Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Kujitegemea haiwezekani kabisa .. Gesi tunayo lakini bei inapangwa na wazungu..mafuta yapo bei inapangwa na wazungu..dhahabu ipo bei inapangwa na wazungu...tukubali tu maendeleo yetu yatatokana na wazungu.
Nigeria wana mafuta lakini bado maskini. Mawaziri wanakomba pesa zote hazina na kuhaimshia akaunt zao. Angola wana mafuta lakini yako kwa wachache akiwepo mke wa raisi??. Bado maskini. Mozambiki wana gesi lukuki lakini safari bado ndefu.
Labda Botswana angalau wananchi wanafaidi raslimali zao;
Tujipe moyo
 
Shida sio misaada, Hoja walizojenga mbona hamzungumzii???? mbona unajitoa ufahamu bure? wewe upo marekani, unaelewa maana ya kukaa na kiza mwezi mzima? acha kufurahisha genge kaka....
Tumejiandaaje kujitegemea kama sio unaongea vitu vya kufikirika? unadhani maisha ni riwaya?
Kujitegemea ni safari ndefu iliyojaa changamoto, naomba ufahamu kua kamwe hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada ya wahisani, ni lazima ifike mahali tuweze kujiendeleza kwa kutumia uwezo wetu wa ndani. Hata wewe huwezi kuendeleza maisha yako na familia kwa kutegemea misaada.
 
mkuu we umenena..yaan watu wanatumia swala la kujitegemea wanafunika kwamba dhulma ya zanzibar ni moja ya mambo yaliyofanya tusitishiwe huu msaada...watu mbona hawajibu hoja za MCC za kusitisha msaada wananza kuzunguka mbuyu!

Ni lini dhulma haikuwahi kufanyika Zanzibar?
 
Tatizo ni sisi Watanzania Bara kujifanya tunajua sana yanayotokea Zanzibar kuliko Wa Zanzibari wenyewe, Atii shughuli za uzalishaji zimesimama, mara zimedorola, kwa taarifa taarifa Zanzibar ilisimama pale Seif alipojitangazia ushindi, hofu ilitanda kote na watu kujifungia ndani. Jecha alinusuri hali ile baada ya kufuta matokeo watu wakarejea mitaani.

Mapicha na video za mitandaoni qmbqao ni propaganda za kugushi haiwezi kuwa kigezo cha kudai kuwa Zanzibar hakuna Amani, na hapa niseme ndiyo umuhimu Cybercrime Law inatakiwa ifanye kazi kweli, Bahati yao wawekao picha nq video hizo, JF wamefungua kesi Mahakama kuu kupinga kutii amri ya serikali ya kutoa taarifa ya vyanzo vya taarifa kwenye mtanzano wake. Lakini ni ukweli matukio ya eneo jingine yanawekwa ili kuonyesha ni hali ilivyo sasa Zanzibar moja ni hiyo video unayo zungumzia ambayo ni tukio la Tanzania Bara la vurugu miaka ya nyuma Waumini walioijifungia pale msikiti wa Mwembechai wakiamini askari hawataingia.
Mwehu.
 
Hizo unazoziita kashfa zimejadiliwa sana humu na zimetolewa sana ufafanuzi lakini sababu ya mihemko ya mahaba ya kivyama hakuna anayekubaliana na mawazo ya mwenzie.
Sababu ya kwanza ni kunyimwa msaada huu ni kutoridhishwa ni jinsi ulivyoshughulikiwa mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar na kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao haukuwa shirikishi. Mtanzania gani leo ni kipofu wa juhudi zilizofanywa kushughulikia mgogoro huu? Yale mazungumzo ya kutafuta muafaka haikuwa juhudi ya kushughulikia tatizo? aliyekwamisha mazungumzo yale alikuwa nani aliyeenda Serena Hotel na kutangaza hana shida ya maridhiano? Kurudiwa kwakitaki. sijui walitaka nchi ikae bila Rais kwa muda gani mpaka hapo wanaotaka kubembelezwa kushiriki wajisikie saswa uchaguzi ni matokeo ya mtu kudanganywa ajitoe katika mazungumzo kuna mataifa yatakuunga mkono huo ni utumwa wa kifikra katika siasa za Kiafrika. Marekani wenyewe waliwahi kufuta matokeo ya Jimbo zima la Texas sababu ya utata wa utoboaji wa karatasi za kupigia kura yaliyoelekea kumpa ushindi mmoja wa wagombea katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki.

