye maboksi lakini bado jamaa yupo tu kwenye chat.... Dah jamaa alikua anauza jumla tu sababu rejareja ilikuwa kama ni kujidharaulisha au kupoteza muda

Ila alivyoanza kuporomoka mpaka utamuonea huruma, me sipendi kabisa kumuona mtu anaanguka lakini nikimuona yule jamaa huwa hata machozi yananilengalenga sababu ni mtu ninaomfahamu toka nikiwa kinda kabisa tunatumwa mahitaji dukani kwake

Ni kwamba yule jamaa saivi ni dereva kirikuu anapaki tu mahali anasubiri wateja nikimuona huwa nakuwa mdogo sana kama piriton na ninajua mtu kushuka ni time yoyote, mtu ambae alikua anafunga hesabu za mamilioni kwa siku saivi anazikimbiza elfu 10 10

Yanaongelewa mengi kuhusu jamaa ila kubwa ni hilo la imani za...
 
Asante kwa mfano hai. Ndumba mwisho wake sio mzuri mara nyingi.
 
Mkuu mi sikopeshi. Sina maana kuwa sikopeshi kabisa. Nina mama ntilie watatu tu ndo wanachukua vitu asubuhi na mchana then wanalipa jioni. Nina watu kama wanne nawakopesha ila huwa hawalazi hela yangu zaidi ya siku mbili.
Mtu akija kukopa hata kama ni mteja wangu huwa nampa maelezo mazuri ya uongo, ninamwambia nina mzigo wa tajiri na leo anatakiwa kuchukua hela yake lakin bado haijatimia.
Au namwambia biashara nafanya kwa mkopo hivyo narejesha kila sku.
Au namueleza kwa sasa hali ni ngumu sana na nina watu wengi sana naowadai kwahiyo kwa sasa nimesitisha kidogo kukopesha ili nisijekurudi nyuma.

Yaani mtu unampa maneno ambayo yatamuonesha hujamnyima. Ajue ulikuwa na nia ya kumpa lakini bahat mbaya mambo yako sio mazuri. Ili aendelee kununua kwako.

Kuna mtu mwingine anakuwa sio mteja wako kabisa, ila akitaka kukopa ndo anakuja kwako, huyo unamchana live kuwa huwa sikopeshi.

Na kwakweli hapa nilipo sijafikisha hata miaka miwili, hivyo watu wengi hawajanizoea kivile kiasi cha kunikopa hovyo hovyo.

Ukishaona madhara ya mikopo huwezi kuiendekeza. Maana tabia ya wengi ni kuwa mtu akishakukopa hata kama ni 1000 anahama duka, humuoni tena hata njia anabadilisha.

Kama upo kwenye location nzuri ukaepuka mikopo, matumizi mabaya ya pesa, na kuzingatia manunuzi yaani kununua bidhaa zako penye unafuu mbona biashara inalipa. Mfanyabiashara hupaswi kukalili duka moja la kununulia bidhaa, utashangaa unauziwa mafuta elf 52 kumbe yalishafika 49. Unatakiwa kuwa mtafiti wa bei. Nenda Manzese, nenda K. Koo nenda River side, nenda Kimara, nenda Tandale.

Mi mzee wangu ana maduka mawili ya reja reja, hana kazi nyingine lakini kanunua assets za kutosha kupitia biashara, ana maviwanja, majumba, magari. Katusomesha pia. Na mifano ya watu wa namna hiyo wapo wengi tu.
Na mimi najiona huko miaka ijayo Mungu akipenda.

Wanaoponda biashara hii jua waliifanya kwa kujaribu tu hawakuwa serious au ni watu wenye tamaa ya mafanikio ya haraka. Jamani hii biashara usifanye ukajua utafanikiwa ndani ya mwaka mmoja.
Mimi hapa nilipo nimefungua mara ya tatu. Nilifungua sehemu ya kwanza mauzo yakawa chini nikashindwa kulipa kodi nikafunga, nikaenda sehemu nyingine zikatokea changamoto kubwa sana nikafunga, nikaenda sehemu nyingine hapa nilipo kwakweli Alhamdulillah. Kama umeamua kufanya usifel mara moja ukaacha, jaribu jaribu jaribu na tena.

Pia kumbuka biashara nzuri ni ile unayoianza na mtaji kiduchu ukaikuza taratibu. Biashara ya kuanza na mtaji mkubwa au biashara ya kufunguliwa na mtu ni mara chache sana hudumu.
Wewe binafsi epuka kufanya biashara yako kwa mikopo. Tumia hela yako \ mtaji wako binafsi hata kama ni mdogo.

Angalizo; Ukimuajiri mtu dukani usitarajie maendeleo.
Mnaonaje tuanzishe group la wasap tuwe tunashea mawzo ya kibiashara..hasa wa maduka ya reja reja
 
Back
Top Bottom