Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Kujitegemea haiwezekani kabisa .. Gesi tunayo lakini bei inapangwa na wazungu..mafuta yapo bei inapangwa na wazungu..dhahabu ipo bei inapangwa na wazungu...tukubali tu maendeleo yetu yatatokana na wazungu.
Nigeria wana mafuta lakini bado maskini. Mawaziri wanakomba pesa zote hazina na kuhaimshia akaunt zao. Angola wana mafuta lakini yako kwa wachache akiwepo mke wa raisi??. Bado maskini. Mozambiki wana gesi lukuki lakini safari bado ndefu.
Labda Botswana angalau wananchi wanafaidi raslimali zao;
Tujipe moyo
 
Kujitegemea ni safari ndefu iliyojaa changamoto, naomba ufahamu kua kamwe hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada ya wahisani, ni lazima ifike mahali tuweze kujiendeleza kwa kutumia uwezo wetu wa ndani. Hata wewe huwezi kuendeleza maisha yako na familia kwa kutegemea misaada.
 
mkuu we umenena..yaan watu wanatumia swala la kujitegemea wanafunika kwamba dhulma ya zanzibar ni moja ya mambo yaliyofanya tusitishiwe huu msaada...watu mbona hawajibu hoja za MCC za kusitisha msaada wananza kuzunguka mbuyu!

Ni lini dhulma haikuwahi kufanyika Zanzibar?
 
Mwehu.
 
huu mtazamo wako uko sawa kabisa na yale tunayoyackia toka kwa viongoz wa ccm kila cku...tunatofautiana mitazamo mkuu binafsi ctokuja kuamini kwamba hakukuwa na dhulma iliofanyika ila kama ww ndo hvyo unasema haki ilikuwepo kwa 100% siwez kukubishia mana kila mtu ana jinsi anavyoliona jambo flan
 
We jamaa unatakiwa kujua kuwa tumenyimwa hiyo misaada sababu ni hzo kasoro za uchaguzi zanzibar na issue ya cybercrime lkn ukweli ni kuwa wamekatisha hiyo misaada ili kutukomesha kwa maana ss ni tegemezi kwao hvyo wanategemea tuwapigie magoti kuhusu hilo na pia wapo watz wenzetu wanaoamini ss kama taifa hatuwezi kujitegemea hvyo tutaathirika kwa kukosa hiyo misaada!! Hoja ni kwamba je na ww unasupport kuwa hatuwezi kujitegeme hvyo kukosekana kwa hiyo misaada itakuwa ni tishio kwa uhai wa taifa letu,,hvyo hapa ndipo kwenye hoja maana mwandishi alitaka kutuonyesha kuwa tuna uwezo wa kujitegemea je ww unaonaje kuhusu mtazamo huo??!!
 
mkuu c kwamba sifaham hilo...ila kuna watu wanatumia hilo kufunika mauzauza ya zenji wanadai zenj hakuna baya lolote lililotokea ila tu hawa wamarekan wana hila zao.......lakin issue ni kuwa zenji kulikua na madudu na hawa wamarekan na wenzao wa ulaya wakatumia issue ya zenji kama excuse ya kusepa zao........
 
I love this piece.. a very candid take on the whole question of American Aid.. thanks for sharing
Naona kwa wazi kabisa kuwa wewe ni mkereketwa wa chama na huna hoja..
Hii ni kwasabab hizo hoja unazojenga hapo hazina shida kama tungeamua kujitegemea kwa kuwa na mipango ya wazi kabisa ila sio mmevurunda hafu et ndo mnadandia hoja ya kujitegemea ili kuficha maovu yenu
 
Mkuu MM , nashukuru kwa maoni yako ingawa hayakujibu maswali haya kwa ukamilifu

1. Ni nani anayelalamika kuhusu kurugwa kwa uchaguzi?
2. Je, ni kweli Jecha alichukuliwa na 'vyombo' au si kweli?
3. Je, kuna kumbu kumbu za kikao cha tume kuhusu kufutwa uchaguzi?
4. Je, ni dai au madai gani yaliyoelezwa na tume a.k.a Jecha?
5. Sheria gani ya ZNZ inayosema tume inaweza kufuta uchaguzi wote?
6. Ni sharia gani ya ZNZ inayoeleza kuhusu uchaguzi wa marudio?

Kwa atakayekusoma vema na kwa kina, tayari ulishachukua upande(ni haki kwasasabu ni maoni yako). Ni vema niangalie maoni yako kwa msingi huo

1. Unapozungumzia 'nullification' iliyotokana na ZEC, nimekuuliza , je kuna kumbu kumbu zozote za kikao cha jumla cha ZEC kuhusu hilo?

2. '' This ....should be settle in court of law''
Swali lingine, Je, kifungu gani cha sheria kinaeleza masuala ya uchaguzi kutafutiwa ufumbuzi mahakamani?

