Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Kumbuka hiyo ni SMO na sio war!Putin anasema hajaanza anything serious hapo Ukraine!
Hizo nyingine ulizoleta hapa ni ngonjera tu!
Hao hao analyst wa west walituzuga kuwa Urusi hana uwezo wa kuendesha SMO miezi 3,hao hao walisema Russia kaishiwa silaha miezi ya mwanzo ya SMO!Imekuja kubainika ni tofauti,so hizo porojo ni propaganda tu kuidiscourage Russia!
Tumekusikia kuwa hoja yako ni kwamba ile siyo vita bali ni SMO.

Swali langu ni moja tu. Nani tumwamini anayesema kweli kati yako na Putin?. Tarehe 09/05/2023 Putin kaitangazia dunia kuwa "It is the real war (True war).
 
Ni mpuuzi pekee atafikiri wababe hawa wakae sehemu moja kisha utoke salama. US, UK, German, France, Italy. Hasa hasa US na UK. Huko kuna watu bright kweli kweli hasa ktk Inteligence. Hapo weka mbali washirika wao wa mbali kama Israel, Japan n.k hizo Race za Asia nazo ni vichwa kweli kweli.

Tukumbuke pia US mpaka Warusi wapo, Wachina n.k. Watu wanachukulia simple uwezo wa US ktk nyanja nzima ya Tec na Vita.
Kwa hiyo hoja yako hapa ni kwamba
1. Russia hawezi kupigana na USA, Germany, Italy, UK, France and allies na akashinda vita.

2. WW3 haiwezi kutokea sababu Russia hawezi kuyapiga mataifa hayo makubwa kama tulivyoaminishwa kabla ya vita
 
Tumekusikia kuwa hoja yako ni kwamba ile siyo vita bali ni SMO.

Swali langu ni moja tu. Nani tumwamini anayesema kweli kati yako na Putin?. Tarehe 09/05/2023 Putin kaitangazia dunia kuwa "It is the real war (True war).
Ikianza vita kamili mtakuja hapa kulialia sijui war crimes NK!
 
Tuliwahi kusema humu ndani, hii vita imekuwa well calculated na Magharibi before and after.

Wanamjua Putin ana Nuclear ila mpaka wakafikia hatua ya kumsapot Ukraine na kutupilia mbali vitisho vya Putin, maana yake kuna namna wameshajua wanamuweza.

NATO ilishasema wameweka bajet for 5 years. Wajinga wakabeza, wakasema kwa nguvu ya Russia, vita haiwezi kumaliza mwezi.

Hakutakuwa na WW III, ila kwa hesabu hizi za NATO, wataidondosha serikali ya mabavu ya Putin na watu wake wa kijamaa.
Hoja yako imeeleweka kwamba,
1. Hakuna uwezekano wa kutokea WW3 sababu NATO amejiandaa vya kutosha kumkabili Russia.

2. Russia hawezi kuwa Super power sababu itapigwa na NATO na serikali ya Russia kudondoshwa.
 
Kwa hiyo hoja yako hapa ni kwamba
1. Russia hawezi kupigana na USA, Germany, Italy, UK, France and allies na akashinda vita.

2. WW3 haiwezi kutokea sababu Russia hawezi kuyapiga mataifa hayo makubwa kama tulivyoaminishwa kabla ya vita
Uzi ungeuedit na kudeclare wewe ni Pro west!Hoja za upande mmoja unaziunga mkono bila kuzichallange na za upande mwingine unakaza shingo!
Endeleeni kujifariji,Russia ni habari nyingine!
 
Nimepitia comments zote naona hakuna comments za maana hasa kwa pro NATO/US.

mtoa mada ungeleta kiini cha vita hii na objectives za Putin au Russia kwa ujumla ili tuone je

1. Urusi imefikia malengo yake?

2. Je ikiisha kwa sasa nani amepoteza?

Jambo la pili naona watu wanazungumzia Urusi kuishiwa silaha sijui kuwa dhaifu. Lakini hakuna anayeweka takwimu zozote kuonesha ni namna gani silaha zao zimepungua?

