URUSI amebadili malengo ya hii vita. Awali alitaka kutumia bajeti kubwa kwa muda mfupi kumaliza SMO.
Ukrain mwanzo alionesha kuhimili makali ya urusi kivita ila mpaka Sasa imethibitika kufirisika kijeshi, silaha hata mbinu.
Hali ambayo inapelekea kuendesha vita kupitia misaada ya siraha, vifaa, inteligensia na hata mamluki.
SUPER POWER URUSI
Kupitia operation hii kwanzia mwanzo mpaka Sasa urusi anaonekana ni super power kwa siraha, dhana za kivita, teknologia katika uwanja wa vita.
Amethibitisha kuwa anaweza kupigana vita na NATO kwa hoja kuu mbili
1. Number of troops on battlefield
urusi ame-deploy idadi ndogo sana ya wanajeshi wake ambao constantly wapi vitani. Hii itakupa ratio kubwa sana kati ya namba ya ukrain+mamluki na yeye urusi pamoja na wagners kwenye uwanja wa maambano.
Hiki ni kipimo muhimu sana Cha umahili wa jeshi lako katika vita..... Uimara wa majeshi ya ardhini ya urusi ndio mafanikio yake
2. Matumizi/utegemezi wa siraha wakati wote wa vita.
Tazama mataifa mengi sana yanatoa msaada kupeleka ukrain siraha toka vita imeanza. Lakini mpaka Sasa hakuna taarifa yakuaminika pasina shaka kwamba urusi anapewa msaada toka kwa yeyote zaid ya drone za Irani ambazo zilipelekwa kufanya majaribio na baadae zimepotea.
3. Jambo linguine lakushangaza, urusi yupo vitani mwaka wa pili huu. Uchumi wake Bado upo imara sana. Tazama JUZI tunaambiwa amerudi top 10 ya nchi zenye uchumi wa juu huku akiwa vitani. Hii ni kuonesha kuwa Russia anamizizi isioweza kuteteleka jeshin. Wengi wamepingi takwimu ile ila wao IMF, WB hawajapinga mpaka Leo.
URUSI ANABADILI MALENGO YA SMO
Mwanzo wa hii operation ilikua ni kumaliza mapema hii operation, ila matokeo ya vikwazo na mafanikio makubwa ya biashara ya urusi baada ya vita ndio yamebadili MALENGO ya hii operation.
1. Mlengo mpya wa kisiasa
Putin anataka kutumia vita hii kutetelesha mataifa makubwa mahasimu. Siasa za uingereza, marekani, ujerumani na mataifa mengi yametikisika na hii vita
2. Mlengo wa kiuchumi
Baada ya kuwekewa vikwazo, urusi ndipo uchumi na mauzo yake yakaanza kuteteleka sana, japo baadae ukaibuka isivyo kawaida.
Urusi Sasa anaonesha kuwa vita inamlipa sana yeye na marafiki zake kama vile UCHINA, IRANI, MIDDLE EAST ALLIES, AFRIKA-RUSSIA AGENDA, LATIN AMERICA, na wengine wengi sana
4. Urusi ametambua kuwa, kupitia vita hii ndio kichocheo kizuri Cha Kasi ya kuidhoofisha nguvu ya Dola ya marekani.
Tazama nchi nyingi za ulaya zimeanza kubadili GIA angani kuhusu kuendelea kuisaidia kijeshi ukreni. Wameanza kurumbana kuhusu packages za vikwazo kwa urusi. Ni wao wenyewe kupitia bunge lao wamekili kwamba utekelezwaji wa vikwazo kwa urusi haujafwatwa hata kwa 60% hivyo package mpya itakua ni kuongeza misimamo juu ya utekelezwaji wa vikwazo vilivyokwisha wekwa awali na vipya vichache.
KUHUSU HAYO NA MENGINE MENGI
Tunashawishiwa kuamini kwamba urusi anamizizi migumu sana kijeshi, kiuchumi, inteligensia teknologia katika vita na itakua sahihi kumuita supapawa katika medani za kivita na si uchumi.
NAOMBA KUWASILISHA
Sent from my Infinix X6511E using
JamiiForums mobile app