Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Naunga mkono kukataa misaada lkn serikali inampango gani kwenye kujifunga mkanda mana tusije pata msote wachache then viongozi wale kuku wote tuingie giza ili kufanya pesa iende kwenye maendeleo tupige mnada magar ya kifaahari ya serikal ili kujijengea uwezo zaidi wakandarasi wa ndani makampuni ya ujenzi ya bongo yapewe tenda kizalendo na kufanya kaz kuwe na wazir wa kuajiliwa kufanya kaz ipasavyo kuwe na dira ili waziri mwenyekuweka kutekeleza kwa awamu apewe mkataba akishindwa kufungwa na kufilisiwa na sekta muhimu zipewe uwezo na umakini kwa muda maalum apo wengi tutaenda shamba kulima maana umoja wa kitaifa utakuwepo kama wakipitisha katiba ile ya warioba itakua imefanikiwa zaid lakin kwa wengine wachache kupinga vitu bila hoja tutaona vioja sna hiki rais huyu anavunja na kujenga akija mwingine anavunja cha mwenzie na kuanza cha kwake
 

Usaliti ni kuwa na msimamo katika ukweli; wasaliti wa demokrasia ndio wamekuwa mashujaa wenu sasa?

Kweli huu uchizi. Wewe huyohuyo unasema "Siasa za Zanzibar" halafu kuna "wasaliti wa demokrasia". Tendea haki neno demokrasia, kabla ya kuandika tuu kwa njaa. Ukweli unajulikana Zanzibar CCM wamekuwa wakiiba matokeo, wewe hujui hilo? Jecha ni instrument tu pale ya mabwanyenye wenye mali na ardhi ambao wanahofia serikali mbadala. Sababu zingine za kipuuzi eti Zanzibar nchi ya kimapinduzi, kwani nchi ngapi duniani zilipitia mapinduzi na sasa demokrasia inatawala?

Eti irrelevant? Wapi?
 
Kuna wakati ambao inatubidi tuseme ukweli tu, kama kweli tunataka tujitegemee ni lazima tubadilike, tuje na vision na mission za kujitegemea ya kipindi cha miaka 20 lakini tukigawanye katika awamu nne ya miaka mitano mitano. Maana yake kipindi chote cha utawala wa Magufuli kama mungu atamsaidia akafikisha pengine miaka 10 aweke misingi hiyo ya kujitegemea, kama tuko serious na neno kujitegemea basi hatuna budi kuanza na Mapinduzi ya Kilimo, Viwanda na Utoaji wa Huduma kwa Jamii. Tutenge mikoa kazaa kwa ajiri ya viwanda tu, tuiite ukanda wa viwanda Tanzania, Pili tuanzishe kilimo cha kisasa, tuwahamasishwe bwana shamba wote wanaomaliza vyuo waende vijijini kusimamia kilimo, pia tutoe vifaa vya kisasa na kiwe na kilimo cha umwagiliaji ili mazao yanayopatika moja kwa moja yaende viwandani kwa ili tutengeneze bidhaa tuweze kuuza nchini na kusafirisha nchi za nje tuweze kuinua pato la Taifa hivyo serikali itaweza pata pesa nyingi za kuweza kutoa huduma za jamii kwa wananchi eg kujenga miundo mbinu, madawa mahosipitali, kujenga mashule, kujenga bandari , airports ili kuchochea maendeleo. Pia tukiwa tuna export thamani ya pesa yetu itaongezeka hivyo kuchochea wawekeza kuja TZ kuweekeza, leo hii pesa ya tanzania its unstable currency,leo imebadilika kuwa hivi kesho kuwa vile, haivutii wawekezaji, hivyo kufanya flow ya pesa nchini kuwa ndogo. Sasa Hii misaada kwa sasa tuichukue ili iweze kufanikisha kwanza azima yetu ya kilimo, ujenzi wa viwanda kimya kimya kwa muda fulani, then tunakuja tunaipiga chini tukiwa stable. Leo hii ukiniambia tunajitegemea wakati serikali haina pa kushika zaidi ya kukata PAYE za wafanyakazi na vikontena viwili bandari inakuwa ngumu, pato letu kwa mwezi tukilipa wafanyakazi , tukalipa madeni ya wakandarasi na maendeleo kidogo tayari pesa zote zinakwisha ,serikali iko broke kila mahali then unaniambia tujitegemee nakuwa sikuelewi, **** mambo mengine hayana siasa ,tunatakiwa just to comply with donors tupate misaada yao at the same time tunaendelea na plan zetu za kujitegemea, otherwise tutawaumiza watanzania bure, kwani kama tungepata hizo trion 1 zingeliajiri wtz wangapi? tungesema tuzimwage kwenye viwanda tungelijenga viwanda vingapi? tuweni wakweli.
 