Jambo la tatu hakuna anayesema combat readiness ya jeshi la Urusi vs wapinzani wake. Hapohapo hakuna anayesema hao wenye nguvu wanazo silaha kiasi (hivyo udhaifu inasemwa ni propaganda).

Kuna wanaosemwa marekani na washirika wanaogopa kutoa silaha nzito kwa Ukraine.... tafsiri ya huo uoga ndio nguvu yenyewe kwa Urusi. Hakuna anayezungumzia.

Vita ni inteligensia kwanza kisha combat readiness na mwisho silaha. Hakuna aliyeonyesha ubora wa intel ya Russia vs NATO/US.

Mwisho mleta mada tahari ulianza na upande mmoja hutapata hoja zenye mizania.

Swali: unaweza kutuambia kwa nini spring counter offensive imesimamishwa hadi sasa na kimsingi haipo tena.

Je unajua kilichoipata NATO main Commanding centre iliyopo Ukraine?

Ni hayo tu
1. Umetoa malalamiko kuwa watu wengi hawajadili hoja badala yake wanapiga porojo tu. Hapo nakuunga mkono 100%. Lakini cha kushangaza na wewe umepiga porojo without laying any fact(s) with evidence.

2. Umesema kuwa mtoa mada (hoja) hajatoa hoja kama unavyotaka wewe na kwa mwelekeo unaotaka wewe
Wewe unashindwa nini kuanzisha mada unayotaka ijadiliwe mpaka ulalamike kiasi hicho?

3. Inaelekea context ya hoja hujaielewa ama umeamua tu kujitoa ufahamu. Kwa nini hujajibu swali lililoulizwa hata moja na ukafanya uchambuzi wako na ukaweka facts na ushahidi.

4. Ukweli ni kwamba hoja zimekulemea ndo maana umeishia kupiga porojo tu.

Hoja hujibiwa kwa hoja siyo porojo
 
Uzi ungeuedit na kudeclare wewe ni Pro west!Hoja za upande mmoja unaziunga mkono bila kuzichallange na za upande mwingine unakaza shingo!
Endeleeni kujifariji,Russia ni habari nyingine!
Wenzako walau wanajibu hoja/maswali. Wewe umejibu hoja ipi?
Kama unapiga porojo unataka tu note porojo.
 
1. Umetoa malalamiko kuwa watu wengi hawajadili hoja badala yake wanapiga porojo tu. Hapo nakuunga mkono 100%. Lakini cha kushangaza na wewe umepiga porojo without laying any fact(s) with evidence.

2. Umesema kuwa mtoa mada (hoja) hajatoa hoja kama unavyotaka wewe na kwa mwelekeo unaotaka wewe
Wewe unashindwa nini kuanzisha mada unayotaka ijadiliwe mpaka ulalamike kiasi hicho?

3. Inaelekea context ya hoja hujaielewa ama umeamua tu kujitoa ufahamu. Kwa nini hujajibu swali lililoulizwa hata moja na ukafanya uchambuzi wako na ukaweka facts na ushahidi.

4. Ukweli ni kwamba hoja zimekulemea ndo maana umeishia kupiga porojo tu.

Hoja hujibiwa kwa hoja siyo porojo
Du mimi sileta hoja mpya na wala sikutaka kujibu hoja yeyote kwa sababu tayari mleta hoja amelemea upande mmoja kisha anataka leveled arguements, haiwezekani.

Mfano nimesema wengi ikiwa ni pamoja na mtoa hoja wanasema NATO ANS ALLIES wanaogopa kutoa silaha nzito. Hi hofu walionao ndio ukubwa wa Urusi.

Nikaweka hoja hakuna aliyesema utayari wa majeshi, ukubwa wa majeshi na vifaa vyao ili kusema Urusi imelemewa, sikuja kutoa facts nimetuhumu watoa hoja hawawek facts.

Pia intelijensia za NATO VS Russia zimelemea wapi?

Lakini kila vita ina objectives yake na ili iishe lazima hayoalengo yatimie au yatatimia kwa mazungumzo.

Pia niongeze gharama za vita zipoje kwa maana ya vifaa, rasilimali watu, fedha hali ipoje.