Je, kipo kufungu kinachoeleza uamuzi wa tume kuweza kupingwa mahakamani?

Je, kifungu gani kinaeleza uchaguzi ukiwa na matatizo majimbo 2, 3,4 au 5 tume inapaswa kufuta matokeo ya Jumla?

Ni kifungu gani cha sheria kinachoeleza utaratibu wa kufuatwa baada ya matokeo ya jumla kufutwa?

3. ''What most people probably missed in Jecha?s reasoning for the cancellation of the Presidential results is the inference on who is responsible for meddling with the election process. If we were to believe his points of irregularities the whole mess started in Pemba. Point 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter clearly accuse (not by mentioning names) that CUF which has an overwhelming presence in Pemba for interfering with the process. This was capped up with Seif declaring himself a winner and thus putting ZEC in crossfire. There was no way out for ZEC; declare Seif the winner and thus ignore those issues raised in points 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter to the wrath of the ruling party or declare Shein the winner and ignore Seif?s allegations. To be between the rock and the hard place would have been a better than this position. He chose the way out ? nullify the whole process to the anger of probably both''

Kama unakubali Jecha alifuta bila kunukuu kifungu cha sheria, je, bado unaamini ZEC ilifuta uchaguzi?

Na kama kulikuwa na malalamiko , nani alilamika kwa ZEC na kwa kumbu kumbu gani?

Kumbuka, kazi ya ZEC si kushiriki uchaguzi ni kusimamia uchaguzi, vipi ZEC iliona tatizo ikiwa hakukuwepo mlalamikaji?

Na ZEC inayolalamika irregularities, ni ipi ikiwa maeneo yanayolalamikiwa, ZEC ilitoa vyeti vya ushindi?

''Last note is that this issue is a Tanzanian issue and I believe with all the deficiencies we have in our legal system we still are capable of addressing them''

Katika maswali uliyouliza, hili linatoa jibu kwako kwanini CUF hawakwenda mahakamani

Defficiencies katika legal system yetu ambapo mwenyekiti wa NEC au ZEC pamoja na Majaji wakuu wanaweza kuwa 'wanachama' wa vyama vya siasa ''under cover'' umeli address vizuri sana

Je, bado unaamini katika CUF kwenda mahakamani?

Lakini pia kuna jingine ambalo hukujibu. Ikiwa Jecha aliyekuwa katika ulinzi wa Taifa na tume yake , aliweza 'kutekwa' bila serikali kujua tena wenzake wakiwa hawajui na ikiwa serikali haijakanusha hilo, nini kilishindikana kwa Jaji 'kutekwa' katika Jecha style?
 
Kwa sasa hakuna nchi yenye uwezo wa kukataa misaada kwa wahisani...
 
Punguza matumizi?
 
Kwani hao bibi na babu yako wameanza kuishi kijijini mwaka huu? Miaka yote umewafikiria kwa misaada what happened?
MM, kuna watu wanapotosha,na mimi nashindwa kuelewa dhana husika. Dhana ya kujitegemea tunayoipigia chapuo na mimi ni mmoja wao. Lakini kama mdau mmoja alivyochangia, hilo jambo ni hatua, haliwez tu kuja eti kisa MCC hela yao imekatwa. Pia kuna mchangiaji alijiuliza kwa nini MCC baada ya kujitoa hela zake zionekane si chochote, lakini majuzi hapa imetangazwa Billion 106> za Japan zimepigiwa chapuo balaa. Kumbe dhana ya kujitegemea inatoka wapi ikiwa bado tunakopa? Kumbuka deni la Taifa ni 42Tn/- na kwa hiyo baada ya mkopo wa jana deni litapanda hadi 42.106Tn/-! Mtu anaejitegemea kweli atakua na deni ambalo ni mara mbili ya bajeti yake? Hapa kuna walakini na ukweli hausemwi! Kujitegemea kuwe ni mkakati maalum, lakini isifanyike kwa kufuatana na matukio, hapo tutakua tunajidanganya.
Nimalizie tu kwa kusema, tunahitaji kujitegemea, lakini twende taratibu kwa step! Tusitukane wakunga na uzazi ungalipo! Pesa za MCC tulizihitaji sana, ila tumejishindishwa wenyewe. Masharti yale ni rahisi kutekelezeka! Nasikitika sana. Kule kwetu tulitegemea kuunganishwa mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa hii MCC2,na hivyo route ya Mtwara Corridor ingeanzia Mtwara-Masasi-Tunduru na Namtumbo hadi Mbamba Bay kwa route hiyo na route nyingine ingerahasisha barabara kuwa kuu hadi Songea-Njombe Makambako kulelekea Mbeya. Sasa hapa inabidi tujipinde hasa kuweza kufudia deficit!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…