Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Mkuu samahani kama ungekuwa unafuatilia uzuri ungeona nani aliyeleta suala la ushoga kwenye majibu yangu. Kwa kweli naafiki huo uungwana wako, sote tupo huru lakini tuchunge ndimi na mikono yetu, maneno mabaya sio mazuri kwa viumbe mwenzio. Pole saana, natumai sijakukwaza.
 
MMM hili povu linalowatoka leo mbona hamukuanza kulitoa miaka 10 nyuma?
Wakati wabunge wa upinzani wakipinga safari za JK kwenda ughaibuni kuomba misaada si nyinyi ndio mlisema hawaitakii mema nchi yetu?
Leo ndio mmeshituka akili baada ya kunyimwa misaada? (Kumbuka tumenyimwa na sio tumeikataa)
Mkiwa mnazungumzia kukatwa kwa misaada ya MCC kuweni wazalendo kwa kutaja pia kwamba sababu za uhuni wa ccm Zanzibar ndio chanzo chake!
 
Mzee Mwanakijiji matamko yanayojitokeza baada ya kunyimwa nayafananisha na sizitaki mbichi hizi, pamoja na maelezo yako swali bado linabakia kwa nini tumenyimwa fedha za MCC je ni kwa sababu sasa Tanzania tunaweza kujitemea bila msaada?

Swali la msingi ni je tuliwaambia hatutaki au tuliambiwa hatutapewa??? ni vizuri kuanza mazoezi ya kujitegemea kiuchumi pamoja na hayo si jambo jepesi na kwenu ninyi msiokaa Tanzania hamtaelewa haya.
 
Hii nchi bwana viongozi wetu wasanii sana, utasign vipi mkataba ambao huwezi kuutekeleza? moja ya masharti ya mkataba wa MCC ni pamoja na kudumisha demokrasia nchini, hayo yote ni mambo ambayo yamo ndani ya huo mkataba ambao mlikubali wenyewe, tujifunze kutekeleza kitu ambacho tuna kisign sio kuja na issue ambazo hazina uhusiano hii ni kuumiza jamii wakati nyie mnaendelea kula mapocho pocho wakati huo mitaani kumekauka.
 
Kwani Seif alipotangaza kura zake, ilizuia vipi tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendelea kutangaza matokeo!?
Tume haikuendelea kutangaza sababu matokeo yalichezewa...na matokeo ya tume ni tofauti na ya Seif.
 
Masharti ya MCC yalikua wazi lakini bado tukaapply? na tuliapply huku tukijua tunaenda kubaka demokrasia... Pathetic!

Well sipendi misaada ila yaliyotokea Zanzibar ni hatari hata zaidi ya hiyo misaada yenyewe!!
 
Kukosa msaada sio hasara.
 
Waruhusu bangi NA madawa ya kulevya NA mirungi wala atuitaji kumtegemea mtu
 
Tume haikuendelea kutangaza sababu matokeo yalichezewa...na matokeo ya tume ni tofauti na ya Seif.

Nnaona unazunguka zunguka tu na kujibu kijumla jumla, yangu macho kwa huko tunapo elekea na ahadi ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati...

CCM Mmejisahahu mnadili na mabeberu...
 
Kukosa msaada sio hasara.

Wakati mwingine uache utani kwenye mambo makubwa, kama huna hoja si vibaya ukakaa kimya? Tuambie hasara ni nini? Huwa tunatofautiana kwa itikadi na nilikuwa naheshimu michango yako maana hoja nilikuwa naziona hata kama sikubalini nazo. Lakini huku unakoelekea naona unatoka kwenye utu uzima unarudi utotoni.
 
Kukosa msaada sio hasara.

Hasa kwa wanaoshindwa kufunga vifungo vya mashati yao kutokana na shibe wanazozipata chini ya mgongo wa CCM, na mzigo mkubwa tupo 'punda' tutaubeba bila maswali.

Poleni sana makabwela wenzangu...
 

Huwezi kuamini huyo mzee mwanakijiji nimemuomba arudi nyumbani aje atupatie na sisi huo ujuzi aliochuma huko nje ili kama taifa tufaidike, hata kunijibu hajathubutu na nimemuomba zaidi ya mara tatu. Ila namuona anajibu vijembe tu. Hawa akina mzee mwanakijiji ni wale wachezaji wanaoona makosa ya wenzao wakiwa nje ya uwanja lakini wakiingia ndani inakuwa aibu. Anajaza minadharia hapa jukwaani, ukimwambia njoo nyumbani tutumie hayo mawazo yake anakaa kimya. Si unafiki ni nini huo?
 