Mleta hoja alizungumzia uchumi lakini hakuna facts nani uchumi umepanda au umeshuka na projection zipo.

Hayo nimeyasema siku na lengo la kujibu bali kuwaambia wanaojibu pasipo facts ni sawa na kuimba singeli
 
Unastahili kupewa taji la propagandist ambaye hana uwezo wa kujenga hoja.
 
1. Umetoa maelezo mengi kweli, nimejitahidi kusoma kwa makini lakini sijaona mahala popote ulipojibu hoja au maswali niliyouliza hata moja. Kama ni penati zote umebutua nje ya goli.

2. Maelezo uliyotoa yako ki hisia zaidi (Hisia zako) kuliko uhalisia. Sijaona fact(s) yoyote zaidi ya story tamu. Propaganda imekuongoza zaidi kuliko kuongozwa na facts. Mtu akikuomba ushahidi wa uliyoeleza nadhani utatokea mlango wa nyuma na tusijue ulikoelekea.

3. Tunasubiri uje na analysis nzuri itakayojibu maswali ya dodoso kwa facts na evidence kibao. Karibu tena
Mkuu, kama hufahamu kwanini Russia iliamua kuchukua Crimea na yaikalia hadi leo.

Pia kama hufahamu ni kwanini Russia imechukua kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia, basi hatuwezi kuwa "level" moja ya mjadahala.

Naona wajitahidi sana kusahihisha watu humu ndani lakini umekosa weledi wa kutambua chanzo cha mzozo wa Russia na Ukraine akitumiwa na nchi za NATO /US.
 
Kwa hiyo hoja yako hapa ni kwamba
1. Russia hawezi kupigana na USA, Germany, Italy, UK, France and allies na akashinda vita.

2. WW3 haiwezi kutokea sababu Russia hawezi kuyapiga mataifa hayo makubwa kama tulivyoaminishwa kabla ya vita
Shekh mpaka unaona vita inashika hatamu ujue ni mioyo ya watu imesharidhia kwa 100% kutetea taifa lao.

Russians wengi hawataki vita.

1. Hii vita ni matakwa ya Putin. Na ili tu ajione anairejesha USSR.

2. Russia kungekuwa na uhuru wa utawala, Putin angeshapingwa mno kuhusu maamuzi haya.

3. Russia kule kwake magenge ya upigaji ndo yanayokula nchi, ni zile familia za vibopa vya USSR vimejimilikisha nchi, hakuna uzalendo tena kama zamani ila vyombo vya habari vinampamba tu lakini uhalisia haupo.
 
Napata tabu kujua unajibu hoja au swali lipi. Maana umeupiga mwingi lakini haufiki golini. kwenye kujibu hoja unatakiwa hoja uifikishe kileleni ili ieleweke zaidi. Kwa hiyo hoja yako ni kwamba;

1. Russia hawezi kushinda vita sababu wananchi wake wanapinga/hawataki vita ni matakwa tu ya Putin. Unaweza ukatupa ushahidi au analytical facts kwenye hili.

2. Russia hawezi kushinda vita sababu wapiganaji (Troops) wake hawana motisha ya kupigana vita, ni utashi wa Putin na genge lake. Unaweza ukatupa ushahidi au analytical facts kwenye hili.
 
Hakuna proof yoyote sababu vyombo vyote vya habari Russia vimefungwa.
 
Hakuna proof yoyote sababu vyombo vyote vya habari Russia vimefungwa.
Ulijuaje sasa kuwa wananchi wa Russia hawataki vita. Kwa hiyo kumbe ni mtizamo na maoni yako tu
 
Tangu Putin atangaze Special Military operational yake Feb 2022 dhidi ya Ukraine, wengi waliamini kuwa huo ndo ulikuwa mwanzo wa vita kuu ya tatu (World War III) hasa Marekani na NATO walipoweka wazi kuwa wataisaidia silaha Ukraine ili iweze kujilinda dhidi ya mvamizi (Russia).

Marekani alipozishawishi nchi za EU kuisaidia Ukraine, fikra za WW3 ndo zilikolea kwa watu wengi (Pro-Russia na Pro-Ukraine).