Shida ni misaada...unadhani ingekuwa sio msaada kwa nini wasiseme tunasitisha uhusiano let say wa kibiashara?
 
Ina maana bila MCC hiyo njia isingajengwa?
Unaujua mfuko wa barabara?
Unajua ni kiasi gani cha fedha za kitanzania zilitumika hapo?
 
Mbona hiyo misaada ilikuwa inatolewa miaka ya nyuma kwanini mna kaa giza mpaka leo ??
 
Mbona hiyo misaada ilikuwa inatolewa miaka ya nyuma kwanini mna kaa giza mpaka leo ??

Kwani MCC ilianzishwa mwaka gani?
Hata hivyo CCM ipo kwenye position nzuri sana kujibu hilo swali lako la msingi.... kwamba kwa miaka 55 tumeshindwa kujitegemea, leo kwa kunyimwa misaada kwa ulafi wa madaraka mnakuja na drama za uzalendo na blabla...kujitegemea bila viwanda, umeme wa uhakika na uzalishaji wa kibiashara umeona wapi mkuu
 
Hilo ndio tatizo; kwa hiyo kama Uchaguzi wa Zanzibar usingefutwa na Shein angeshinda kihalali bado watu mngeendelea kutaka misaada?

Kuna mambo mnataka kuchanganya hapa. Sasa sijui ni kwa bahati mbaya au ni makusudi tu. Tuliosoma somo la Siasa ni kwamba chuki dhidi ya Misaada tulipewa wakati huo. Ilikuwa ni chuki ya kielimu na wazi kabisa. Jiulize ni kwa nini bado tunaamini katika hiyo misaada kupitia tune ya SAP hasa leo kupitia kejeli ya Zanzibar. Nimesema kejeli ya Zanzibar
 
Kama kauli yako ingerandana na mawazo ya viongozi wa UKAWA unafikiri kungekuwa na mabishano kama hivi. La hasha. Ungepata like hadi ungeomba poo. Kama kauli ya kutoshabikia misaada katika kipindi hiki angeitoa kiongozi wa UKAWA ungeona maoni tofauti na haya yanayoendelea katika mitandao.
Kwa ufupi wa fikra hivi sasa watanzania tumekuwa washabiki wa maneno ya viongozi wa vyama na sio mantiki au uhalisia wa kauli. Hakuna mtu anayependa kuishi kwa kuombaomba. Tusiwe muflisi wa fikra, hili jambo halifurahishi hata kidogo. Kila kiongozi wakati wa kampeni alikuwa anahubiri jinsi ya kuondokana na utegemezi, leo hali imekuwa tofauti kabisa, misimamo imebadilika. Kulikoni? Tulikuwa tunasikia wanasiasa wanajinadi "nchi hii ni tajiri lakini tumekuwa ombaomba." Hili geuko la ghafla linatokana na nini? Hili jambo kwa kipindi hiki limegubikwa na utashi wa kisiasa lakini mwanzoni viongozi wa serikali walikuwa wanalaumiwa sana kwa kutembeza mabakuli kwa wafadhali.
Leo muombwa amekuwa tofauti kwa sababu tofauti ambazo zinazobadilika kila inapofika kipindi cha kutoa msaada sasa fikra za watu zimehama na kuwa tofauti na misimamo yao ya awali. Je shida ni Zanzibar au Sheria ya Mtandao ndizo zinazobadilisha fikra zetu? Hata tukitimiza matakwa yao kwa kipindi kijacho tutasikia mambo mapyaaa, jamaa wanatudhalilisha sana! Hebu tubadilike tuepuke huu udhalilishaji.
 
Ina maana bila MCC hiyo njia isingajengwa?
Unaujua mfuko wa barabara?
Unajua ni kiasi gani cha fedha za kitanzania zilitumika hapo?
Usujtie ujuaji wa kipunda barabara hizo na ile ya Namtumbo/Songea/Mbinga ni fedha za MCC
Source yako ya information ni gazeti la Uhuru hujui lolote ushuzi mtupu
YOU do justice to your name
 
Demokrasia inakuwepo wakati gani?..kwa hiyo Sefu alivyosema kapata zile kura alizosema ndio demokrasia?
 
Usujtie ujuaji wa kipunda barabara hizo na ile ya Namtumbo/Songea/Mbinga ni fedha za MCC
Source yako ya information ni gazeti la Uhuru hujui lolote ushuzi mtupu
YOU do justice to your name
Hivi unajuwa zaidi ya nusu ya fedha za MCC hurudi US?..Hivi unajuwa kauli ya Raisi kukataa kuongeza mikataba kwa Syimbion ni sababu ya kusitish?...Hivi unajuwa US hupata faida ya hadi mara tano ya kila dola anayotowa?..hivi unajuwa kampuni binafsi za kimarekani zimepata pigo?...Hivi unajuwa US/EU na vibaraka wao wa ukawa kwa pamoja walishindwa uchaguzi?...Hivi unajuwa kwamba Luwasa aliingia mikataba ya siri na serikali za kimagharibi wakiamini angepitishwa na CCM...na hata wamefadhili kampeni zake?
 