Madai mengine ya kijinga ni ya uchaguzi kutokuwa shirikishi. Ushirikishi kwa wenzetu hawa ni kulazimisha wale walioamua kwa hiari yao kutoshiriki washiriki. leo hawaamini mtu kuamua kushiriki au kutoshiriki mchakato wa uchaguzi nayo ni Demokrasia. Na wanaoshangilia uamuzi huu wa MCC ni wale waliokuwa wakilalamika wasilazimishwe kushiriki kitu ambacho wao ha
a wanataka kushiriki.

Suala la Cyber crime law ni la taratibu na sheria za kibunge zaidi, Serikali ilishatoa maelezo kama kuna mapungufu katika sheria ile mapendekezo ya marekebisho yanatakiwa kupitia katika taratibu za kawaida za kibunge. Sasa mtu utashangaa walitaka uchaguzi uahirishwe mpaka marekebisho hayo yafanyike? na yangefanywa na chombo gani hali kuwa muda wa wawakilishi wetu umeisha? Hivi tufikirie kana Watanzania mswada ule ungalikuwa haujapitishwa, uchaguzi wa 2015 ungalikuwaje ukizingatia uhuni na uchochezi uliokuwa ukifanywa kupitia mtandao? kama ilifikia waharifu wa mtandao kuaminisha kuwa sasa nchi haina mkuu wa majeshi ati amekufa, lengo lilikuwa nini? Ukizingatia na wageni walioletwa kusaidia baadhi ya vyama kitekinologia kujaribu kuharibu matokeo Ni lazima tukubali hii sheria imesaidia sana uchaguzi huu kuwa wa Amani kama si hivyo kungalitokea machafuko makubwa.
huu mtazamo wako uko sawa kabisa na yale tunayoyackia toka kwa viongoz wa ccm kila cku...tunatofautiana mitazamo mkuu binafsi ctokuja kuamini kwamba hakukuwa na dhulma iliofanyika ila kama ww ndo hvyo unasema haki ilikuwepo kwa 100% siwez kukubishia mana kila mtu ana jinsi anavyoliona jambo flan
 
hakuna mtu anayepinga swala la kuacha utegemezi..issue hapa ni kwann jamaa wamesitisha hio misaada..mbona mkuu unataka kuzima ukweli kuwa swala la zanzibar ni moja ya chanzo cha kusitishiwa msaada...hebu kwanza tusifiche kuwa mauzauza ya zenji ni moja kati ya sababu tuache kufunikafunika mambo hapa
We jamaa unatakiwa kujua kuwa tumenyimwa hiyo misaada sababu ni hzo kasoro za uchaguzi zanzibar na issue ya cybercrime lkn ukweli ni kuwa wamekatisha hiyo misaada ili kutukomesha kwa maana ss ni tegemezi kwao hvyo wanategemea tuwapigie magoti kuhusu hilo na pia wapo watz wenzetu wanaoamini ss kama taifa hatuwezi kujitegemea hvyo tutaathirika kwa kukosa hiyo misaada!! Hoja ni kwamba je na ww unasupport kuwa hatuwezi kujitegeme hvyo kukosekana kwa hiyo misaada itakuwa ni tishio kwa uhai wa taifa letu,,hvyo hapa ndipo kwenye hoja maana mwandishi alitaka kutuonyesha kuwa tuna uwezo wa kujitegemea je ww unaonaje kuhusu mtazamo huo??!!
 
We jamaa unatakiwa kujua kuwa tumenyimwa hiyo misaada sababu ni hzo kasoro za uchaguzi zanzibar na issue ya cybercrime lkn ukweli ni kuwa wamekatisha hiyo misaada ili kutukomesha kwa maana ss ni tegemezi kwao hvyo wanategemea tuwapigie magoti kuhusu hilo na pia wapo watz wenzetu wanaoamini ss kama taifa hatuwezi kujitegemea hvyo tutaathirika kwa kukosa hiyo misaada!! Hoja ni kwamba je na
mkuu c kwamba sifaham hilo...ila kuna watu wanatumia hilo kufunika mauzauza ya zenji wanadai zenj hakuna baya lolote lililotokea ila tu hawa wamarekan wana hila zao.......lakin issue ni kuwa zenji kulikua na madudu na hawa wamarekan na wenzao wa ulaya wakatumia issue ya zenji kama excuse ya kusepa zao........
 
