Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Mbona ni kama watu hamtaki hata kusoma tunachosema; hatujasema misaada haiitajiki...

Ni kwa nini wakati huu tu ndio muone hamtaki misaada!!? Kwa nini sasa!?. Au baada ya awamu ya tano kuingia madarakani na hazina nayo imejaa kimiujiza!!? Kwa nini hamsemi ukweli wa uhuni mlio wafanyia wananchi, na sasa wananchi ndio wanalipa gharama za uhuni wenu!? Tunajua ninyi ni wakubwa mtatuumiza kugharamia anasa za maisha yenu, ila ipo siku tu....
 

Misaada ikikatwa itatulazimisha kuamua nini tufanye nini, vipi, na kwanini. Kwa kadiri ya kwamba tunakinga mikono hatufikiri kupanga wala kuchagua. Ndio maana kuna watu wameanza kulalamika ati hela sasa inabidi waanze kuipangia bajeti kwa sababu Magufuli anabana kila kona! Of course!
 
Mwanakijiji
You can't eat your cake and have it. Kubali tu Sikuhizi unauona ukweli nusunusu

I am right 99.99% of the time. Ukichagua upande kinyume na mimi una uwezekano wewe umekosea. Naongeza hasira za wakosoaji wangu tu...
 
Tanzania inayojitegemea inawezekana
 
Huyo mpumbavu mwanakijiji yuko us. Anaongea nadharia tu. Hana hisia jua linawakaje huku uwanjani.
C ndo hapo mkuu? Mtu unashindwa kuwafikiria babu na bibi yako walioko kijijini ambao bado wanatumia vibatari.. Bongo bado tuna safari ndefu sana ya kujitegemea wenyewe kutokana na hili janga la viwanda mfu
 
Ni kweli mkuu ulishasema. Ni kweli pia wengi tulilaani vikali utamaduni wa kuombaomba uliokuwa ukipaliliwa na serikali zilizopita.
Tatizo kuna watu wanajisahaulisha kwa makusudi misimamo yao ya awali. Mbaya zaidi wanalazimisha kila mtu abadilishe misimamo yake ya awali ATI ili tufanane wote.
Toka tulipoletewa yale mabadiliko ya kuzungusha mikono tumekuwa majuha kwelikweli.
 
Kujitegemea ni jambo zuri sana, wengine tulishasema siku nyingi kwanini hatupangi bajeti inayolingana na mahitaji yetu?

Kwanini tunasubiri kutembeza bakuli?

Tulilaani sana utaratibu wa kuzunguka duniani na bakuli badala ya kufikiria nanma ya kujikwamua. Wakasema, ziara za Rais zina manufaa ikiwemo MCC

MM, kuna kitu kinaitwa 'Weaning' kule SUA na Muhimbili watanisaidia.
Weaning si tukio ni hatua. Kinachoonekana tumeifanya tukio.

Kwasababu hatufuati kanuni za 'weaning' jana wametumabia hatutaki misaada, tunaweza wenyewe ,tuwe Wazalendo.

Leo wameacha Uzalendo wanashangilia Japan kachaingia bajeti

Unaona kwanini wengine tumesimama katika uzalendo na si kuburuzwa tu kila asubuhi

Unaona kwanini tunasema MCC hawana hatia.
Tuliomba, wakaweka masharti tukakubali wakamwaga pesa tukashangilia!

Leo tumeshindwa masharti wamegoma na pesa tunasema wanatudhalilisha.

Haya ni kwasababu tunaongozwa tu na watu wasiojua kesho kuna ni!

Wanafeli
 
Kama kweli mi saada si kitu kwetu kwanini iwe habari ya mjini tunaongozwa na viongozi wenye empty mind kiingeleza tu shida utaperi na uhuni umetawara kwa mtu mweusi marekani wa metuunga mkono wanyonge ambao atukupiga kura kwakua haki imekandamizwa kilamtu analijua ilo Tanzania sio ya watu wachache yakwetu wote? Naamini hatufiki popote bira msaada mapato na matumizi vinapishana runakusanya kodi vizur matumizi hayaendani na kodi nipo apa kama mtu ajarudi kupiga mogoti
 
Hivi Kyoma huyu Salim alikosa msaada wakati wa Wahutu na Watusi leo anawezaje kuwa msaada wa Darfur ? Je kama nikisema kaitwa kule kwa sababu wanao waua waafrika wenzetu ni waarabu wenzake wewe utasema ndiyo akili hiyo ???