Kinachoendelea sote tunaofuatilia vita hiyo tumekiona na tunajua, sina sababu ya kueleza.

Waliokuwa wakiamini kuwa hiyo vita ni mwanzo wa WW3 walikuwa na sababu muhimu zifuatazo;

1. Waliamini kuwa Russia ni super power na kwamba ina uwezo wa kupiga nchi zote ikiwemo marekani.

2. Waliamini vita ya Russia na Marekani itakuwa vita ngumu sana na wengine wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Marekani akiingilia ugomvi wa Russia na Ukraine ndo utakuwa mwanzo wa Marekani kupigwa na kusambaratishwa na super power aitwaye Russia.

3. Pro Russia na hata viongozi wa Russia waliamini kuwa Russia ina uwezo wa kumpiga Marekani kwa makombora yake anayoyaitwa Intercontinental Ballistic missiles, Hypersonic missiles na Nuclear missiles. Eti Kwamba Russia makombora yake ni hatari sana na ya technology ya hali ya juu sana.

4. Sababu nyingine ni kwamba waliamini kuwa Russia ana air defense systems hatari sana wakiwa wanarejea S-300 na S-400 series. Kwamba anga la Urusi linalindwa sana huwezi kupenya na kwamba marekani hana air defense systems kama za Russia.

Katika kutafakari na kufanya assessment kuhusu hali halisi ya kinachoendela katika vita ya Ukraine na Russia. Tunahitaji kujua kama kweli watu walichokuwa wanafikilia kimekuwa kweli au kimeenda kinyume chake kwa kujiuliza maswali yafuatayo.

1. Je, bado tunaamini kuwa vita ya Ukraine na Russia itazaa vita kuu ya tatu ya Dunia (World War III) ?

2. Ni kweli Russia ni supper power kama watu walivyoamini kabla ya vita kuanza ?

3. Ni kweli Russia ana uwezo wa Kuipiga Marekani na nchi zingine Duniani na pengine kuitawala Dunia.

4. Ni kweli Russia and air defense systems za hatari kuliko marekani na nchi yoyote duniani na kwamba anga lake liko salama hakuna kitu cha kupenya kwenye anga lake?

5. Ni kweli Russia ana silaha nzito za kutisha na zenye kutumia technology kubwa kuliko marekani na nchi zingine?

6. Ni kweli jeshi la Russia liko imara sana kama ambavyo tuliamini mwanzo na kwamba wana mafunzo imara ya kutumia silaha za kivita?

Tupate maoni na tafakari yenu bila matusi na ushabiki usio na hoja yenye mantiki. Tusitawaliwe na u pro-Russia au Ukraine tukajikuta tumetoka kwenye hoja.
Inawezekana pia
 
Umesema propaganda ndo Inaendesha vita Ukraine na siyo uhalisia. Cha ajabu na wewe umechangia ki propaganda badala ya facts, hapo ndo umeniacha hoi.

Binafsi ningefurahi kama ungejikita kwenye kujibu maswali ya dodoso ya hoja uliyopo mezani.

1. Hebu tueleze uhalisia ukoje? Na uje na takwimu kudhibitisha uhalisia unaoujua ili na sisi tuelimike.

2. Hebu tupe uhalisia wa nchi ambazo NATO walienda kuzichapa baada ya kuona zimekuwa dhaifu. Na nani alizifanya hizo nchi kuwa dhaifu kabla ya NATO kwenda kuzichapa.
Hata wewe mtoa mada umeileta kishabiki tatizo limeanzia hapo
 
Hata wewe mtoa mada umeileta kishabiki tatizo limeanzia hapo
1. Hebu tuonyeshe ni swali gani au hoja ipi iliyokaa kishabiki?

2. Kama hoja ni za kishabiki, ikiwa na maana zimekugusa upande wako, kwa nini hujatoa uchambuzi (analytical facts) ili kujibu kwa kutetea upande unaoona wewe haujasemewa. ? Hoja hujibiwa kwa hoja siyo porojo.
 
Back
Top Bottom