I love this piece.. a very candid take on the whole question of American Aid.. thanks for sharing
Naona kwa wazi kabisa kuwa wewe ni mkereketwa wa chama na huna hoja..
Hii ni kwasabab hizo hoja unazojenga hapo hazina shida kama tungeamua kujitegemea kwa kuwa na mipango ya wazi kabisa ila sio mmevurunda hafu et ndo mnadandia hoja ya kujitegemea ili kuficha maovu yenu
 
Mimi jibu langu - na haya ni mawazo yangu tu:
Tarehe ile ya 28 Oktoba mimi niliandika mada hii kuelezea mawazo yangu siku ile. Baadhi ya maswali yako yanajibika mle. Nitajinukuu kidogo tu na naamini hatuko mbali kifikra katika hili.

Juu ya Jecha na kufuta uchaguzi:

the only grave issue here is the authority of NEC or its chairman to nullify the whole election based on some irregularities that could have been dealt with otherwise. As I read Chairman Jecha?s letter to announce his decision I found nowhere in it where the chairman argued a point of law to defend his decision. He didn?t mention a single law to show that indeed he has the power to nullify the law. This does not mean he doesn?t or that NEC doesn?t have that authority. This means then that this question cannot be settled by politicians who would benefit either way with the decision. This issue should be sorted and settled in a court of law immediately. Everything else stands or falls on this point.

Nikaeleza tena kidogo kuwa:

What most people probably missed in Jecha?s reasoning for the cancellation of the Presidential results is the inference on who is responsible for meddling with the election process. If we were to believe his points of irregularities the whole mess started in Pemba. Point 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter clearly accuse (not by mentioning names) that CUF which has an overwhelming presence in Pemba for interfering with the process. This was capped up with Seif declaring himself a winner and thus putting ZEC in crossfire. There was no way out for ZEC; declare Seif the winner and thus ignore those issues raised in points 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter to the wrath of the ruling party or declare Shein the winner and ignore Seif?s allegations. To be between the rock and the hard place would have been a better than this position. He chose the way out ? nullify the whole process to the anger of probably both.

Nikatoa wito kuwa:

As I have said above the issue of ZEC power to nullify election is the fundamental one to be dealt here and as a matter of fact urgently.

Sasa, sijui kwanini unaweza kudhania kuwa sijajali sana hoja hii nzito ya masuala hayo. Lakini niliamini wakati ule na nikatoa neno la hekima tu kuwa:


Last note is that this issue is a Tanzanian issue and I believe with all the deficiencies we have in our legal system we still are capable of addressing them. Foreign entities should not be allowed to put undue pressure on the country. This is a very delicate time and we should expect our friends to refrain from inflaming the wounded sentiments of our people. They should be wise to let the Tanzanian people sort these things on their own.
Mkuu MM , nashukuru kwa maoni yako ingawa hayakujibu maswali haya kwa ukamilifu

1. Ni nani anayelalamika kuhusu kurugwa kwa uchaguzi?
2. Je, ni kweli Jecha alichukuliwa na 'vyombo' au si kweli?
3. Je, kuna kumbu kumbu za kikao cha tume kuhusu kufutwa uchaguzi?
4. Je, ni dai au madai gani yaliyoelezwa na tume a.k.a Jecha?
5. Sheria gani ya ZNZ inayosema tume inaweza kufuta uchaguzi wote?
6. Ni sharia gani ya ZNZ inayoeleza kuhusu uchaguzi wa marudio?

Kwa atakayekusoma vema na kwa kina, tayari ulishachukua upande(ni haki kwasasabu ni maoni yako). Ni vema niangalie maoni yako kwa msingi huo

1. Unapozungumzia 'nullification' iliyotokana na ZEC, nimekuuliza , je kuna kumbu kumbu zozote za kikao cha jumla cha ZEC kuhusu hilo?

2. '' This ....should be settle in court of law''
Swali lingine, Je, kifungu gani cha sheria kinaeleza masuala ya uchaguzi kutafutiwa ufumbuzi mahakamani?

Je, kipo kufungu kinachoeleza uamuzi wa tume kuweza kupingwa mahakamani?

Je, kifungu gani kinaeleza uchaguzi ukiwa na matatizo majimbo 2, 3,4 au 5 tume inapaswa kufuta matokeo ya Jumla?

Ni kifungu gani cha sheria kinachoeleza utaratibu wa kufuatwa baada ya matokeo ya jumla kufutwa?