Kwa nini unakwepa tatizo halisi ambalo ni ukiukwaji wa democrasia nchini na matumizi mabovu ya sheria ya mtandao kuumiza wananchi kwa maslahi ya watawala?

Kuna mendeleo yakinifu chini ya utawala mbovu usiojali wananchi badala yake unalinda genge la watawala?

Unapiga kelele juu ya wageni na misaada, mbona sioni unaongelea njia mbadala za kufikia kujiendeleza bila kuwaumiza Wafanyakazi wa Tanzania ambao diyo wamebeba zigo la kodi isiyotosha kitu kwa mahitaji muhimu ya binadamu wa Tanzania achilia mbali maendeleo?

Unachokifanya hapa ni unafiki na propaganda ambazo haziwezi kuwa mbadala wa utawala bora unaolalamikiwa. Ninatamani uje uugue hapa uende hospital ukose hata drip ya maji kwa kuwa hazipo ili ushike adabu. Naona kama unaongea ukiwa umevimbiwa. Njoo huku ukutane na vibaka wakuvue hadi huo mkanda unashikilia suruali yako wakuache mtaroni na kuiba laptop yako kwa kuwa hakuna ajira na maisha magumu ndipo utajua kuvimbiwa ni dhambi.

Fika hapa umpeleke mkeo kujigungua akose huduma ndipo ukapofahamu madhara ya unafiki wako.

Kujitegemea kunakujaga kwa makelele ya kinafiki, adhabu ya utawala mbovu au ni mipango inayopangwa na kutekelezwa kitaalamu kwa kupunguza degree ya dependency gradually hadi hapo inapokuwa zero?

Acha upumbavu wako wa kinafiki hapa. Wewe haupo Tanzania unaimba nyimbo kikasuku kwa ujinga huku wanaoumia ni wengine. Ninatamani hata huko uliko mfukuzwe ili uje uone madhara ya ushenzi wa kutetea utawala mbovu na uonevu wa raia. Halafu ndipo uanze kuleta uharo wako kwamba tujitegemee bila maandalizi.



 
Wanaompinga Mwanakijiji wanafanya hivyo kwa sababu za kisiasa tu na si uhalisia.....

Na wengi wanaompinga ni washabiki wapya wa CDM waliokuja na Lowassa.....huo ndio ukweli.
 

Kama hayo unayoyasema ni Ukweli wenye kupanga njama za kuiba uchaguzi wangekuwa Lupango sasa hivi, hizo unazozisema ni conspiracy theory!

Eti kwa kuwa Zanzibar walielekea kushindwa, wakifuta uchaguzi unaona sawa kwa kuwa " Waliiba".

Lakini kumbuka hata huko Zanzibar kuna kura za Raisi wa Muungano, Nikuulize swali, Je nazo waliiba ngapi?, Iweje basi waiba uchaguzi wa huko Zanzibar ambao kimsingi ni walewale tu wa nchi nzima waibe za Raisi wa Zanzibar lakini wasiibe na kura za Muungano kwa upande wa Zanzibar?
Vipi uchaguzi wa Raisi wa Muungano na Wabunge kwa huko Zanzibar uwe sahihi kwa muktadha huo?
 
MM, hili halihusiani na kujitegemea acha kupotosha. Halikufanywa au halikutokea kwa sababu tunataka tujitegemee. Zipo nchi zinajitegemea na bado wanapata misaada. Ni kupotosha kwa makusudi kufikiri kuwa tanzania tulikiuka vigezo vya MCC ili tukose package ya pesa za Changamoto za milenia ili tuanze kujenga mazingira ya matayarisho ya kujitegemea. By the way, wewe uko US, huwez ona madhara kukosa hela hii, ambayo masharti yake siyo magumu!

Sote MM tunakubaliana umuhimu wa kujitegemea, lakini siyo kwa style hiyo unayotaka kutuaminisha!
 
Mkuu, naamini kila mmoja angependa nchi yetu ijitegemee, lakini bado tunazo changamoto, ni hatua siyo suala la muda mfupi. Jana tumeahidiwa mkopo wa Tsh 100bn> wa masharti nafuu kutoka Japan. Maana yake ni nini, ni kuwa bado tuna changamoto ya rasilimali pesa.

Hivyo kuhusianisha kukosa pesa za MCC kuwa ni kwa sababu tunefanya hivyo kwa nadharia ya maandalizi ya kuanza KUJITEGEMEA, hilo si kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…