WanaCCM tumeshaeleza wazi kuwa hatuna shida na vijimisaada vyenye masharti. Hili hata mstaafu Kikwete alilizungumza na sasa rais Dkt Magufuli anazidi kulikazia.

Ni marais wawili tu walioamini katika kujitegemea nchi hii. Baba wa Taifa na kitukuu chake Magufuli. Wengine wote hapo katikati hawajawahi kujiamini kama wanaweza. Na hili suala sio la CCM, maana CCM ilikuwepo hata wakati wa Kikwete. Hili ni la MAGUFULI.
 

Kujiamini tu kuwa utajitegemea bila mipango inayoonekana hiyo itakuwa kazi bure, suala la Uchumi ni kanuni sio siasa mkuu..

Na mpaka hapa mh raisi amesha feli..... muda utaamua.
 

Mkuu hawa jamii ya watanzania waishio nje ya nchi hawajui kabisa tunapitia changamoto zipi katika maisha. Ila wanapenda sana kujiachia nyuma ya computer na nadharia zisizotekelezeka.

Huwezi tu kuanza kusifia kunyimwa misaada bila kueleza tutawafikia vipi wananchi walio wengi waliopo gizani. Nini mbadala wa Trilioni 1 ya MCC???
 

Ndugu yangu wacha tu, watu wanapiga siasa hapa, ukiwasikiliza hao viongozi ndio utabaki kinywa wazi, wakija hao madiaspora utatamani hata kutapika. Leo uniambie eti hutaki 1trilioni zenye masharti ya kutii demokrasia, halafu ubaki unakimbizana na 2b tshs za mkwepa kodi wa makontena manne!! Hao madiaspora ukiwaambiwa waje watekeleze hayo manadharia yao hapa nchini akija wiki moja kuzika tu, wiki inayofuata karudi kwa wazungu. Ukimuuliza mbona unaondoka haraka hivyo anakuambia huku maisha ni hovyo sana. Sasa si wayabadilishe hayo maisha ya hovyo, wanabaki kupiga vijembe vya kiingereza visivyo na msaada kwa mkulima wa tandahimba.
 
Msiwe na Wasiwasi na hizo fedha za MCC. Rais wetu mpendwa alishasema TANZANIA YA VIWANDA INAKUJA!
 
Pamoja na kwamba ninaunga mkono HOJA yako (either uwe uliianza siku nyingi au le, kwangu mimi hilo sio muhimu) lakini ni vizuri pia tujikite kwenye kisababishi ya kuondolewa hiyo inayoitwa misaada. Nini msimamo wako kwa kile kilicho tokea Zanzabar? Lakini pia tukumbuke hivi, rais mstaafu wa awamu ya 4 alikua muumini mzuri sana wa kuamini katika misaada, ilifikia kipindi watu wakaanza kukumbuka nukuu mbali mbali za maias waliopita kuhusu misaada na kumlinganisha na yeye, ukweli kwake iliishia kua matusi tu; kama kumbukumbu zangu zitakua zipo sawa, ni kama na yeye alianza kutuandaa kisaikolojia kua tuanze kujitegemea, na kama kumbukumbu zangu zitaendelea kua sawa basi nakumbuka kuongezwa kodi ya Mafuta ya jamii ya Petrol ili tujitegemee (hi ni miongoni mwa sababu zinazo sababisha Tanzania bei ya mafuta kuendelea kua juu ili hali sokoni yameshuka). Kinacho nihuzunisha ni hiki, JK, Magufuli pamoja na wewe mwenyewe MMM ni kutwambia tujitegemee bila kujali kisababishi. JK alituandaa hivyo mara baada ya Wazungu kutishia kuto kutoa pesa kwasababu ya mambo ya Escrow, Kafulila alitaahadharisha hili JAMBO bungeni wakati mambo ya Escrow yanachangiwa, aliyekua waziri wa fedha bi Saada Mkuya na profesa Muhongo wakabisha, KIKO wapi leo? Haya jambo la Zanzibar ndio hilo, hakuna mwana ccm yeyote anayetaka kuligusua akiliunganisha na hilo la kukatiwa misaada kwamba ndio kisababishi, wote tunaimba wimbo wa kujitegemea. Nakumbuka Mbowe akiwa Denmark alitoa hotuba iliyo shiba sana na akaizungumiza hiyo hiyo misaada, aliponda sana, wengine walimlaumu sana na kuonekana haitakii mema Tanzania. Leo wale wale waliokua wakimponda Mbowe ndio hao hao wanaosema tujitegemee! Tusubiri KODI mbali mbali kuongezwa ili kufidia PENGO. Yetu macho,
 
juzi japan nao wametugea bilions kama 116 hivi hizi safii eeh....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…