3. ''What most people probably missed in Jecha?s reasoning for the cancellation of the Presidential results is the inference on who is responsible for meddling with the election process. If we were to believe his points of irregularities the whole mess started in Pemba. Point 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter clearly accuse (not by mentioning names) that CUF which has an overwhelming presence in Pemba for interfering with the process. This was capped up with Seif declaring himself a winner and thus putting ZEC in crossfire. There was no way out for ZEC; declare Seif the winner and thus ignore those issues raised in points 2, 3, 4, 7 and 9 in his letter to the wrath of the ruling party or declare Shein the winner and ignore Seif?s allegations. To be between the rock and the hard place would have been a better than this position. He chose the way out ? nullify the whole process to the anger of probably both''

Kama unakubali Jecha alifuta bila kunukuu kifungu cha sheria, je, bado unaamini ZEC ilifuta uchaguzi?

Na kama kulikuwa na malalamiko , nani alilamika kwa ZEC na kwa kumbu kumbu gani?

Kumbuka, kazi ya ZEC si kushiriki uchaguzi ni kusimamia uchaguzi, vipi ZEC iliona tatizo ikiwa hakukuwepo mlalamikaji?

Na ZEC inayolalamika irregularities, ni ipi ikiwa maeneo yanayolalamikiwa, ZEC ilitoa vyeti vya ushindi?

''Last note is that this issue is a Tanzanian issue and I believe with all the deficiencies we have in our legal system we still are capable of addressing them''

Katika maswali uliyouliza, hili linatoa jibu kwako kwanini CUF hawakwenda mahakamani

Defficiencies katika legal system yetu ambapo mwenyekiti wa NEC au ZEC pamoja na Majaji wakuu wanaweza kuwa 'wanachama' wa vyama vya siasa ''under cover'' umeli address vizuri sana

Je, bado unaamini katika CUF kwenda mahakamani?

Lakini pia kuna jingine ambalo hukujibu. Ikiwa Jecha aliyekuwa katika ulinzi wa Taifa na tume yake , aliweza 'kutekwa' bila serikali kujua tena wenzake wakiwa hawajui na ikiwa serikali haijakanusha hilo, nini kilishindikana kwa Jaji 'kutekwa' katika Jecha style?
 
Kwa sasa hakuna nchi yenye uwezo wa kukataa misaada kwa wahisani...
 
Kama kweli mi saada si kitu kwetu kwanini iwe habari ya mjini tunaongozwa na viongozi wenye empty mind kiingeleza tu shida utaperi na uhuni umetawara kwa mtu mweusi marekani wa metuunga mkono wanyonge ambao atukupiga kura kwakua haki imekandamizwa kilamtu analijua ilo Tanzania sio ya watu wachache yakwetu wote? Naamini hatufiki popote bira msaada mapato na matumizi vinapishana runakusanya kodi vizur matumizi hayaendani na kodi nipo apa kama mtu ajarudi kupiga mogoti
Punguza matumizi?
 
Kwani hao bibi na babu yako wameanza kuishi kijijini mwaka huu? Miaka yote umewafikiria kwa misaada what happened?
MM, kuna watu wanapotosha,na mimi nashindwa kuelewa dhana husika. Dhana ya kujitegemea tunayoipigia chapuo na mimi ni mmoja wao. Lakini kama mdau mmoja alivyochangia, hilo jambo ni hatua, haliwez tu kuja eti kisa MCC hela yao imekatwa. Pia kuna mchangiaji alijiuliza kwa nini MCC baada ya kujitoa hela zake zionekane si chochote, lakini majuzi hapa imetangazwa Billion 106> za Japan zimepigiwa chapuo balaa. Kumbe dhana ya kujitegemea inatoka wapi ikiwa bado tunakopa? Kumbuka deni la Taifa ni 42Tn/- na kwa hiyo baada ya mkopo wa jana deni litapanda hadi 42.106Tn/-! Mtu anaejitegemea kweli atakua na deni ambalo ni mara mbili ya bajeti yake? Hapa kuna walakini na ukweli hausemwi! Kujitegemea kuwe ni mkakati maalum, lakini isifanyike kwa kufuatana na matukio, hapo tutakua tunajidanganya.
Nimalizie tu kwa kusema, tunahitaji kujitegemea, lakini twende taratibu kwa step! Tusitukane wakunga na uzazi ungalipo! Pesa za MCC tulizihitaji sana, ila tumejishindishwa wenyewe. Masharti yale ni rahisi kutekelezeka! Nasikitika sana. Kule kwetu tulitegemea kuunganishwa mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa hii MCC2,na hivyo route ya Mtwara Corridor ingeanzia Mtwara-Masasi-Tunduru na Namtumbo hadi Mbamba Bay kwa route hiyo na route nyingine ingerahasisha barabara kuwa kuu hadi Songea-Njombe Makambako kulelekea Mbeya. Sasa hapa inabidi tujipinde hasa kuweza kufudia deficit!
 
Back
Top Bottom