Ulivyoandika hapo ni kama vile serikali ya magufuli ndio imezikataa pesa za MCC wakati ni kinyume chake.

NI kweli kujitegemea kuzuri lakini kunahitaji maandalizi kusilazimishwe na kukataliwa msaada. Kwa hili la MCC watakaoumia ni wale babu zetu Nanjilinji na kwingineko wanaoutumia vibatari na yule mkulima ambaye nyanya zake zitaozea shambani kwa kukosa usafiri kwa kuwa barabara ni mbovu na si wanasiasa wanaoongea upupu majukwaani kujilisha upepo.
 
Leo Lowassa akitoka na kusema "misaada inahitajika kweli kweli" wazungusha mikono watadandia kwa haraka kweli; "tunataka misaada tunataka misaada". Sisi wengine ambao tumepinga misaada na tunaendelea kupinga misaada tunaonekana tumebadilika.
 
C ndo hapo mkuu? Mtu unashindwa kuwafikiria babu na bibi yako walioko kijijini ambao bado wanatumia vibatari.. Bongo bado tuna safari ndefu sana ya kujitegemea wenyewe kutokana na hili janga la viwanda mfu
Kwani hao bibi na babu yako wameanza kuishi kijijini mwaka huu? Miaka yote umewafikiria kwa misaada what happened?
 
Wacha wee!! Nakuapia kwa jina Mungu aliye hai hata kama wewe ni mfuasi wa shetani basi nakuhakikishia kwa jina la Lucifer nafsi yako haitokaa na amani kamwe mpaka siku mzoga wako unafukiwa shimoni. Pesa imekuharibu wewe na padre mzinzi daktari wa canon law. Mlaaniwe nyinyi na vizazi vyenu vyote.
 
Kwa hiyo kunyimwa fedha za MCC ndio starter ya kuanza kujitegemea sio ?
 
Leo Lowassa akitoka na kusema "misaada inahitajika kweli kweli" wazungusha mikono watadandia kwa haraka kweli; "tunataka misaada tunataka misaada". Sisi wengine ambao tumepinga misaada na tunaendelea kupinga misaada tunaonekana tumebadilika.
Mkuu
Naona unamuiga Makonda ukidhan utapata u RC
 
Mkuu
Naona unamuiga Makonda ukidhan utapata u RC
Huyo na Dr Mihogo walishalipwa mgao wao tangu mwaka jana, kwahiyo hapo anamtumikia kafiir.

Kwa sasa Mwanakijiji kwakuwa ni msukuma basi na ukabila umemjaa kwahiyo kwa Magufuli ni pot pot na hana dosari, nchi imejaa wanafki hii.
 
I am right 99.99% of the time. Ukichagua upande kinyume na mimi una uwezekano wewe umekosea. Naongeza hasira za wakosoaji wangu tu...
Zamani ulifanikiwa kuziteka akili zetu kwa 100% lakini sasa, watu wanajitambuwa muulize hata njaa kali mwenzako Majid Mjengwa atakueleza.
 
I am right 99.99% of the time. Ukichagua upande kinyume na mimi una uwezekano wewe umekosea. Naongeza hasira za wakosoaji wangu tu...

Duh!

Unamshinda hata Rush ambaye yuko documented to be almost always right 99.7% of the time😀.

 
Mkuu Mwanakijiji, don't be disingenuous please! Unafahamu fika (unless you have been infected with the "CCM" disease) kwamba kinachowasukuma Watanzania wengi kufurahia huu uamuzi wa MCC siyo suala la sisi kunyimwa huo msaada. In fact, nadiriki kusema Watanzania wengi wana chuki dhidi ya dhana ya sisi kutegemea misaada - wanachama wa CCM na hata Wapinzani wengi tu. Issue hapa ni sababu za sisi kunyimwa misaada. Be truthful and tell us if you truly believe CCM didn't commit foul in the Zanzibar election saga, and deserve MCC's rulling. Tell us if you really think the Cyber Security law passed by CCM is not undemocratic, to say the least. Come on Brother! You used to be my model!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…