chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Aisee umegusa penyewe, kwenye biashara yoyote ile ni kinachowaangusha watu ni detail ndogo ndogo sana ambazo wanazipuuza, Wahindi na Waarabu wamefanikiwa sana sababu ya attention to details, disciplineHilo la Imani na mambo ya kishirikina litakuangusha usipokuwa makini. Nasema hivi kwa sababu kwenye biashara HAKUNA ushirikina. Huduma yako nzuri kwa wateja ndiyo ushirikina. Kwa uchunguzi wangu ni kuwa maduka mengi Bongo customer care zao ni majanga. Hili la ubovu wa customer care ni jambo common kiasi cha ku weza kuliandikia kitabu kikubwa kama biblia. Baadhi ya tabia mambo mabovu:
1. Dukani kwa nje kukaa watu (hasa vijana) wasio na kazi na kuangalia/kusikiliza kwa udadisi kila anayekuja dukani
2. Wenye maduka kuhudumia wateja huku wanafanya shughuli nyingine kama kuzungumza na simu etc
3. Kauli chafu za wauzaji
4. Kutokuandaa chenji za kutosha hivyo kulazimika kurudisha baadhi ya wateja au kuwachelesha.
5. Kuhudumia kwa dharau wateja wanaonunua mali za bei ndogo
6. Kuuza vitu vyenye hitilafu kwa ujanja ujanja au kurudisha chenji za noti mbovu bila kujali kuwa mteja asiporidhika leo kesho harudi tena
7. Wenye duka wanaume kutongoza wasichana wanaokwenda dukani eg ma-house girls
8. Kutoa majibu ya mkato na kukasirika wanapokutana na mteja msumbufu
9.
10.
11. Kuna mengi sana unatakiwa uzingatia.
Waafrika wote tungeukuwa makini hivi tungekua mbali sana